YEYOTE ALIYEWEZESHA HII ' IDEA ' NAMPA HESHIMA YAKE
Magoiga SN
Rafiki yangu mmoja ambaye ni kijana wa upinzani amenifuata inbox akiwa na lengo la kuniambia kuwa wananchi wote waliohudhuria tamasha la CCM uwanja wa Taifa jana walienda kwa sababu ya wasanii na siyo CCM, kwahiyo nisishangilie uwanja kujaa
Nilichomjibu:
Ni kweli, wapo walikwenda pale kwasababu ya wasanii na wapo waliokwenda pale kwasababu ni tamasha linaloihusu CCM ndiyo maana uliona wengi wamevaa nguo za chama, lakini kitu cha muhimu cha kukumbuka ni kwamba tamasha la jana lilihusu uzinduzi wa nyimbo 500 za kampeni za CCM zilizoimbwa na wasanii zaidi ya 200 nchini.
Nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa ni nyimbo zinazoihusu CCM , Rais Magufuli na utekelezaji wa ahadi na ilani ya uchaguzi tu, hakukuwa na Bedroom ya harmonize wala money money ya 20 Percent, yaani kwa lugha rahisi sana ni kwamba wananchi kwa hiyari yao wenyewe walikaa uwanjani kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa saba usiku wakisikiliza na kucheza nyimbo zinazoisifia CCM, kumpongeza Rais Magufuli na serikali anayoiongoza, what a milestone
Wasanii wote walipanda jukwaani wakiwa wamevalia mavazi au sehemu ya vazi yenye nembo ya CCM nk, wasanii waliwaimbisha watazamaji, kuwachezesha na kuwashirikisha ktk uimbaji wa nyimbo za CCM. Yaani kuanzia saa moja asubuhi mpaka usiku wa maneno neno CCM, neno Magufuli, neno utekelezaji wa miradi ya maendeleo, neno amani na utulivu yalikuwa yakijirudia kila baada ya sekunde kadhaa. Ukumbi mzima ulitapakaa alama za CCM, rangi ya vazi la CCM, screen kubwa jukwaani haikukauka kauli mbiu za CCM, yaani ni sawa na kusema uwanja mzima influenced kwa kijani na njano kuanzia mazingira mpaka maudhui ya nyimbo zote
Kwa lugha nyingine ni kwamba, wananchi walikuwa wakicheza nyimbo ambazo ujumbe mkubwa ulihusu ubora na uimara wa CCMkaka chama cha siasa, Rais Magufuli kaka kiongozi makini na mafanikio makubwa yaliyopatikana ktk miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa
Watu wakiwa wanawasikiliza wasanii ambao wanawakubali na kuwapenda kuanzia saa moja asubuhi mpaka usiku wa manane wakiwa wanatumbuiza ujumbe wa aina moja kuhusu CCM, Rais Magufuli na miradi ya maendeleo iliyoelekezwa huku wakicheza na kufurahia ina faida kubwa sana ktk ushawishi na afya ya akili.
Mimi siyo mwanasaikolojia lakini wataalamu wa masuala ya 'marketing and branding' wanajua vyema hii mbinu, wataalamu wa masuala ya saikolojia wanajua vyema hiki kitu, kwahiyo ukweli ni kwamba hili tamasha la CCM kuzindua nyimbo za kampeni zilizoimbwa na asilimia 99 ya wasanii wote nchini siyo kitu kidogo
Akili ya kawaida ya kibinadamu inapenda kuunga mkono upande ambao unaonekana kuwa smart, upande ambao hata wale unaowapenda na kuwaamini wanauunga mkono, upande ambao una uhakika na kile ambacho unaakifanya.
Ndiyo maana hata ambao hawakuweza kufika uwanjani walikaa kwenye TV zao kufuatilia nini kinafanyika uwanja wa uhuru, ninachoweza kusema ni kwamba tamasha hili limefuatiliwa na watu wengi sana bila kujali itikadi zao, na nyimbo zilizokuwa zikitumbuizwa jukwaani ni nyimbo za CCM, na bado waliendelea kufurahia.
Aliyewaza na kusimamia utekelezaji wa hiki kitu (hii idea) nampa heshima yake, kama ni wewe Ndugu Hamphrey Polepole BIG UP sana.
Sasa chama kitazame namna ya kuifanya hii idea iwe ya kila mwaka, angalau mara moja kwa mwaka wasanii wawe wanafanya kitu kama hiki, kama mwaka huu kinefanyika Dar es Salaam, mwaka kesho inaweza kufanyika Mtwara, au Mwanza au Arusha nk nk, burudani ni tiba, na burudani ya nyimbo za CCM ni tiba ya uzalendo.
Magoiga SN