Mwachiluwi
JF-Expert Member
- Mar 10, 2022
- 25,258
- 48,589
Huwa sipendi kusoma story za kuuzunisha zina niletea kumbu kumbu mbaya sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
,Shunie ,Nakadori ,IBRA wa PILI ,Antonnia mkuje nyingine hiiGood afternoon brothers and sisters [emoji112]
Based on a true story!
Mimi nafanya kuiwasilisha kwenu, hivo fuatana nami mpaka mwisho.
Mimi naitwa Alphonse ni kijana niliezaliwa miaka 36 iliyopita yaani 1986 huko mkoani Kilimanjaro katika hospital ya KCMC. Kwetu tupo watatu mimi na dada zangu wawili, wa kwanza Anna alizaliwa 1988 na mwingine Agness alizaliwa 1992. Baba ni mchaga wa rombo useri na mama ni mchaga wa marangu kirua. Baba alikuwa mfanyabiashara mkubwa hapa jijini Arusha wa vitambaa maeneo ya kilombero na mama yeye alikuwa mtumishi yaani mwalimu katika shule ya Arusha Secondary School kifupi Arusha sec. Tulikuwa tukiishi sakina maeneo ya silentini ndipo wazazi walipojenga.
Maisha yetu kwa kweli yalikuwa mazuri sana hapakuwahi kuwa na shida nyumbani upendo ulitawala na ndugu walitupenda sana na kila tukifunga shule basi bibi wa huko kijijini wa pande zote kila mmoja alikuwa anang'ang'ania tukakae kwake. Shule tulisoma nzuri mimi nakumbuka nilisoma st. Constantine iliyopo Arusha, shuleni tulienda kwa school bus na kurudi kwa school bus. Hata shuleni kulikuwa na tour za kwenda mbuga za wanyama mbali mbali na vivutio vingine nchini.
Kwa kweli shida sikuwahi kuzijua maana nyumbani tulikuwa hatuli maharage na dagaa maana mama alikuwa na vidonda vya tumbo. Nakumbuka hata nguo nlikuwa nafuliwa na dada wa kazi ambaye alikuwa mwenyeji wa Singida. Asubuhi ilikuwa lazima tule cornflex na maziwa. Nilikuwa mtoto wa geti kali hata kucheza ni ndani kwa ndani tu.
Mwaka 1995 nakumbuka nikiwa shule alikuja mjomba shule hivyo niliitwa ofisini kwa mwalimu mkuu nakuambiwa nirudi nyumbani. Tuliondoka na mjomba kwenye gari aina pegeout mpaka nyumbani ambapo kulikuwa na watu wengi tayari, sikujua nini kinaendelea kwa hiyo mimi na wadogo zangu tulikuwa na mjomba muda wote, ndipo baadae alipokuja baba mkubwa na kutuambia baba na mama hawapo tena! Mdogo wangu aliuliza wamesafiri watarudi lini? Alijibiwa hawatarudi tena na sasa ninyi ni jukumu letu.
Mimi sikuielewa na hakuna ambaye pia alielewa tukazidi kuhoji na tuliambiwa tu wameenda mbinguni kwa Mungu. Bado kwetu kuamini na kuelewa ilikuwa ngumu lakini tulienda kuzika Rombo na huko tulilia sana ila mdogo wetu wa mwisho Agness yeye wala hakulia ni kama alikuwa haelewi kinachoendelea. Mazishi yalikamilika hakuna aliyekuwa na nawasi wasi sana ila ndio hivo tulishabaki yatima bila kujijua.
Kilichobaki hapo ni mgawanyo wa mali na kwa mila zetu mimi ndio nilimikishwa mali zote za Mzee ikiwemo mashamba huko Rombo na nyumba hapo sakina. Na huko Rombo pia mzee alijenga nyumba yake. Kule kwa mama kirua pia napo mzee alimjengea mama mkwe wake nyumba.
Basi baba mkubwa ambaye alikuwa akiishi dar kwa wakati huo alisema angetuchukua tukaishi kwake huko dar na kwamba angetusomesha mpaka tutakapokuwa. Ile nyumba baba mkubwa alisema isiuzwe bali waishi ndugu zetu nayeye pia akiwa anakuja arusha aweze kufikia huko.
Sikuwahi kujua kuhusu hati ya nyumba, mafao yoyote ya mama maana alikuwa mtumishi na wala kujua kama mzee alikuwa na hela benki au akiba yoyote. Mzee alikuwa na magari 3 pegeout ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kupeleka abiria namanga, defender 110 ambayo ilikuwa inafanya kazi ya kubeba abiria kutoka mererani kaza moyo kupitia mbuguni mpaka arusha mjini na staut nyeupe ambayo ndio alikuwa akiiendesha yeye katika shughuli zake ilikuwa ikimsaidia sana. Ila baba na mama walipata ajali ndani ya hiyo staut maeneo ya mto nduruma na umauti kuwafika hapo hapo!
Pegeout alibaki nayo mjomba akiendelea na ruti za namanga na ile defender 110 baba mkubwa aliipeleka kijijini ikafanye kazi ya kubeba maziwa na kuleta moshi mjini. Statut ilibaki imekaa juu maye na ilichinjwa ikauzwa.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatilia mkasa huu wa maisha ya kweli unaosisimua na kutoa machozi.
Nakuja kwa kunyataaa asantew
Uko poa?Nakuja kwa kunyataaa asantew
Nimefika mkuu shukrani sana!
Asante sana ccy
Sana tu....pembeni pamezungukwa na migomba ....so tulikuwa tunazama humo kupiga story tukichokaNapafahamu sana...seems ulikaa siku nyingi
Huko ndani kuzuri mnoo mawe, miti mirefu na maji tirirka majira yote.Sana tu....pembeni pamezungukwa na migomba ....so tulikuwa tunazama humo kupiga story tukichoka
Tena na kaubaridi kutoka mlima meru huku maji yakitiririka basi burudani na vinanda vya ndege vinavyoingiliwa na kelele za magari juu ya darajaHuko ndani kuzuri mnoo mawe, miti mirefu na maji tirirka majira yote.
Pametulia sana
Mambo yangu hayo🤣Tena na kaubaridi kutoka mlima meru huku maji yakitiririka basi burudani na vinanda vya ndege vinavyoingiliwa na kelele za magari juu ya daraja
Chugga nilipapenda sana yaani tengeru sokoni t-shirt ni bukubuku ila ukiipandisha town huko sanawari bila 15000 huitoi dukani,Kiatu cha 5000 Tengeru ukifika Clock on bila 70000 hupati kiatu.....wazee wa fursa wanazitumia haswaMambo yangu hayo🤣
Wauzaji wa viatu viksli huwa wanawahi Tengeru sokoni 05:00 wanachagua viatu bomba kwa 10k na town wanauza kuanzia 50 hadi 90kChugga nilipapenda sana yaani tengeru sokoni t-shirt ni bukubuku ila ukiipandisha town huko sanawari bila 15000 huitoi dukani,Kiatu cha 5000 Tengeru ukifika Clock on bila 70000 hupati kiatu.....wazee wa fursa wanazitumia haswa
Saladi tena ukieka na nazi hatari kabisa, sema inabidi uziandae mapema la sivyo utakula saladi nyama (vikonokono vidogo na vyura) bibi angu alikua mkiandaa saa kumi na mbili jioni hali anahofia asile saladi nyama😂😂😂😂😂Hakikaa.. Huo mto kama mto themi..hivi ndo unaitwa hivyo..nimesahau long tym..ila hzo mboga ni maarufu..
Mboga weweHizo sio mboga ni magugu maji tu
Utakuwa mwarusha au mmeru weqe🤣Saladi tena ukieka na nazi hatari kabisa, sema inabidi uziandae mapema la sivyo utakula saladi nyama (vikonokono vidogo na vyura) bibi angu alikua mkiandaa saa kumi na mbili jioni hali anahofia asile saladi nyama😂😂😂😂😂