Sehemu ya 12
Niliondoka nakurudi mwanga kisha kurudi Tabora. Baada ya kufika Tabora nilimkuta mwanamke wangu na mwanaume mwingine geto kwangu, hasira zilinipanda sana ila kila nikipiga hesabu niwafanye nini naona haiji kabisa na nguvu nilikosa. Ilibidi niondoke na kwenda mwinyi mchichani maeneo ya bar [emoji481] kupiga vyombo kidogo. Kule nlipata dokezo juu ya vifo vya kina kinehe na Mpoladuhu. Ila madelagawisa yeye alikuwa korokoroni hivyo nikaona kukaa hapa tabora nimsala tayari.
Nikarudi home mida ikiwa imeenda, kufika bado namkuta msela hajaondoka ilibidi nipambane nae sasa kiume na mwanamke akanipigia kelele za mwizi! Sahiyo tungi namimi zipo kichwani, watu wakaja full shangwe wakijua ni mwizi kweli ila bahati nzuri na pona yangu majirani ndio walikuwa wa kwanza kufika nawenyewe kutaka kujua kulikoni?
Mimi nikasema huyo ni mke wangu na nimemfumania, mwanamke naye anasema mimi siyo mumewe ila nilikuwa mpenzi na tulishaachana sasa nimekuja kumvunjia ndoa yako. Kutokana na pombe watu wakanisihi niondoke na niwe mstaarabu kesho pakikucha basi nirudi nikiwa timamu. Kwangu niliona hapakuchi kabisa nikaondoka na kurudi mwinyi nilila huko kwa tungi mpaka majogoo. Mida ya saa nne nilienda kiyungi kuvuta bangi kidogo ili akili ikae sawa, na kweli ilikaa sawa nikaenda geto isevya nikatulia zangu kimya kwa muda wa wiki nzima nawaza na kuwazua.
Usiku wa saa mbili nilitoka na kwenda kwa mwanamke, bahati nzuri nilimkuta nikamuuliza tena mara ya mwisho mimi ni mwizi na siyo mumeo? Akanijibu usinisumbue huku akifyonza kurudi ndani na mimi sikuchukua raundi nilimlima na panga upande wa kushota kichogoni kwenda kwenye sikio alipiga kelele nikamwongeza lingine akiwa tayari yuko chini ni kama naua nyoka. Kisha nikakimbia usiku huo huo na kuelekea mpaka usule. Nilikaa huko mpaka kunapambazuka, nikarudi mwinyi kesho yake pale pale bar nikaambiwa natafutwa kama shilingi kwa kumjeruhi mwanamke na mapanga. Sikujali sana nikaanza kuunga unga magari mpaka nikafika sikonge. Nililala usiku mmoja hapo sikonge likapita doria kali sana kwenye nyumba za wageni ila hawakunibaini. Kutoka nilienda mpaka chunya kisha nikaingia mbeya mjini. Nililala mbeya siku moja alfajiri na mapema kulivyokucha nikaingia stendi bahati nzuri nikakutana na jamaa mmoja wa kitambo kidogo huko Arusha. Tukapiga story sana mi nikamwambia saivi nafanya biashara ya karanga kutoka malawi kuja Tanzania. Nayeye akaniambia saivi ana miaka 2 mbeya anafanya kazi kubadili hela na kijiwe chao kikuu ni Tunduma. Nikampa hongeranna kumuuliza unaelekea tunduma sio? Akasema bado kuna hela anasikilizia basi na mimi nikamwambia tutafte eneo tukae tunywe kidogo maana tumekutana ugenini basi muhimu kukumbukana. Nakweli bila hiyana alikubali na kwasababu yeye ni mwenyeji zaidi yangu basi tulienda location kujipongeza.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho