Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 4,994
- 9,625
Kiislam Jina John linaitwa Yahya....Ni jina ambalo limetoka moja kwa moja kwa Mungu kama zawadi aliyompa Nabii Zakariyah ampe mwanawe pekee wa kiume aliyempata katika uzee mkubwa hali ya kuwa mkewe alikuwa Tasa. Kabla ya hapo hakukuwa na mtu aliyeitwa Yahya hapa duniani. Wazungu wakaja kulibadilisha na kuliita John.Hawa akina John wana nini maana ni kama wana mtazamo fulani wa kutokubali mambo kwenda isivyo
- John Pambalu
- John Heche
- John Magufuli
- John Mnyika
- Ongeza wengine
Yahya (John the baptist) historia yake ni kuwa alikuwa akipingana na mfalme wa Roma aliyekuwa akitawala Jerusalem. Kutokana na kupinga kwake ilimpelekea mwisho kuuliwa kwa kukatwa kichwa.
Majina huwa yanafata Asili...hawa ni watu wenye misimamo isiyotingishika wala kuogopa wenye mamlaka. Wakisimamia jambo ni mpaka liwe, sio waoga na pia ni watu wanaokuwa na elimu na hekima sana katika jamii. Misimamo yao hupelekea kuingia matatizoni dhidi ya watawala na hata kufikia kupata madhara.