Kutokujua Sheria za Soka Chanzo cha Malalamiko ya Goli la Yanga!

Ukielewa kanuni niliyoielezea hapo juu kama inavyotambuliwa na FIFA utaona kuwa hakuna mwamuzi yeyote mwenye beji ya FIFA anayeweza kusema hiyo ni faulu..
unatetea upuuzi uliouleta ukiamini utapata wapuuzi wa kukuunga mkono
 
Hata hivyo wenye maamuzi ya mwisho kua mpira umefata mkono au mkono umefata mpira ni waamuzi wa uanjani,sisi huku nje hatuna filimbi wala kibendera
 
Mzee huyu huyu kila anatuambia Juma Pombe anafuata utawala wa demokrasia na sheria (pamoja na kufuta mikutano ya siasa nk),eti leo anataka tumuamini.wewe ni design ya mtu anayeweza kuita pengo ni mwanya kutokana na mahabati.
yaani mpaka nimejuata kuingiabkwenye Uzi wa hili tahira mbaya zaidi linaingiza siasa...
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya mambo ambayo yanaudhi wakati mwingine ni watu kutolea maoni jambo ambalo hawalijui au hata kuchukua muda kulijua hasa kama liko ndani ya uwezo wao. Katika mechi hii ya leo goli la kwanza la Yanga dhidi ya watani wao wa jadi Simba limezua sokomoko uwanjani nan je ya uwanja. Maoni ya wengi ambao wanalipinga goli hilo ni madai kuwa refa “kawabeba” Yanga kwa sababu goli lile lilifungwa baada ya mchezaji kuunawa mpira yaani, kugusa mkono mpira wakati anapokea pasi.

Ni wazi kuwa wengi ambao wanafikiria mchezaji alifanya kosa lililohitaji faulu (free kick) wanafanya hivyo kwa sababu hawajui sheria za soka zinazohusu kuunawa mpira. Refa alikuwa sahihi kutokutoa faulu pale kwani hakukuvunjwa sheria zozote.

Kuelewa kama mchezaji alifanya kosa ni lazima turejee Kanuni za Mchezo ambazo zinatumika kuongoza mchezo wa Soka duniani. Kanuni hizi zimepitishwa na Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) na kama mtu hatosoma na kuelewa basi basi anaweza kufanya makosa ambayo mtu yeyote anayejua kanuni za mchezo huu hawezi kuyafanya. Bahati nzuri – nafahamu mchezo wa soka vizuri – na ninaweza kutolea maoni ambayo makocha na wachezaji wengine watakubaliana name kuhusiana na kutokuwepo kosa katika goli la kwanza la Yanga.

Kanuni za soka zinazohusu faulu mbalimbali (Kanuni ya 12) katika ukurasa wa 119 inaeleza wazi kuwa “Handling the ball involves a deliberate act of a player making contact with the ball with his hand or arm” yaani “Kuugusa mpira kwa mkono inahusisha kitendo cha mchezaji kwa makusudi kugusana na mpira kwa kiwiko chake au mkono”.

Sasa mojawapo ya mambo ambayo mwamuzi anatakiwa kuangalia kuhusiana na hili na ni jambo la kwanza kabisa – na ninaamini ndilo lililofamya refa kutokutoa faulu – ni kuangalia “mwelekeo wa mkono uliko mpira siyo wa mpira uliko mkono”. Hii ina maana kuwa endapo mpira unapigwa na mkono wa mchezaji hauufuati mpira – kama kuuzia, kubadilisha mwelekeo wake n.k – na mpira ukaenda ukagusa mkono bila kuonesha kusudio la mchezaji kuugusa mpira huo basi ni vigumu kutoa faulu au hata penati.

Ukielewa kanuni hii na ukipata muda kuangalia video ya goli la Yanga na ukimsikiliza mtangazaji unaweza kuamini kosa la mchezaji ni kuugusa mpira kwa mkono. Kosa kama hilo halipo kwenye kanuni za Soka! Hakuna kanuni inayokata mpira kugusa mkono; ipo kanuni inayokataza mchezaji kuugusa mpira kwa mkono wake kwa “makusudi” na neno la msingi sana hapa ni hilo la “kwa makusudi”. Kiingereza limetumia neno “deliberately”. Hii makusudi ina maana ya “nia, kusudio, kudhamiria”. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuona video ile na kudai kuwa ilikuwa ni kosa na refa hakuibeba Yanga bali amesimamia kanuni zinazoongoza mpira. Ni vizuri mashabiki, wachezaji na watu wengine wanaotolea maoni soka watumie muda kujifunza kanuni za mpira ili wasije kujikuta wanasababisha mambo ya aibu kama yaliyotokea leo uwanjani na kwenye mitandao ya kijamii.

Ni muhimu kujua sheria hizi ili kuondoa ulazima wa kufanya mambo ya uharibifu yaliyotokea uwanjani ambayo asili yake ni kutokujua kanuni za mchezo. Mashabiki wanapopata hasira kwa kitu ambacho hawakijui – wenyewe wakidhani wanazijua sheria zote za mchezo – ni aibu na kashfa kwa watu wote wanaopenda kandanda.

Upande wa pili, tumeona pia goli zuri, nono na tamu lilifungwa na Simba kupitia kona. Ni goli liliotumia nafasi ya uzembe wa golikipa kukaa kwenye kona. Bahati nzuri miaka yangu nikicheza soka nilicheza kama golikipa na goli kama hili linamuuma sana golikipa kwani anajua kosa lake ni kukaa mbali na posti ya goli wakati wa kona. Golikipa yeyote mzuri anajua wakati wa kona anatakiwa awe nyuma ya wachezaji wake wote kwani ni rahisi kwake kuupima mpira unaokuja kutoka kwenye kona na kuweza kukimbia mbele kwenye eneo lolote kuukoa. Ni vigumu sana kwa golikipa kukaa mbele ya wachezaji, au katikati na mpira ukajaa juu yake kama ilivyotokea leo; ni vigumu kurudi kinyume nyume kuuwahi mpira unaokuja kwenye posti. Hapa ndio uzuri wa goli hili ulipo.

Nje ya hapo, ni kweli tuna matatizo kwenye soka letu lakini inawezekana siyo tu tatizo la uchezaji lakini pia tatizo la kutokujua kanuni za mpira. Yeyote anayetaka kufundisha soka, kucheza au kushangilia soka ni vizuri ajifunze kanuni za msingi za mpira.

Unaweza kupata kanunizamchezo kwa kubonyeza hapa.
Ebu tutafsirie pia mazingira ya mtu kuwa offside na kutokuwa offside, maana goli la Ajib pia limeleta mzozo mkubwa mtaani.
 
Goli walilofungwa burney na arsenal leo ingekuwa ni bongo hapa uwanja usingekalika aisee....hata km mwamuzi kakosea lakin ile reaction ya nahodha wa simba kwa refa na reaction ya washabiki wao ni mambo ya kilimbuien kabisa katika soka na km issue ya jana ingetokea kwe ligi ya mabingwa hivi au ligi za wenzetu ulaya basi tungeshuhudia adhabu kubwa sana ila hapa kwetu ndo hvyo tena
Unasema alikosea na kwenye goli la Ajibu? vipi napo alukosea kwanini kila mechi akosee kuiangamiza Simba tu kwanini hakukosea kukataa hilo goli lao yanga...
 
Huyu mzee @M. M. Mwanakijiji anaanza kuzeeka vibaya naomba ukatoe sindano jukwaa la siasa maana haya mahaba kwa chura wa jangwani ni mwisho, hili la yanga uzuri halitaki usomi hata mtoto angeweza kutoa yake ya moyoni.
 
Hahahaa sawa mkuu.lakin hamna excuse ya kuharibu uwanja kisa refa kaganya kosa,hayo ni mambo ya watoto wa primary
Haki haiombwi inadaiwa na hakuna fomula hii ya kungoa viti itasababisha wachibue tatizo..acha iwe noma...
 
Tuwe wa kweli tu.
Mwamuzi aliwabeba Yanga, iwe alifanya vile kwa makusudi, au bahati mbaya au udhaifu wa kinadamu nk. Huu ni ukweli wa dhahiri kabisa.
hii siyo Bahati mbaya angalia goli letu alilolukataa angalia beki Tatu Wetu alivyokuwa anafanyiwa faulu halafu anapotezea angalia kadi nyekundu na goli la tambwe...
 
Goli la Koscileny dhidi ya Burnely afadhali ya Tambwe!
katika soka kunamakosa ya kibinadamu lakini siyo ya juzi...juzi refa alifanya makosa makubwa matatu hii inaonyesha alidhamilia na records za refa na upangiwajibwa mechi husika nao unamashaka ikumbukwe alikywa amefungiwa baada ya kuibeba yanga zidi ya Coastal ya Tanga na usisahau kila mechi ya Simba na yanga lazima Simba wapewe red card ya mazingira ya kutatanisha
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya mambo ambayo yanaudhi wakati mwingine ni watu kutolea maoni jambo ambalo hawalijui au hata kuchukua muda kulijua hasa kama liko ndani ya uwezo wao. Katika mechi hii ya leo goli la kwanza la Yanga dhidi ya watani wao wa jadi Simba limezua sokomoko uwanjani nan je ya uwanja. Maoni ya wengi ambao wanalipinga goli hilo ni madai kuwa refa “kawabeba” Yanga kwa sababu goli lile lilifungwa baada ya mchezaji kuunawa mpira yaani, kugusa mkono mpira wakati anapokea pasi.

Ni wazi kuwa wengi ambao wanafikiria mchezaji alifanya kosa lililohitaji faulu (free kick) wanafanya hivyo kwa sababu hawajui sheria za soka zinazohusu kuunawa mpira. Refa alikuwa sahihi kutokutoa faulu pale kwani hakukuvunjwa sheria zozote.

Kuelewa kama mchezaji alifanya kosa ni lazima turejee Kanuni za Mchezo ambazo zinatumika kuongoza mchezo wa Soka duniani. Kanuni hizi zimepitishwa na Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) na kama mtu hatosoma na kuelewa basi basi anaweza kufanya makosa ambayo mtu yeyote anayejua kanuni za mchezo huu hawezi kuyafanya. Bahati nzuri – nafahamu mchezo wa soka vizuri – na ninaweza kutolea maoni ambayo makocha na wachezaji wengine watakubaliana name kuhusiana na kutokuwepo kosa katika goli la kwanza la Yanga.

Kanuni za soka zinazohusu faulu mbalimbali (Kanuni ya 12) katika ukurasa wa 119 inaeleza wazi kuwa “Handling the ball involves a deliberate act of a player making contact with the ball with his hand or arm” yaani “Kuugusa mpira kwa mkono inahusisha kitendo cha mchezaji kwa makusudi kugusana na mpira kwa kiwiko chake au mkono”.

Sasa mojawapo ya mambo ambayo mwamuzi anatakiwa kuangalia kuhusiana na hili na ni jambo la kwanza kabisa – na ninaamini ndilo lililofamya refa kutokutoa faulu – ni kuangalia “mwelekeo wa mkono uliko mpira siyo wa mpira uliko mkono”. Hii ina maana kuwa endapo mpira unapigwa na mkono wa mchezaji hauufuati mpira – kama kuuzia, kubadilisha mwelekeo wake n.k – na mpira ukaenda ukagusa mkono bila kuonesha kusudio la mchezaji kuugusa mpira huo basi ni vigumu kutoa faulu au hata penati.

Ukielewa kanuni hii na ukipata muda kuangalia video ya goli la Yanga na ukimsikiliza mtangazaji unaweza kuamini kosa la mchezaji ni kuugusa mpira kwa mkono. Kosa kama hilo halipo kwenye kanuni za Soka! Hakuna kanuni inayokata mpira kugusa mkono; ipo kanuni inayokataza mchezaji kuugusa mpira kwa mkono wake kwa “makusudi” na neno la msingi sana hapa ni hilo la “kwa makusudi”. Kiingereza limetumia neno “deliberately”. Hii makusudi ina maana ya “nia, kusudio, kudhamiria”. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuona video ile na kudai kuwa ilikuwa ni kosa na refa hakuibeba Yanga bali amesimamia kanuni zinazoongoza mpira. Ni vizuri mashabiki, wachezaji na watu wengine wanaotolea maoni soka watumie muda kujifunza kanuni za mpira ili wasije kujikuta wanasababisha mambo ya aibu kama yaliyotokea leo uwanjani na kwenye mitandao ya kijamii.

Ni muhimu kujua sheria hizi ili kuondoa ulazima wa kufanya mambo ya uharibifu yaliyotokea uwanjani ambayo asili yake ni kutokujua kanuni za mchezo. Mashabiki wanapopata hasira kwa kitu ambacho hawakijui – wenyewe wakidhani wanazijua sheria zote za mchezo – ni aibu na kashfa kwa watu wote wanaopenda kandanda.

Upande wa pili, tumeona pia goli zuri, nono na tamu lilifungwa na Simba kupitia kona. Ni goli liliotumia nafasi ya uzembe wa golikipa kukaa kwenye kona. Bahati nzuri miaka yangu nikicheza soka nilicheza kama golikipa na goli kama hili linamuuma sana golikipa kwani anajua kosa lake ni kukaa mbali na posti ya goli wakati wa kona. Golikipa yeyote mzuri anajua wakati wa kona anatakiwa awe nyuma ya wachezaji wake wote kwani ni rahisi kwake kuupima mpira unaokuja kutoka kwenye kona na kuweza kukimbia mbele kwenye eneo lolote kuukoa. Ni vigumu sana kwa golikipa kukaa mbele ya wachezaji, au katikati na mpira ukajaa juu yake kama ilivyotokea leo; ni vigumu kurudi kinyume nyume kuuwahi mpira unaokuja kwenye posti. Hapa ndio uzuri wa goli hili ulipo.

Nje ya hapo, ni kweli tuna matatizo kwenye soka letu lakini inawezekana siyo tu tatizo la uchezaji lakini pia tatizo la kutokujua kanuni za mpira. Yeyote anayetaka kufundisha soka, kucheza au kushangilia soka ni vizuri ajifunze kanuni za msingi za mpira.

Unaweza kupata kanunizamchezo kwa kubonyeza hapa.
Vipi mbona hujaongelea goli la simba lililokataliwa?
Mzee Mwanakijiji
 
Kweli kabisa Refa hajui Sheria za Soka ndio kalikubali Goli la Basketball ndio maana kakataa Goli halali la Ajibu
 
Tuwe wa kweli tu.
Mwamuzi aliwabeba Yanga, iwe alifanya vile kwa makusudi, au bahati mbaya au udhaifu wa kinadamu nk. Huu ni ukweli wa dhahiri kabisa.
Ukishikwa shikamana
1475471661892.jpg
 
Nashauri Marefa wote wafanyiwe Uhakiki ili kuwaondoa Marefa wasio Na sifa.Imethibitika kuwa kuna idadi kubwa ya marefa wa BASKETBAALL lakini wamesajiliwa Na TFF.Mfano in Refa aliyechezesha mechi baina ya Simba Na Yanga juzi Kwa kulikubali Goli la Mkono lililofungwa Na mchezaji Amis Tambwe wa Yanga.Kwa kuwa Refa Huyo in wa Basketball aliamini in goli halali
 
Back
Top Bottom