Julias Vimvinyira
Senior Member
- Jun 2, 2025
- 155
- 205
Katika shamrashamra za maadhimisho ya Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika jijini Stockholm, Sweden, mgeni rasmi, Mhe. Nyamko Sabuni, Waziri wa zamani wa Usawa na Jinsia nchini Sweden, ametoa hotuba kwa lugha ya Kiswahili fasaha na yenye mvuto.
Mhe. Nyamko, mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na aliyekulia Tanzania, amesema Kiswahili ni lugha inayovuka mipaka, akilitaja kuwa chombo muhimu cha biashara, utambulisho na mshikamano.
Amesisitiza kuwa hata anapokuwa nchini Kenya kwa shughuli za kibiashara, huendelea kutumia Kiswahili kama lugha ya mawasiliano.
Hotuba yake imeibua hisia za fahari na mshikamano miongoni mwa Watanzania na wageni zaidi ya 500 waliokusanyika kusherehekea urithi huu wa lugha ya Kiswahili kwa shangwe, nderemo na hali ya kuhamasika.