Kutoka vibanda hadi viwanda, maonyesho ya CIIE yamekuwa "chachu" ya ushirikiano wa China na Afrika

Kutoka vibanda hadi viwanda, maonyesho ya CIIE yamekuwa "chachu" ya ushirikiano wa China na Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
VCG111463250973.jpg

Wakati dunia inapokabiliwa na changamoto za kuongezeka kwa hatua za upande mmoja na kujilinda kibiashara, Maonyesho ya 8 ya Uagizaji Bidhaa ya Kimataifa ya China CIIE yamefunguliwa tarehe 5 kama ilivyopangwa huko Shanghai. Likiwa jukwaa muhimu la kukuza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika, CIIE ya mwaka huu ilipanua zaidi maeneo ya kutangaza bidhaa za Afrika, huku idadi ya kampuni za Afrika zinazoshiriki ikiongezeka kwa 80% kuliko maonyesho ya mwaka jana. Hii haionyeshi tu kasi kubwa ya ushirikiano wa China na Afrika bali pia inaleta uhakika mkubwa kutoka Nchi za Kusini katika uchumi wa dunia usio na uhakika.

Kwa muda mrefu, Afrika imekuwa ikizingatiwa kwa kiasi kikubwa kama "mtoaji wa malighafi" katika mnyororo wa thamani wa kimataifa. Hata hivyo, CIIE, ikiwa na sifa ya "uagizaji" inavunja dhana hii, ikitoa jukwaa kwa nchi za Afrika kuonyesha bidhaa zao na kubadilisha viwanda vyao. Haiangalii tu rasilimali za jadi kama vile mafuta na madini bali pia inakuza bidhaa za kilimo zenye thamani kubwa na zile zenye umaaluma wa Afrika kama vile maparachichi ya Kenya, achari ya pilipili ya Rwanda, mafuta ya ufuta ya Tanzania, na mvinyo wa Afrika Kusini katika soko la China.

Kwa miaka saba, Maonyesho ya CIIE yamesaidia kampuni za Afrika “kuwasiliana” moja kwa moja na kampuni na wateja wa China, yakileta mabadiliko kutoka "kuuza maliasili" hadi "kutengeneza chapa." Bidhaa nyingi zaidi za Afrika zinapata kutambuliwa katika soko la China.

Umuhimu wa CIIE upo kwenye zaidi ya maonyesho yenyewe; hufanya kazi kama chachu ya ushirikiano wa kina wa viwanda kati ya China na Afrika. Tukichukulia mfano achari ya pilipili ya Rwanda: baada ya kupata umaarufu mkubwa katika maonesho ya CIIE, ongezeko la oda lililopatikana lilichochea upanuzi wa kilimo cha pilipili nchini Rwanda na uboreshaji wa vifaa vya uzalishaji, na kuvutia kampuni za China kushiriki kwenye mtaji, teknolojia, na uzoefu wa usimamizi. Hii haisaidii tu Afrika kujenga mnyororo kamili wa viwanda, kuboresha kiwango chake cha viwanda, na kuunda ajira, bali pia huleta usambazaji thabiti na wa hali ya juu katika soko la China. Kwa hivyo, CIIE imeunda mzunguko mzuri wa "uwekezaji unaoendesha biashara, na uwekezaji unaokuza biashara," ikiimarisha msingi wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika.

Mafanikio ya CIIE yaliyopatikana kwa awamu nane mfululizo hayawezi kutenganishwa na uungaji mkono wa sera za China za kupanua ufunguaji mlango. Mnamo Juni mwaka huu, China ilitekeleza ushuru sifuri kwa 100% ya bidhaa kutoka nchi 53 za Afrika ambazo zina uhusiano wa kibalozi na China. Maonyesho ya CIIE sasa yanakuwa jukwaa la kutegkeleza sera hiyo moja kwa moja. Kupitia ukaguzi ulioboreshwa kwenye karantini, taratibu rahisi za uondoaji wa forodha, na uainishaji sahihi wa ununuzi na uuzaji, faida za sera zimebadilishwa kwa ufanisi kuwa matunda ya soko.

Data inajieleza yenyewe: Katika CIIE ya kwanza mnamo 2018, uagizaji wa China kutoka Afrika ulikuwa dola bilioni 99.2 za Marekani; Kufikia mwaka 2024, takwimu hizi zilikuwa zimeongezeka hadi dola bilioni 116.8 za Marekani, ongezeko la 17%. Ripoti ya IMF inaonyesha kwamba ushirikiano wa China na Afrika umekuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa Afrika, huku biashara kati ya China na Afrika ikichangia asilimia 1-2 katika ukuaji wa uchumi wa Afrika kila mwaka, na uwekezaji wa China ukiongeza kiwango cha usindikaji wa ndani wa Afrika kutoka 15% hadi 45%.

Kama msemo unavyosema “Ukiwa karibu na muwaridi basi nawe utanukia”. Kwa maana hiyo unapofuatana na China bila shaka utakuwa unafuatana na fursa. Wakati ambapo baadhi ya nchi zinajenga kuta na kutumia vibaya ushuru, China inafuata ushirikiano wa wazi na kunufaishana, ikionyesha maono ya nchi kubwa inayowajibika. Kadri “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Mapendekezo Manne Makubwa yaliyotolewa na China yanavyozidi kuendana na mikakati ya nchi za Afrika, Maonyesho ya CIIE yatatumika kama kichocheo muhimu zaidi, kusaidia kuboresha muundo wa biashara kati ya China na Afrika, na kukuza bidhaa za Afrika kupata soko kubwa zaidi duniani.
 

Attachments

  • VCG111601610124.jpg
    VCG111601610124.jpg
    1.1 MB · Views: 38
  • VCG111529110751.jpg
    VCG111529110751.jpg
    191.9 KB · Views: 40
Back
Top Bottom