Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aah jana nilishindwa kukuelewa kumbe Krokoni?😂Ata mimi nilinunua kiatu clock on ila nilipopagundua Tengeru nikajiona boya aisee
Duh.... mbwa kala mbwaaGood morning brothers and sisters [emoji112]
Sehemu ya 8
Tulienda Njiro na kuangaza maeneo hayo, tukashuka mpaka contena na kwenda kutia nanga makaburini kule Njiro.
Huko tulishtua kwanza bangi maana vichwa tulihisi vimechoka sana na kujiboost kidogo na ugoro maana kipindi hicho kuberi ilikuwa imeanza kupigwa vita sana kuwa inaleta kansa n.k. Tulivuta mpaka usingizi ukatuijia tukalala pale pale makaburini. Kuja kushtuka mida ishaenda sana.
Tukaondoka na kwenda Philips hapo tulikutana mr x ambaye alitupa zana za kazi na gari moja kwa ajili ya tukio. Na dereva pia alitupatia wa kwake ili tusije tukamgeuka.
Hapo hatukuonana na mdosi zaidi ya mpambe wake Mr x. Alfajiri mapema kabla hata adhana haijalia tuliamua kwenda eneo la tukio, kulikuwa na geti la kuingilia pale PPF ukiachana na ile njia ya kwenda cocacola. Tulifika nyumbani kwa muhindi jumba la kifahari la ghorofa moja limepigwa vigae vyekundu juu na sio bati.
Nyumba ilikuwa na electric wires zile kuzunguka uzio wa nyumba, na mbwa watatu hawa German shepherd yameshiba kweli. Pia kulikuwa na kijana wa kazi anayelala servant kotaz.
Mimi Mroso aliinama Palangyo akapanda kwa juu ili ashike ukuta adandie( zile nyaya zikishikwa na kitu huwa zinapiga alarm zinalia) hivyo Palangyo alijitahidi asiziguse na wote mkononi tulikuwa tumevaa gloves [emoji3451] hivo hatukuogopa shoti.
Nyakati hizo ili uwende kuwaibia wadosi majumbani kwao haswa maeneo ya njiro au uzunguni kule lazima uwe na zile silencer ambazo zilikuwa zinakodishwa na Mmanga mmoja huko horohoro. Na pia lazima uwe na nyingine ambayo sio silencer kwaajili ya kuleta heshima kwanza na kutisha watu.
Mbwa zilikuwa zinaunguruma huku udenda unawatoka na wanajua kunusa balaa, palangyo hakupoteza muda alianza kufyetua mmoja baada ya mwingine, mimi nikainama mroso akanikanyaga apande ukuta na mimi nikachumpa kurukia ukuta maana nilikuwa mwepesi na nimezoea. Wote tulikuwa ndani hivyo tukaanza na servant kotaz jamaa amelala hana habari, dirisha lake liko wazi tukachukua cd moja ambayo ilikuwa imelowekwa kwenye tindikali X alafu inaachwa ikauke. Ile mnaichoma pale kama udi mnamuacha alale unono.
Tukaanza kuzunguka madirishani kuchungulia na tukapata upenyo dirisha la jikoni halikufungwa, tukakata nondo moja kwanza mimi nikaingia alafu ikakatwa ya pili akaingia mroso na palangyo. Palangyo n mroso wakaenda juu mimi nikabaki chini maana ndipo kulikuwa na chumba cha house girl. Nikajaribu kufungua, kilikuwa kimefungwa kwa ndani nikamgongea na kukohoa, yeye asijue hili wala lile akafungua hata hajamaliza kufungua vizuri mimi nilipita na teke moja mpaka ndani na ule usingizi na wenge alienda chini mimi nikamrukia nakumuoneshea upanga na akae kimyaa.
Mroso aliniita kwa jina la kazi nije juu hivyo nikamnyanyua yule dada na kupanda naye juu kule nikakuta wote washawekwa chini ya ulinzi. Muhindi alikuwa na mke wake na mtoto mmoja wa kike na ndugu zake wawili watu wazima. Huwa kwenye maisha yao hawana mzaha, kabisa mroso aliniambia mkate mkono huyo mzee wanatusumbua kutupa hela yule muhindi akasema hapana, nawapa hela na chumbani kwake na mke wake walikuwa na sanduku limejaa hela nyingi sana ni sefu kwaajili ya kuhifadhia pesa, mroso alimwambia fungua na bila hiyana muhindi alifungua, nikaambiwa beba twende tuongozane na muhindi na mke wake mpaka nje ya geti. Hivyo walitufungulia na ndani alibaki mroso na palangyo na kule nje mimi na dereva ambao tuliwaamuru walale chini. Kule ndani waliwafunga kamba na kuwafungia wote chooni na kutoka nje yule muhindi na mke wake tukawapakia kwenye gari na kwenda kuwatelekeza kule dampo napo huko huko njiro. Hivyo sisi tuliondoka na tulienda kijenge mwanama hapo tulichukua gari nyingine aina ya mazda na dereva mwingine tukaenda mpaka sekei, napenyewe tulibadilisha gari na kuingia kwenye carina nyeusi kisha tukaondoka na kuelekea kimandolu ambapo tulimkuta mdosi na watu wake. Hela zilihesabiwa na sisi tulikabidhi zana za kazi huku mdosi akitukazia sana macho. Baada ya hapo jamaa akaja kumng'ata sikio mdosi. Mdosi akasema mbona hela ni chache sana hizi hapa mgao wenu utakuwa mdogo sana, hivyo kila mtu atapata milioni 3 jumla tisa. Wote tukagoma tukiamini mdosi hatutendei haki na kwanini hakutaka kuhesabu hela mbele yetu?
Mdosi alimwita jamaa mmoja yupo kimya sana akamwambia wape hizo hela kama hawataki malizana nao. Wote tuliangaliana huku mdosi akiondoka tukaona hamna namna tukapokea na kuondoka na sisi. Kesho yake ulikuwa ni msako mkali sana wa polisi maana hela ziliibiwa nyingi sana, huku kiwango kikisemekana kuwa milioni 500 nasisi tuliambulia milioni 3 kila mmoja!
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
Ile ilikuwa chai moja ya moto sana naona anasubiri ipoe poeeMbon ile hujamaliza? Ya nyumba ya maajabu
Chukua somo hapa ukikopesha mfanyabiashara utafilisika. Nilikuwa na baangu mmoja anadai kuwa Bora kioze atupe kuliko kukopesha.Niliifanya biashara hiyo ila haikudumu maana ilikuwa ni ya mikopo sana. Hivyo nilifilisika rasmi na back to square one.
Yes Ni mpakani Kuna mto ugalla na unao mamba wengi mno. Pia asali ipokilomita 90 Ugala huko mpakani mwa Tabora na Katavi.
Dunia haiko fair kwakweli dohAsee 500M na mnapata 9M, daah.
Ndio, zipo ndugu yangu, karibu sanaNakusalimu Jane Msowoya
Zile bidhaa bado zipo?
Tunaweza kuteta pembeni unishauri?Ndio, zipo ndugu yangu, karibu sana
Mama.
Kwani nafuatiliaga hizi mambo!😕Mama.
Nipatie link ya ule uzi wa Geita kwa babu mchawi...kuna akina Yunge mkubwa na mdogo😂
Sa kama.alikuwa mwanafamilia kwa nini Alalame kufanya hizo kazi ..alitaka alelewe kama yai asifanye kazi yytesema nin, nadhani hapo cha kuhuzunisha ni kupoteza wazazi wako, mali zenu kuuzwa na huyo dingi mkubwa, ndugu kutupiana mpira kwenye kukulea na manyanyaso ya chakula. Lakn kukata majani ya ng'ombe, kuwalisha, kusafisha banda na kuokota kuni sio mateso bali ni wajibu.