Kutoka kwenye Utajiri mpaka kuishi kwenye lindi la umasikini!

Sehemu ya 13

Tulipiga vyombo sana na jamaa akasema anatoka kama nusu saa atarudi. Kweli alitoka ila alikawia kurudi na mimi nikasema niondoke zangu nikiwa nanyanyuka naye huyu hapa.

Tukaendelea jioni akasema twende Tunduma kwanza nikapaone na nyumbani kwake na nimjue na shemeji. Mi bila hiyana nikasema sawa maana si sina location, kweli tulienda kwake na kupokelewa na mke wake. Ilikuwa ni mitaa ya ng'ambo ya Tazara reli nadhani ni panaitwa Sogea kama sijakosea.

Pale nilikaa na jamaa vizuri akawa ananipa vidili vidogo vidogo na vichaneli vya hapa na pale. Shida ilianza kwa shemeji yaani mke wa jamaa alikuwa ananisumbua sana na kila nikimkwepa wapi.

Siku moja nikiwa nimekaa zangu Nakonde upande wa Zambia jamaa alikuja akaniambia kuna udhuru kidogo umetokea hivyo anaenda Mbeya Mjini kwahyo kuna mzigo wa kama milioni 5 ataniacha nao, kweli jamaa alienda Mbeya na alikaa wiki nzima. Katika hiyo wiki nzima mimi sikukanyaga pale nyumbani maana nilijua ni moto utawaka. Alirudi na hela yake aliikuta salama na faida pia ipo.

Maisha yakaendelea hivo, jamaa akaniuliza maisha sasa hivi ya Tunduma nayaonaje mi nikamwambia hayana shida.

Akaendelea utaweza kupanga sasa chumba chako mwenyewe uanze maisha ya maparangano mi nikwambia ndio. Basi akasema anasafiri anaenda Dar kwenye mishe mishe akirudi atanipangishia chumba na kodi ya mwaka mzima.

Mi nikasema sawa ila nilibaki na maswali juu yake. Hapo ukumbuke ashanisoma sina mbele wala nyuma nipo nipo tu kama gunia la uwele.

Alisafiri kweli nikabaki pale na shemeji, ikabidi sasa nimuulize shem kwani jamaa anafanya kazi gani haswa inayompatia hela hivyo. Akasema ni dalali wa viwanja na nyumba, hayo maongezi yakaishia hapo.

Shemeji alizidisha vituko na uzalendo kwa kweli ulinishinda haswa ukizingatia alikuwa amejazia ana kishundu na mipaja. Saa zingine akurembulie mara akuombe umfunge zipu ya gauni, alimradi kunitesa tu! Nilijizuia sana ila nilishindwa nikasema nitaonja mara moja tu nakuacha. Mara moja ikawa mara mbili, mara mbili ikawa kila mara nikanogewa na mke wa jamaa na alikuwa amezaa na jamaa mtoto mmoja.

Alijua kuniteka yule mwanamke na sauti yake nyembamba na lips nene nene. Jamaa naye yuko busy Dar anatafuta hela kwaajili yetu mimi nipo busy namsaidia mke wake.

Jamaa alirudi kutoka Dar na alinipangishia chumba changu kwahyo pale kwake nikahama kimoja. Ila kumgongea mke wake ilikuwa ni mara kwa mara mpaka akashika mimba na jamaa hakuwahi kujua kuwa nilikuwa nammegea mke wake.

Hakunaga siri chini ya jua taarifa zikamfikia jamaa, bahati mbaya na mwanamke pia akaniambia hataki tena kuishi na jamaa na anataka tuishi wote! Kazi kwa kweli

Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.
 
weka ndefu jomba
 
Wanawake huwa wanapenda mashetani kuliko wanadamu..huu ni ushajidi tosha
 
Wewe jamaa kweli ni mafia[emoji2]
 
Unyama mwingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…