Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Namsikiliza hapa akitangaza nia:

Anasema:

Jimbo la mtama lipo salama, na milele daima litakuwa ccm. Anasema hivi kwa msisitizo mkubwa kabisa. Kama kiongozi anaetarajia kuwa kiongozi wa juu hakupaswa kusemea wananchi eti tu kwa kwa sababu ya maslahi ya chama.

Anasema:

Ana uzoefu mkubwa serikalini na kwenye chama. Sawa. Kwa kipindi chote alichokaa madarakani ni wapi alipogusa mioyo ya watanzania walalahoi?

Anasema:

Suala la elimu JK kafanya mazuri sana kwenye eneo hili, asibezwe. Sawa. Ina maana kuporomoka kwa elimu kwa kiwango cha kutisha ndio mazuri aliyofanya JK? Sasa hv kuna hadi div 5 ambayo kimantiki haina maana yoyote isipokuwa siasa tu.

Anasema:

Hatakubali katika utawala wake rais mstaafu aguswe kwa namna yoyote ile. Sawa. Vipi wananchi wakitaka katiba ibadilishwe na kuruhusu rais kuwajibishwa kwa makosa aliotenda madarakani? Membe ana hati miliki ya watanzania?

Anasema:

Haoni mtu mwingine mwenye uwezo zaidi yake. Sawa. Vipi maamuzi ya kamati kuu, halmashauri kuu na mkutano mkuu ukimtengua? Membe anasahau kuwa anapaswa kutoa hotuba ya kutia nia na siyo ya kupambana na UKAWA.

Anasema:

Yeye amesomea masuala ya usalama hivyo anatoa salam kwa wauaji wa albino maana hawana pa kujificha pindi akiingia madarakani kama rais. Sawa, lakini kinachomnyima sasa hivi asikabiliane nao ni kitu gani? Mbona yupo kwenye system ya serikali kama kiongozi mwandamizi wa serikali?

Anasema:

Ana uzoefu mkubwa sana katika masuala ya kimataifa. Sawa. Je, ina maana alisahau kauli zake tata kama waziri wa masuala ya nje kuhusu masuala ya nje. Ooohh nchi haibebwi kwenye toroli, nk nk

Anasema:

Anatambua kazi za wasanii. Anakubali kuwa kazi za wasanii zinaibiwa. Sawa. Yeye ni waziri mwandamizi kwenye serikali iliyopo madarakani, nini kinachomzuia asifanikiwe kuwasaidia hawa wasanii?

Anasema:

Anasema kuhusu utawala bora. Kama mla rushwa na mpokea rushwa wakikamatika na rushwa na kupelekwa mahakamani. Na mahakama ikamwona kwamba hana hatia basi yeye atamwita ofisini na kumpongeza kwa kuruka kiunzi cha mahakama, lakini kwa kuwa yeye ndie aliemteua atamwachisha kazi mara moja na kumwambia aende akalime mihogo. Membe anasahau kuwa mahakama ni chombo cha haki. Anasahau kuwa yeye hata kama akiwa rais hayupo juu ya sheria kwa tafsiri hiyo anayotaka yeye kuitafsiri. Membe hatambui nguvu na uhuru wa mhimili wa mahakama?

Anasema:

Nchi kwa ujumla imekaa ki rushwa sana kiasi kwamba hata wafanyabiashara wanaogopa kupokea simu. Sawa. Sasa membe wewe upo ndani ya serikali hii hii, umechukua hatua gani? Mbona unalalamika kama UKWA?

MBONA MEMBE UNAZUNGUMZA KAMA VILE WEWE SIO SEHEMU YA HII SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI?

cc: Team Membe
 
Last edited by a moderator:
Wala rushwa wana sifa moja kubwa nayo ni uongo. Akipendwa na watu sita yeye atasema anapendwa na watu laki sita. Akichukua rushwa utasikia kapewa na marafiki zake. Aisee!!!! Shughuli ni kubwa ndani ya CCM.
 
nimeshangaa huyu jamaa imekuwaje kadumu uwaziri wa mambo ya nje..ndio maana jumuia ya afrika mashariki iliyumba,mahusiano na malawi yakayumba,mahusiano na rwanda,kenya uganda
 
"Nikiwa Raisi nitabadilisha kipengele cha mtoa rushwa na mpokea rushwa kuwa wote ni wahalifu na badala yake itakuwa Mtoa Rushwa ataachiliwa huru na mpokea rushwa atakwenda jela"

by Membe.

Duuh....huyu mtu nilikuwa namuona bungeni najifariji atakuwa bingwa wa debate kumbe mweupe hivi:what::what:hivi hakujipanga?
 
Sasa Membe kulikuwa na haja gani kuwapiga mkwara wanaume na familia zao eti watakukoma.
 
Kweli nimependa demokrasia ndani ya CCM kila mgombea tumsikilize na tuone uwezo wake.

demokrasia au kiini macho?? Maana wenye chama tayari wana mtu wao
 
chonde chonde vyama vya upinzani wekeni maslahi ya TAIFA mbele,tafadhali sana wekeni mgombea mmoja wa URAISI,Membe kishaahidi kuwalinda maraisi waliopita.Vyama vya upinzani sikilizeni vilio vya watanzania kama kweli mna nia njema na maslahi ya TAIFA
 
Hawa sijui nani kawadanganya watoe hizi hotuba..bora kuchukua fomu kimya kimya ..huyu kaharibu kabisaaa
 
Hahaha Membe atakuwa anajua hana chake kwenye Urais ndio maana katoa speech ya kipuuzi hivi.. Si bure anamjua Rais huyu
 
Back
Top Bottom