Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Kiukweli Mwigulu ni jembe ukimlinganisha na Membe.Aliongea kwa muda mrefu tena akiwa na mipango mizuri hadi huchoki kumsikiliza tofauti na leo hotuba fupi halafu hakuna kitu.
KARIBU TUELEKEE 'CAANAN' NA LAMECK M. NCHEMBA! teh teh kwenye asali na maziwa.
 
Kama mtu katika dakika kama hii muhimu kabisa ktk maamuzi ya maisha yako na matumaini ya Watanzania unatoa speech nyepesi kama ile mtu huyu anafaa kuwa hata diwani?

Hata familia yake sidhani kama anaiongoza vizuri
 

Sasa Mkuu Ritz kwa nini awaongelee hao jamaa hata kabla hajapitishwa na chama chake?

Nilitegemea kwa kuwa tupo katika mapambano ndani ya chama chake angejikita sana huko, mfano jinsi gani atarudisha imani ya chama chake ambacho kwa matokeo ya serikali za mitaa yanaonesha hawakufanya vizuri kama chaguzi za nyuma.

Angeongea ni jinsi gani atawaunganisha makanda wa juu wa chama chake iwapo atapitishwa na chama chake.

Angeongelea jinsi ambavyo mathalani miladi ya chama itasimamiwa ili kukisaidia chama kutotegemea kwa sehemu kubwa ruzuku toka serikalini!
Angeongelea pia mathalani mianya katika chama chake na ataziziba vipi

Then mwishoni angeongelea maswala ya SERA kwa maana nini serikali yake itasimamia pamoja na uwepo wa ilani ya chama.

Kwa mlengi huo, angeonekana zaidi kama mtia nia wa sisiemu na sio kama tayari yeye ni mgombe mteule katika nafasi ya urais.

Cc Team Membe
 
Last edited by a moderator:
Iv membe amesahau yy n wazir wa mambo ya nje?
Anavyojnad atasaidia michezo, alkua wap kuanza nalo bado wazir wa mambo ya nje! Ata kupeleka vijana au kushawishi club kutoka nje kuchukua au kuanzsha taasis hapa nchi imesmshinda leo ajiwa rais ndo ataweza

Awa mawazir wanazid kuprove failure kwa uongoz wa j.k
 
Nakumbuka kwenye uzinduzi wa mkutano wa ACT - Wazalendo kule Mwanza kuna mbunge wa CCM alipata mualiko watu walipiga sana kelele kuwa ACT - Tanzania na CCM lao moja.

Sasa leo kulikoni tena kwenye mkutano wa Membe kutangaza nia ya kugombea urais kumejaa wabunge wa Ukawa.

Cc; Mkandara Mchambuzi Mag3 Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Mara wengine wanaambiwa hawajui kuongea na hao wanaoambiwa wanajua kuongea wanaambiwa hawawezikutekeleza. Basi hata haieleweki mnachokitaka ni nini.
 
Bongo movie wote ni team ya Membe
 
Kwa hiyo pale alikuwa anaomba ridhaa kwa UKAWA, maana nusu ya hotuba yake amezungumzia Ukawa na nusu iliyobaki kaongelea matambiko na jinsi chama kilivyo na vyama rafiki vya nje.
 
Wewe kilaza...ilani ya chama ndio itasema mgombea wa CCM atafanya nini...ila hayo ya sera uwa hayasemwi siku ya kutanga nia...acha ushamba.

Mi na wewe nani Kilaza urais ni cheo cha kitaifa angewaomba wanachama Wa ccm Tanzania Kwa ujumla
 
Shughuli ya leo imepambwa na usanii mtupu.Sasa hao wasanii wanini?
 
Hizo hadithi za ccm hizo!!!! Wenyewe kwa wenyewe hawapatani hahahaaaaa
 
Membe hivi unatangaza nia au upo kwenye mkutano wa kampeni daahh!!

Na mm nimeshangaa sana, imekua kama ameshapitishwa tayari, kwa mtazamo wangu leo ilikua kutangaza nia sio kampeni, maanna amejipa mamlaka mengi mno kama vile chama kimeshampitisha au kama vile amedokezwa kwamba atapitishwa yeye. Bt ndio siasa bana kila mtu na utashi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…