Hivi msitu wa Pande na Mabwepande kuna tofauti?
Ninavyofahamu msitu wa Mabwepande uko wilaya ya Kinondoni karibu na Mpiji, Bunju, Mbopo wakati Pande ni kijiji kilichoko Zinga wilaya ya Bagamoyo ukiwa unaelekea chuo cha uvuvi Mbegani.
Hawa makada wa CDM walitupwa eneo lipi kati haya?
Walipotesewa ni kwenye nyumba za NSSF zilizojengwa kwenye mkondo wa bahari zikatelekezwa pale Ununio mkabala na mikoko au barabarani kwenye shamba la chumvi?
Nchi imefikia pabaya sana na askari wanaotumika kutesa Watanzania wenzao kisa wana itikadi tofauti!?
Kimsingi hakuna raia anayekubaliana, viongozi wa kidini na kiroho hawakubaliani na mwenendo wa utawala hata baadhi ya askari hawakubaliani ila wanatii kuepuka kuuwawa na wenyewe.
Hii nchi ni ya Watanzania wote haijalishi ni nani atakuja kuiongoza, Marekani inadumu kuwa na nguvu na kuonesha namna ya uvumilivu. Trump D, amenyanyaswa sana na utawala wa Bidden lakini alipoingia madarakani hajalipiza kisasi chochote zaidi ya kufanya mabadiliko ya kimfumo. Tanzania inachochea raia wake yenyewe kuwa na chuki dhidi ya chama kinachotawala na huenda visasi vikamea kuelekea uchaguzi ujao. Upungufu urekebishwe na waliotenda matendo haya yasiyofaa wawajibishwe ipasavyo kuliko kuwa na kiburi cha madaraka ambayo sio ya milele.