Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Membe anasema alienda kuomba kwenye kaburi la nyerere ili amruhusu awe rais na anasema ameshapewa majibu kuwa anafaa... huu ni uhuni sana sana. huyu mwalimu mwaka huu atatumika sana kisiasa na watu naona hawana jambo jipya la kuongea isipokuwa kusingizia nyerere. membe anasema pia kuwa kuna wajumbe wa halmshauri kuu wamenunuliwa. hii ni hoja ambayo wajumbe wa halmashaur kuu nadhan itawakwaza sana. hawa wazee wangeachwa wapumzike tu kwa kweli maana naona wanatumika vibaya. hasa nyerere kila mtu atakuja kusema ameruhusiwa na nyerere wakati tunajua nyerere ni marehemu.
Teh Teh...UKAWA nje ya Lipumba na Slaa kuna mwingine?
Membe hana tofauti na Gwajima,vijembe vijembe kwa kwenda mbele,yeye anawaza kuwatandika wapinzani tu ila hawazi atashughulikia vipi matatizo ya Tanzania
Hapo nimempenda kwenye VETA/UFUNDI ana idea nzuri,kuongeza na kufufua viwanda kutaongeza ajira,pia vijana wataweza hata kujiajiri,ila je atayaweka kwenye VITENDO?
Mtu wao yupi? Mkuu lini Ukawa tutawajadili wagombea wake au yupo mmoja tu Dr.Slaa ukimpinga unafukuzwa kama Panya.
CCM tuleteeni Membe,UKAWA tumalize Mechi mapema
Membe anaomba ubunge au uraisi?
Hakika UKAWA wanayo kazi yani wanapigwa kutoka kila mkoa leo watapigwa kutoka Lindi na baadae watapigwa kutoka Dar....! Bavicha hawana jinsi inabidi wacheze ngoma ya CCM maana sasa wameamini Rais wa nchi hii lazima atoke CCM!
CCM ina demokrasia isiyosemeka, ndio maana hata watu kama MEMBE wanapata fursa ya kuutamani Urais na kusema wazi dhamira zao. Ila katika hali halisi, MEMBE HAFAI KUWA RAIS WA TANZANIA. Ukweli usemwe!!!!!!!