Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 5,445
- 14,828
- Thread starter
- #481
Good afternoon brothers and sisters Sehemu ya 14
Jamaa taarifa alikuwa ameshapata, hivyo hakuwahi kuonyesha dalili yoyote kwangu ya kujua kinachoendelea. Moyo wa mtu ni kichaka na ni fumbo kubwa sana. Kiujumla nilikolea sana kwa mke wa jamaa ikafika hatua akawa mpaka anamwibia jamaa hela na kunipa na mimi kila ninapokuwa naye nilijihisi amani kwa mke wa mtu.
Siku ya ijumaa nakumbuka kuna dalili ya wingu asubuhi ya saa tatu, tumbo lilikuwa linaniuma sana yaani lile la kukata na unajisokota kama nyoka umaaji wake. Niliwaza shida ni nini haswa ghafla nilisikia hodi mlangoni, ni mke wa jamaa alifika. Nilimkaribisha nayeye alikuwa amekuja na ameleta mapocho pocho asubuhi ile kwa ajili ya chai.
Tumbo liliachia ila nilihisi sasa limekuja tumbo la kuhara ikabidi nikimbie niwahi chooni, kufika kuna mtu ikabidi kwa haraka haraka niende nyumba ya jirani niombe kuingia chooni. Lakini nikiwa kule nahisi kuhara ila vitu havitoki ndio ghafla nikatapika sana na mapigo ya moyo yakienda kwa kasi mnoo!
Nilitoka kule mwili ukiwa unatetemeka wakati narudi sio mbali na geto nasikia fujo na kama kuna zogo hpo home. Kiutaalam nilishajua kuwa kwa zile ishara basi balaa lilikuwepo mbele yangu hivyo nilisogea ado ado nichungulie kunanini? Ile kusogeza kichwa nichungulie nikasikia sauti yule kule!
Walinikimbiza sana nikiwa nimevaa bukta na singlendi, walivyoona hawanikamati wakaanza kuniitia mwizi na kwa Tunduma hawana mchezo na wezi kabisa. Kilichoniokoa na kipigo ni mvua iliyoanza kunyesha na mimi kuingia kwenye pagale moja kujificha nikiwa hoi sana.
Nilikaa pale sana nikiwaza na kuwazua sana kuwa nimenusurika, lakini kwanini waniite mimi mwizi? Na mbaya sana mwanamke wangu itakuwaje kule nyuma, hivyo lazima niangalie njia ya kurudi na kujua mambo yanakwendaje.
Giza lilipoingia nilirudi mpaka mitaa ya jirani na geto nikakutana na mama mmoja njiani nakumuuliza kinachoendelea pale kwetu! Aliniambia kwa usalama wangu nihame huu mkoa lasivyo wakinikamata hakuna rangi ntaacha kuona.
Geto pale naona pamepigwa kofuli kwa nje, nikatafta bisi bisi( komeo ni zile za kugongea misumari au ufunge na screw) hiyo kwangu ilikuwa ni kazi rahisi, na majira hayo yalikuwa mida ya 2 usiku. Bado kuna pilika pilika za majirani na wengine wananiona.
Nilifanikiwa zoezi langu na kuingia ndani nilikaa kwa muda wa kama nusu saa, nikavaa nguo zangu na kubeba hela. Wakati sijafika hata mbali nao wakawa wameingia hivyo taarifa walipata nikasikia hajaenda mbali lazima arudi, maana mlango sijafunga. Kwasababu ni giza wakashauriana twendeni tuelekee stendi tukamvizie na akirudi utupe taarifa! Kwahyo kuna jirani ndio aliuza mchongo.
Tulipishana sasa mimi niliharakisha kwenda kwake wakati huo yeye anawahi stendi kunivizia kama atanidaka huko.
Nilifika kwake kuko kimyaa kidogo, nikawa nasikilizia kwanza nijue kuna mtu au laa! Nilikaa sana pale, nikamwona kwambali jamaa anajongea wako wawili wamebebana kwenye pikipiki. Akashushwa na yule mwenzake wakapiga story zao na kujipa matumaini ya kuwa watanikamata na nitajuta.
Mwenzake aliondoka na sasa alibaki jamaa mwenyewe, akawa anafungua grili akamaliza wakati anafungua sasa mlango mimi nilimvaa na kumpiga kabali yaani roba kwa nyuma alikuwa naye si haba hivyo alianza purukushani na mimi katika ile hali ya kuona huyu atanishinda nilimchoma na bisi bisi mara tatu. Alilegea akawa analia kwa maumivu na mimi nikakimbia eneo la tukio kabla watu hawajaanza kujitokeza. Usiku huo huo mi nilitorokea upande wa zambia boda kule kunaitwa Nakonde. Na kwa usiku huwa hamna ule mwingiliano wa mchana wa watu.
Je? Nini kitaendelea usikose kufuatana nami hadi mwisho.