Kutokana na mwenendo mbaya wa Simba SC ufuatao ni ushauri wa bure kwao

Kutokana na mwenendo mbaya wa Simba SC ufuatao ni ushauri wa bure kwao

Hizo BAN anazopigwa mara kwa mara zinasaidia Kukuondolea Umasikini mkubwa na Uhaba wa Akili ulionao?
Tuanze kukuuliza wewe kwanza kwanini unongoza kupigwa ban je wewe ndiye unayeongoza kwa kuandika pumba humu ama kupigwa ban kwako mara kwa mara inakufaidisha na kipi kiasi kwamba huwezi kubadilika kiakili?
 
Simba walikosea kumleta kocha ambae hajawah kufundisha soka afrika ni mgeni wa soka letu lakin pia kocha ni tatizo haiwezekan hadi leo hajapata first eleven..mwisho niwapongeze yanga kwa kutwaa ligi kwa mara ya 28..
Hao wenye uzoefu walianzia kufundisha soka wapi?
 
Makolo wamepigwa na kitu kizito kichwani mpaka akili ziwarudie ligi itakuwa imekwisha
 
1. Mtimueni upesi Kocha Mkuu Franco, Msaidizi wake Matola na Meneja Rweymamu.

2. Mpeni Kazi kwa Kipindi hiki Kocha Ndayiragije kisha asaidiwe na ama Pawasa au Mgosi kisha Meneja awe ni Nico Nyagawa.

3. Wachezaji watafutiwe haraka Mwanasaikolojia na nampendekeza awe ni mwana Simba SC Chris Mauki.

4. CEO wa Simba SC Barbara na Mwenyekiti wa Wanachama Simba SC Mangungu wawe karibu sana ikiwezekana kuliko muda wote na Matawi ya Klabu nchini.

5. Simba SC itafute Mkuregenzi wa Ufundi ambaye atajikita zaidi katika Kuijenga Simba SC kwa kuanzia na Vijana ( Kikosi B ) na aje na Mikakati ya Kuimarisha Simba SC kwa miaka Mitatu au Mitano ijayo.

6. Msemaji mpya wa Simba SC Ahmed Ally asijikite zaidi katika Propaganda za Kushindana na Msemaji Mkongwe wa Yanga SC Haji Manara bali aisome Kwanza Klabu na atangulize zaidi Uweledi (Professionalism) na aachane na Uswahili ambao haumpendezi na unaweza Kumuharibia hata Kiutendaji.

7. Simba SC ikubali (japo inauma) kuwa kwa Msimu huu iliteleza katika Usajili na Kujipanga Kimalengo na Kimkakati kuliko Watani zao Yanga SC na kwamba Mbio za Ubingwa zinafifia hivyo basi ijikite zaidi katika Kombe la FA (ASFC) ili ilibebe na ishiriki Kimataifa mwakani huku ikifanya Scouting ya Umakini kwa Wachezaji wazuri wa Kuichezea Simba SC mwakani tofauti na hawa Wabovu waliopo iliyowasajili kwa bahati nasibu na kwa 10% nyingi.

Yanga SC wamejipanga na Wanastahili.
Nakuunga mkono hasa kwa hoja namba 7.
 
Yaani timu umpe mgosi? Pawasa?... yule kocha hana tatizo jamani tatizo ni wachezaji wenyewe
 
[emoji94].... Djigui Diara aliondoka akiacha Simba ina point 24

Anarudi anakuta Simba ina point 25

Anajiuliza Ligi ilisimama au???!![emoji848][emoji848][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom