Ugumu wangu
JF-Expert Member
- May 6, 2021
- 1,685
- 3,552
- Thread starter
- #21
Inaendelea......
Basi siku hiyo ndio ikaisha hivyo nami nipo kimya tu sikutaka kumshirikisha mtu yeyote hata rafiki yangu ninaelala nae geto moja pia sikumwambia, Basi baada Kama week moja hivi yule mzee alikuja na Gari akashuka hapo alikuwa kavaa miwani nyeusi fulani akaniita njoo kijana wangu nikaenda akaniambia vipi Kuna mtu unamdai nikamjibu hapana, je Kuna mtu anakudai nikasema ndio maana hela ya kazi siku mbili sijakabidhi na ninazo zote Basi akaniambia utamkabidhi Nani Sasa nikamwambia Kuna mtu hapa naweza mkabidhi atampa ni mwaminifu tu.
Baada ya kumjibu maswali hayo nikamuuliza kwani mie naenda wapi kwa mda huu baba angu akaniambia unaenda Tabora shuleni, ukweli hapa sikuamini ninachokisikia masikioni mwangu ghafla machozi yananitoka nikamuuliza ni kweli inawezekana ? Je jina langu bado lipo kweli huko akaniambia wewe nenda shuleni Kama bado unapenda kusoma nikamwambia napenda sana kusoma.
Baada ya hapo nimekabidhi hela nikaandika kibarua kidogo kumwaga rafiki yangu tulikuwa wote getoni maana hakuwa na simu na kipindi hicho wenye simu ni wa kuhesabu maana hata huyo mzee sijui Kama alikuwa nayo maana sikumuona akiwa nayo hata kidogo,
tulianza safari Hadi karume pale nikaambiwa chagua viatu pair 4 hivi nikachagua akalipa mzee tukaondoka Hadi kwenye mashuka akanunua nakuweka kwenye bag tukaanza safari Hadi ubungo nikakatiwa ticket tukaondoka tukaenda nikapelekwa kwa Dada mmoja hivi nikatambulishwa nikaambiwa huyu dada atakupeleka stand asubuhi, mzee akaniuliza wewe una sh ngapi hapo mfukoni nikamwambia Nina laki na nusu akaniambia hiyo inakutosha kabisaa njiani mahitaji mengine utayapata shuleni.
Basi kesho yake safari ikaanza Kama siku tatu hivi ndio nikaingia Tabora kumbuka kipindi hicho kwanzia dodoma ni vumbi mwanzo mwisho, nilifika stand pale Tabora maana nilikuwa nimeambiwa ukishuka chukua daladala ya baiskeli mpka hapo shuleni utapokelewa Basi nami niliuliza watu hapo Tabora boys ni wapi nikachukuliwa na daladala Hadi hapo shuleni nikapelekwa ofsi ya mkuu wa shule nikapokelewa na second master akaniuliza wewe ndio Fulani nikasema ndio, basi akaniambia wewe umekuja kusoma au umekuja kuiona shule tu alafu urudi nikamwambia nimekuja kusoma.
Hapo nakumbuka ilikuwa umebaki week moja tu mitahani ya mwezi wa sita ianze Basi nikapelekwa kwa mkuu wa shule nikaambiwa utakaa hapa mpaka shule ikija kufunguliwa ndio utaenda bwenini nikaona hapa sawa na kwenye Chumba tulikuwa wawili na jamaa mmoja alikuwa form six basi tukawa tunapiga story ananitia moyo sana nikaanza kukopy notes na kusoma karibia usiku kucha week likakata , mkuu wa shule aliporudi alinikuta kidogo nimechangamka akaniambia vipi unaweza kufanya mitihani na wenzio nikasema ndio naweza kujaribu akasema sawa Basi jiandae jumatatu mitahani unaanza.
Nami bila kinyongo nilipiga msuli haswa wa kusoma huku yule jamaa wa form six akinitia moyo na kunifundisha sana tena kwa bidii kweli jtatu ikafika nami huyo kwenye Chumba Cha paper nikazama hapo ndipo nilianza rasmi kumwogopa Mungu kwani kila siku nilikuwa naingia kwenye Chumba Cha mtihani nimefunga na haya ndio matokeo yangu ya mtihani wa mwezi wa sita form one nikiwa nimefika shuleni week mbili kabla ya mitahani kuanza,
MATHEMATICS: A 100
PHYSICS. A 95
CHEMISTRY A 98
BIOLOGY. A 100
GEOGRAPHY A 100
HISTORY. A 100
CIVICS. A 98
ENGLISH F 15
KISWAHILI A 100
Baada ya matokeo hayo mkuu wa shule alinambia unastahili kutunzwa kwa gharama yeyote nikasema sawa akaninunulia saa Kama zawadi na maisha yakasonga mbele miaka iliyofuata ikawa napita kwenye kipindi kigumu sana hasa kwenye likizo mda mwingi nilikuwa naweza shinda bila kula na mda mwingine tukifunga shule nami naenda kutafuta vibarua kwa mfano niliendaga huko wilaya ya Uyui kata ya Loya kuvua samaki na mwaka mwingine pia nikaenda huko kuvuna mpunga sikurudi nyumbani maana nilikuwa naogopa kurudi home likizo najua nikirudi naweza nusirudi shuleni tena.
Itaendeleaa.....