Kutoka Singida hadi Dar es Salaam kwa matumaini ya kupata msaada wa elimu

Kutoka Singida hadi Dar es Salaam kwa matumaini ya kupata msaada wa elimu

Inaendelea......

Baada kuchukua elfu hamsini yangu na kutunziwa laki moja nikaondoka hapo shuleni nikapita kanisani FPCT Ng'ambo ilikuwa ni ibaada ya siku ya jumatano, ibaada ilipoisha nikaenda getoni kwa furaha kabisa siku hiyo nikabadili na msosi vizuri na maumivu yangu ya kipigo.

Siku zilienda hatimae mtihani wa mock form 4 ukafika niliufanya kwa kujiamini sana lakini mwisho wa Siku matokeo yanatoka nina 4.28 ukweli moyo wangu uliumia mno siku hiyo baada ya matokeo nilienda kwenye miembe ya nyuma karibu na kambi ya Jeshi hapo nikalia sana sana ile wakati nimekaa wakaja wajeda wawili walikuwa wanazunguka tu hapo wakaniuliza dogo vipi nikasema poa,shida Nini nikawaambia matokeo yangu mabovu na sijui nitakuwa mgeni wa Nani na je nitawashawishi vipi watu wanipe msaada kwa matokeo haya?.

wale maafande wanilinitia moyo sana na kusema mbona mbona hata mabosi wetu hapa wana nyota zao hapa lakini hata elimu yao ni ndogo tu dogo acha kuwaza mtegemee Mungu, basi nikatulia tukaanza kupiga story hapo mdogo mdogo nawadodosa vipi nami nikitaka kuingia jeshini nawezaje kupata nafasi tukaongea mengi sana baadae takaagana mie nikarudi zangu bwenini kwangu Kimweri.

siku zikayoyoma kidogo kwa kipindi hiki nilikuwa na mahitaji yote vizuri mawazo yalipungua sana nikamweleza kwenye kusoma, Mungu ni mwema necta hii hapa ikafika nikafanya nilipomaliza nikawaza kwenda home maana nimepamic na hasa nimekumbuka mama yangu lakini kila nikiwaza kwenda roho inakataa na naona kabisa nikienda tu Nyumbani Basi elimu kwangu ndio mwisho.
 
Ukiendelea uni tag! I'm interested! Naamini hii story yako ni ya ukweli! Hivi mkuu wa shule Tabora Schiol kipindi hicho alikuwa nani vile?
 
Basi katika kuwaza sana nilion njia pekee ni kwenda dar wakati bado nasubiria matokeo Basi nikatafute kibarua Cha kufanya, Basi nikaenda kwa mkuu nikaomba kwanza anipe hata namna ya kuonana na yule mzee alienitoa kwenye kibanda kushona viatu lakini na mkuu hakuweza kunipa na akasema yeye aliambiwa tu anipokee na mpaka hapa yule msaada wake ndio uliisha hapa, nililia nikamwambia naomba hata mawasiliano tu Mimi nimshukuru tu lakini hakuweza kunipa na Hadi leo sijui huyo mzee yupo wapi, basi nilimuaga mkuu akanipa na tuakiba za pesa zangu zote na zingine ambazo alitumiwa Ila hakuniambia Ila siku hiyo kanikabidhi zote nikaenda na kwa yule mama nikamwambia mama Mimi naondoka nae akanipa kafungu fulani kazuri na kaniandikia barua kanipeleka kwa RTO nikatandikiwa barua ya kupewa msaada wa kusafiria bure hii Hadi leo barua hii ninayo Kama kumbukumbu yangu.

Nilienda kituo Cha tren nikapanda baada ya kuonyesha kibarua changu huyoo mpaka dar nikafika sehemu nilipokuwa nashona viatu nikamkuta jamaa yangu yupo nikafurahi sana kumwona tukasalimiana baadae nikaenda kulala gongo la mboto guest kesho yake mapema nikashuka Pugu mnadani kwa mbele panaitwa mwambisi hapa ni kile kipindi bado watu hawajahamishwa huko kulikuwa na mzee mmoja wa kinyaturu huko Mwambisi tulifahamiana wakati nashona viatu akanipa maelekezo akaniambia ukiona maisha yanakuwa magumu naomba uje tubanane hapahapa.

Nilifika yule mzee akanipokea vizuri kabisa kwa furaha nikajitambulisha akawa amenifahamu vizuri na maisha yakaanza ya kukata mkaa na kwenda kuuza Pugu kajiungeni huko na Goms mwisho wa lami.

Katika kukata mkaa kwangu nilikutana na watu wengi sana na tukafahamiana nikawa mwenyeji mno na nikapata fedha nyingi tu, matokeo ya form 4 yalitoka siku yanatangazwa nipo zangu Buguruni narudi zangu Goms nasikia kwenye Gari matokeo matokeo mie nikawa nahamu ya kutaka kujua Nini kinaendelea nikapita kwa binamu yangu kwa Mara ya kwanza tangu niondoke hapo kwa kutoroka Basi nikamkuta binamu yupo karudi job nikamwambia binamu unajua nilikuwa shuleni, Wala hakuchukulia uzito sana duuh mood yote ikaisha kabisa nikaondoka kwenda kwa mzee mmoja alikuwa jirani yake na ni mtu wa home nikamwambia yote lakini ombi langu naomba unifanyie mpango nijue matokeo yangu ya kidato Cha nne mzee akasema usijali mwanangu kesho nikienda job nitakuambia.

Siku ikafika kesho yaani Nina Moto vibaya mzee kaja kwanza kacheka kaniambia we kweli mwanaume, nikamwambia Basi niambie tu, mzee kauvuta mkeka akaniambia Tabora boys mna one ya 7 zipo kadhaa na wewe umo nikamwambia unanitania akasema ni kweli Basi nikafurahi Hadi machozi siku hiyo ilikuwa ni ijumaa nikasepa Hadi church kukesha kabisa kwa maombi.

Itaendeleaa.........
 
Ukiendelea uni tag! I'm interested! Naamini hii story yako ni ya ukweli! Hivi mkuu wa shule Tabora Schiol kipindi hicho alikuwa nani vile?
Ili uhisi eti ?? Endelea kuhisi mkuu🤸🤸🤸🤸😂😂
 
Duuh aisee kuna watu wamesota bna daah pole na hongera kwa kutokata tamaa mkuu. Nadhani ukaribu wako na M/Mungu ulijengwa zaidi na kuepuka anasa, vijana wengi tunafeli kwenye mbunye tuuuu. Daah aisee.
 
Bas nitarejeaa na mm Niko apa singida karakana karibu ingawa nimetoka Arusha ila pia nilisoma na wanyaturu kadha hakika Hawa watu wakipatia shule wanakuwa wakali mno na wanaelewa vzr sana ingawa vijana waadhiriwa na ulevi na hatimae kashindwa kumalizia shule ama vyioo vikuu ..respect kwako kwa kuweza kufika uliko pia mungu amekuzimamia Sana sifa na utukufu Ni zake
 
Hongera kwa uhodari uliotukuka, yaani kila kipande cha historia yako kinaamsha hisia kali sana hakika ulipigana kiume nimetokwa na machozi japo najaribu kujikaza kwa sababu umenikumbusha mbali sana.
Hapa home nina wadogo zangu huwa nawaambia kuna watu wamepitia au wanapitia magumu sana kwa hiyo kama mkishindwa kutumia fursa basi mtanikumbuka mkiwa wakubwa na majukumu yenu.

Binafsi nimesota.
 
Duuh aisee kuna watu wamesota bna daah pole na hongera kwa kutokata tamaa mkuu. Nadhani ukaribu wako na M/Mungu ulijengwa zaidi na kuepuka anasa, vijana wengi tunafeli kwenye mbunye tuuuu. Daah aisee.
Ameen mkuu
 
Bas nitarejeaa na mm Niko apa singida karakana karibu ingawa nimetoka Arusha ila pia nilisoma na wanyaturu kadha hakika Hawa watu wakipatia shule wanakuwa wakali mno na wanaelewa vzr sana ingawa vijana waadhiriwa na ulevi na hatimae kashindwa kumalizia shule ama vyioo vikuu ..respect kwako kwa kuweza kufika uliko pia mungu amekuzimamia Sana sifa na utukufu Ni zake
Ameen mkuu
 
Back
Top Bottom