Sasa Mkuu
Ritz kwa nini awaongelee hao jamaa hata kabla hajapitishwa na chama chake?
Nilitegemea kwa kuwa tupo katika mapambano ndani ya chama chake angejikita sana huko, mfano jinsi gani atarudisha imani ya chama chake ambacho kwa matokeo ya serikali za mitaa yanaonesha hawakufanya vizuri kama chaguzi za nyuma.
Angeongea ni jinsi gani atawaunganisha makanda wa juu wa chama chake iwapo atapitishwa na chama chake.
Angeongelea jinsi ambavyo mathalani miladi ya chama itasimamiwa ili kukisaidia chama kutotegemea kwa sehemu kubwa ruzuku toka serikalini!
Angeongelea pia mathalani mianya katika chama chake na ataziziba vipi
Then mwishoni angeongelea maswala ya SERA kwa maana nini serikali yake itasimamia pamoja na uwepo wa ilani ya chama.
Kwa mlengi huo, angeonekana zaidi kama mtia nia wa sisiemu na sio kama tayari yeye ni mgombe mteule katika nafasi ya urais.
Cc
Team Membe