Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

Uchaguzi 2020 Kutoka viwanja vya CCM, Lindi: Membe atangaza nia ya Urais!

naona anachezesha na kuimba nyimbo...hiyo ndiyo kazi inayomfaa
 
Kwa hotuba hii ya membe namuona Makongoro ndani ya ccm hana mpinzini. Membe kachemsha sana! Kaharibu sana
 
Membe anasema alienda kuomba kwenye kaburi la nyerere ili amruhusu awe rais na anasema ameshapewa majibu kuwa anafaa... huu ni uhuni sana sana. huyu mwalimu mwaka huu atatumika sana kisiasa na watu naona hawana jambo jipya la kuongea isipokuwa kusingizia nyerere. membe anasema pia kuwa kuna wajumbe wa halmshauri kuu wamenunuliwa. hii ni hoja ambayo wajumbe wa halmashaur kuu nadhan itawakwaza sana. hawa wazee wangeachwa wapumzike tu kwa kweli maana naona wanatumika vibaya. hasa nyerere kila mtu atakuja kusema ameruhusiwa na nyerere wakati tunajua nyerere ni marehemu.

Anamtumia Nyerere kama hirizi!
 
'Naomba niishukuru mizimwi ya Kimwera kwa kunilinda mpaka nimemaliza hotuba yangu" By Membe.

Naona membe anatambika tena
 
Membe hana tofauti na Gwajima,vijembe vijembe kwa kwenda mbele,yeye anawaza kuwatandika wapinzani tu ila hawazi atashughulikia vipi matatizo ya Tanzania

Unless ulikua u-pay attention...ila amesema kwa uchache jinsi atavyosaidia kuimarisha uchumi, kuongeza zaidi ulinzi na nk

Pia vilevile uelewe, kwa sasa Ilani ya chama bado haipo tayari, mtangaza nia anaweza kusema ambayo yatawafurahisha Watanzania kumbe hayapo kwenye Ilani...hivyo wengi wanaamua waishie tu kutangaza nia na hilo ndilo lengo kuu la huo mkutano...sio kutangaza sera wala sio kuomba kura kwa Watanzania. Elewa hivyo.
 
Sasa huyu anataka kuwa rais wa wamwera au watanzania?
 
Hapo nimempenda kwenye VETA/UFUNDI ana idea nzuri,kuongeza na kufufua viwanda kutaongeza ajira,pia vijana wataweza hata kujiajiri,ila je atayaweka kwenye VITENDO?

Maisha bora kwa kila mtanzania hukumbuki? Nadhani unayapata haswaa
 
Mtu wao yupi? Mkuu lini Ukawa tutawajadili wagombea wake au yupo mmoja tu Dr.Slaa ukimpinga unafukuzwa kama Panya.

Mbona Lipumba katangaza nia Ukawa??
 
Anaamn bila kuiimbia mizimu, mizimu itakasirika nimeshamgazwa sana.
Huyu labda awe mwenyekiti wa ta.wi ccm.
 
Pamoja na kwamba membe ni mwanadiplomasia aliyebobea,Bado uwezo wa kujenga hoja,kutoa hotuba yenye mtiririko wenye ladha ni SIFURI KABISA.Kwa jinsi membe anavyotagaza nia yake,Anavyorukaruka katika hoja zake,Huenda akajikuta anakuwa na maadui wengi kutoka maeneo mbalimbali.Hotuba yake imejaa sifa binafsi kuliko uwezo wake.
Kama angekuwa na washauri wazuri,Membe angejitahidi sana kuonyesha ni kwa jinsi anao anaouwezo wa kutuongoza katika nafasi ya juu kabisa ya nchi yetu
 
hana sera yyte aliyoongea.......speech mbovu ambayo haichambui dira ya yale atakayofanya.....
 
Hakika UKAWA wanayo kazi yani wanapigwa kutoka kila mkoa leo watapigwa kutoka Lindi na baadae watapigwa kutoka Dar....! Bavicha hawana jinsi inabidi wacheze ngoma ya CCM maana sasa wameamini Rais wa nchi hii lazima atoke CCM!

Chadema wanahusianaje na watangaza nia wa ccm.
 
Mmh,kwa akili hizi,Tanzania tunayo safari ndefu sana.
 
CCM ina demokrasia isiyosemeka, ndio maana hata watu kama MEMBE wanapata fursa ya kuutamani Urais na kusema wazi dhamira zao. Ila katika hali halisi, MEMBE HAFAI KUWA RAIS WA TANZANIA. Ukweli usemwe!!!!!!!

Mkuu nilimuamini sana huyu kumbe hovyo kabisa...kama mko karibu na January mshaurini ajipange asitake kujibu wenzake
 
Back
Top Bottom