Katika hali isiyo ya kawaida jana CCM wamezindua rasmi kampeni uchaguzi 2020 zilizofanyika katika uwanja wa UHURU huku zikihuduhiriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Serikali pia kama Msemaji mkuu wa Serikali. Kampeni hizo ambazo zilipewa jina la TAMASHA LA CCM zilichagizwa na wasanii mbali mbali wa muziki huku kila mmojawapo akihamasisha na kumkampenia Rais magufuli katika uchaguzi wa mwaka huu ambaye nae baadae aliwahutubia wahudhuriaji kwa njia ya Simu. Kwa Teknolojia ya sasa huitaji mgombea kuwa sehemu ya tukio unaweza kutumia mitandao pia kuhutubia kama alivyofanya jana.
Kwa hili lilofanykja jana wadau wengi wa siasa wanasubiri tamko au adhabu ya NEC dhidi ya CCM kwa tukio lilitokea jana. Kwa muijbu wa sheria za uchaguzi kuanza kampeni kabla ya mda wake adhabu yake ni mgombea wa chama husika kuengeliwa katika uchaguzi.
Nawakilisha.