jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Sehemu ya 4
Nilifika arusha na maisha yangu yalianza rasmi ambapo nilikuwa nakaa maeneo ya ngarenaro oysterbay na geto jingine lilikuwa ungalimited. Hiyo nakumbuka ilikuwa mwaka 2002 ambapo shughuli kubwa pale chuga ilikuwa ni wizi. Hao ambao nilikuwa nao mmoja ni mmeru na wawili ni waarusha. Hivo kwa kipindi hicho kwa sababu mimi nilikuwa mdogo nilikuwa napewa kazi ya unyokaa. Yaani kuchumpa dirishani na kuzama ndani kuangalia vya maana nakuiba.
Nyakati za mchana tulikuwa tuderee maeneo ya kilombero na kuwapiga watu finga kuchomoa wallet zao mfukoni. Hayo ndio yalikuwa maisha ukishtukiwa mtu akiita mwizi basi sisi tunakimbilia kule mtoni hakuna anayekuja na hupati msaada maana kipindi hicho kwa pale maeneo ya kilombero mgeni ukiibiwa wenyeji hawakusaidii.
Biashara hiyo ikaendelea nikaanza kuuza bangi na mirungi ambayo ilikuwa inalipa sana maana kama gomba wachanjaji walikuwa wengi. Na stimu zetu ilikuwa lazima utumie kuberi au ugoro unachanganya kwenye mbege. Siku ya jumapili mchana nikiwa maeneo ya soko mjinga naangalia mamangulo nimkware mmoja, nilifatwa na jamaa wawili wakaniambia wanamaongezi namimi na mimi bila hiyana nilikubali. Hivyo tuliondoka hapo na kuelekea mianzini ukiwa unataka kutokea sakina. Huko niliwakuta wale wenzangu hivo tukapewa msuko na ramani nzima ya kwenda kupiga tukio kwa bensonii tajiri mmoja wa vifaa vya simu maredio tv camera n.k
Sisi tulikuwa 4 kundi letu na wale jamaa kundi lao walikuwa watatu. Msuko wa hiyo ramani ni lazima mmoja ajifanye ni mteja ile mida ya jioni, mwingine atakuwa na pikipiki aina ya baja akiangalia uelekeo wa kwenda mawingu na mwingine atakuwa na gari ambayo itakuwa uelekeo wa kwenda kilombero na wa mwisho yeye atakuwa na pikipiki nayo baja yeye uelekeo wake na mjini kati. Kumbuka tuko 7 waliobaki watatu kazi yao ni silaha tu.
Kutokana na umbo langu kuwa dogo niliambiwa niwe mteja na kwakuwa English najua hivo nitavaa nipendeze siku ya tukio na hela ntakuwa nayo ya shopping. Wengine waliingia kwenye mazoezi ya kupigwa msasa namna ya kuchezea piki piki na gari. Mafunzo yakiendelea huku pia namimi nikiendesha shughuli zangu za kimagendo na uwizi.
Ilipita miezi miwili siku ya alhamisi tulikubaliana kuwa leo ndio ile siku ya kuushinda umasikini, hivyo tulipeana moyo na kwa mtu mwenye uwoga maana ulikuwepo tulitumia bangi na kuberi ili kuondoa uwoga. Tulikaa pamoja tukikumbushana majukumu yetu na kiongozi ambaye tulimuita jombaa, yeye alikuwa ana imani sana huku akisema hakuna kushindwa jambo. Muda ulienda na ilipotimu saa 8 tulianza kujisogeza eneo la tukio taratibu huku wale wa vyombo vya usafiri wakikagua njia na kuangalia mapai wamekaa eneo gani foleni ya magari ikoje na mizunguko ya watu. Majira ya sa 9 tulipewa vidonge aina ya benzodiazepine kwaajili ya kutuliza wenge kichwani. Nilitoka kwenye gari nimevaa jeans na tshirt nikaingia ndani kwa muhindi kwa nia ya kununua camera. Ile nikiwa nachagua chagua naonyeshwa na ufanisi wake nilisikia mlio wa bunduki hapo ndani paa! Wote laleni chini!
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Duuuh