Kutokujua Sheria za Soka Chanzo cha Malalamiko ya Goli la Yanga!

Kutokujua Sheria za Soka Chanzo cha Malalamiko ya Goli la Yanga!

IMG_8156.jpg
V
 
Bangesyrup,
Mwaka 1995 Madaraka Selemani akiwa mchezaji wa Simba alifunga goli la kwanza la Simba dhidi ya Yanga kwa mkono na refa alilikubali, ulikuwa hujazaliwa? Kama ulizaliwa mbona hukulalamika hapa? Thiery Henry alifunga goli baadaya ya kuuseti mpira kwa mkono kwenye mechi za ku qualfy World Cup, Diego Armando Maradona alifunga goli la mkono dhidi ya England kwenye quarter final ya World Cup, jana kwenye EPL mechi ya Arsenal na Burnley Alex- Oxlade Chamberlain amefunga goli kupitia mkono wa Coexylin. Marefa ni binadamu wanafanya makosa pia, hata ukitoa machozi ya damu hapa haitabadili matokeo.
 
Umemaliza mkuu
 
Kwa hiyo unataka makosa ya marefa yasijadiliwe?
 
Na wewe lazima utakuwa miongoni mwa wavuta bange walioharibu viti pale uwanja wa Taifa, ngoja nilitaarifu jeshi la Polisi maana upuuzi wa namna hii hauvumiliki.
 
Kwa hiyo unataka makosa ya marefa yasijadiliwe?
Hata ukishinda hapa 24/7 unajadili makosa ya waamuuzi mwisho wa siku matokeo yatabaki vilevile na waamuzi kwakuwa ni binadamu basi nakuhakikishia makosa yataendelea kuwapo japokuwa hayatafanana mpaka siku ya kiyama.
 
Ni kweli usemacho lakini haiishii kwenye matokeo tu hata ukweli kuwa refa alikosea na makosa yakaifaidisha Yanga litabaki hivyo hivyo milele. Mijadala itaisha lakini hizo facts za matokeo na makosa zitabaki palepale
 
Nashauri Marefa wote wafanyiwe Uhakiki ili kuwaondoa Marefa wasio Na sifa.Imethibitika kuwa kuna idadi kubwa ya marefa wa BASKETBAALL lakini wamesajiliwa Na TFF.Mfano in Refa aliyechezesha mechi baina ya Simba Na Yanga juzi Kwa kulikubali Goli la Mkono lililofungwa Na mchezaji Amis Tambwe wa Yanga.Kwa kuwa Refa Huyo in wa Basketball aliamini in goli halali

mpira ni mchezo wa kusisimua na hayo matukio yanaufanya mchezo uendelee kuleta msisimko ndo mana ulaya walikuwa wanakataa goal technology mana inapunguza matukio ya utata yanayoufanya mchezo kuwa na msisimko henry aliivusha france kwa goli la mkono na jana uwanjani kwa burnley viti havikung'olewa kwa kuwa hayo ni matukio ya mpira yanayoufanya kuwa tata.
 
Mtoa post wewe Yanga damu so lazima utete tuuu hilo ni goli la mkono labda useme refa hakuona vizuri lakini Sio kusingizia watu hawajui sheria za Soka
 
Kwahio kuvunja viti ndo kudai haki?
utaona matokeo yake kunanchi baada ya ajira kukosekana kijana mmoja alijimwagia mafuta na kujiwasha uliza nini kilifata... hata kwa uhalibifu uliofanyika najua Simba itatugarimu lakini angalau tumeonyesha tunakerwa na huo uhuni wa tff na marefa wao...
 
We endelea kushangilia magamba huku kwenye mpira hapakufai...
 
Duh.....mwanzisha mada alipaswa kutuwekea hii picha pale mwanzo ili hata kina sie ambao ni yanga damu, tumuelewe vizuri!😀😀😀😀😀

Au hii picha nyie 'simba' mumeitengeneza (photoshop)?

Kwa hiyo baada ya hizi picha hitimisho ni kuwa mechi iliisha kwa 1-1 ama 1-0?🙄🙄

Namitakieni siku njema
 
Jinsi tukio la tambwe lilivyofanyika katika speed ya 4g hata Colina angeweka kati tu,mbona henry kashafanyaga hizo mambo mara nyingi tu,hawa wanalalamika kama mwanamke aliyepewa ujauzito bar.
Usimdhalilishe Peluig Colina
 
Acha uchambuzi wa kishabiki kila MTU aliona namna mkono ulivyofanya tambwe alitakiwa apewe kadi ndio maana marefa wenu ni was hapahapa
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Mojawapo ya mambo ambayo yanaudhi wakati mwingine ni watu kutolea maoni jambo ambalo hawalijui au hata kuchukua muda kulijua hasa kama liko ndani ya uwezo wao. Katika mechi hii ya leo goli la kwanza la Yanga dhidi ya watani wao wa jadi Simba limezua sokomoko uwanjani nan je ya uwanja. Maoni ya wengi ambao wanalipinga goli hilo ni madai kuwa refa “kawabeba” Yanga kwa sababu goli lile lilifungwa baada ya mchezaji kuunawa mpira yaani, kugusa mkono mpira wakati anapokea pasi.

Ni wazi kuwa wengi ambao wanafikiria mchezaji alifanya kosa lililohitaji faulu (free kick) wanafanya hivyo kwa sababu hawajui sheria za soka zinazohusu kuunawa mpira. Refa alikuwa sahihi kutokutoa faulu pale kwani hakukuvunjwa sheria zozote.

Kuelewa kama mchezaji alifanya kosa ni lazima turejee Kanuni za Mchezo ambazo zinatumika kuongoza mchezo wa Soka duniani. Kanuni hizi zimepitishwa na Shirikisho la Soka la Duniani (FIFA) na kama mtu hatosoma na kuelewa basi basi anaweza kufanya makosa ambayo mtu yeyote anayejua kanuni za mchezo huu hawezi kuyafanya. Bahati nzuri – nafahamu mchezo wa soka vizuri – na ninaweza kutolea maoni ambayo makocha na wachezaji wengine watakubaliana name kuhusiana na kutokuwepo kosa katika goli la kwanza la Yanga.

Kanuni za soka zinazohusu faulu mbalimbali (Kanuni ya 12) katika ukurasa wa 119 inaeleza wazi kuwa “Handling the ball involves a deliberate act of a player making contact with the ball with his hand or arm” yaani “Kuugusa mpira kwa mkono inahusisha kitendo cha mchezaji kwa makusudi kugusana na mpira kwa kiwiko chake au mkono”.

Sasa mojawapo ya mambo ambayo mwamuzi anatakiwa kuangalia kuhusiana na hili na ni jambo la kwanza kabisa – na ninaamini ndilo lililofamya refa kutokutoa faulu – ni kuangalia “mwelekeo wa mkono uliko mpira siyo wa mpira uliko mkono”. Hii ina maana kuwa endapo mpira unapigwa na mkono wa mchezaji hauufuati mpira – kama kuuzia, kubadilisha mwelekeo wake n.k – na mpira ukaenda ukagusa mkono bila kuonesha kusudio la mchezaji kuugusa mpira huo basi ni vigumu kutoa faulu au hata penati.

Ukielewa kanuni hii na ukipata muda kuangalia video ya goli la Yanga na ukimsikiliza mtangazaji unaweza kuamini kosa la mchezaji ni kuugusa mpira kwa mkono. Kosa kama hilo halipo kwenye kanuni za Soka! Hakuna kanuni inayokata mpira kugusa mkono; ipo kanuni inayokataza mchezaji kuugusa mpira kwa mkono wake kwa “makusudi” na neno la msingi sana hapa ni hilo la “kwa makusudi”. Kiingereza limetumia neno “deliberately”. Hii makusudi ina maana ya “nia, kusudio, kudhamiria”. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuona video ile na kudai kuwa ilikuwa ni kosa na refa hakuibeba Yanga bali amesimamia kanuni zinazoongoza mpira. Ni vizuri mashabiki, wachezaji na watu wengine wanaotolea maoni soka watumie muda kujifunza kanuni za mpira ili wasije kujikuta wanasababisha mambo ya aibu kama yaliyotokea leo uwanjani na kwenye mitandao ya kijamii.

Ni muhimu kujua sheria hizi ili kuondoa ulazima wa kufanya mambo ya uharibifu yaliyotokea uwanjani ambayo asili yake ni kutokujua kanuni za mchezo. Mashabiki wanapopata hasira kwa kitu ambacho hawakijui – wenyewe wakidhani wanazijua sheria zote za mchezo – ni aibu na kashfa kwa watu wote wanaopenda kandanda.

Upande wa pili, tumeona pia goli zuri, nono na tamu lilifungwa na Simba kupitia kona. Ni goli liliotumia nafasi ya uzembe wa golikipa kukaa kwenye kona. Bahati nzuri miaka yangu nikicheza soka nilicheza kama golikipa na goli kama hili linamuuma sana golikipa kwani anajua kosa lake ni kukaa mbali na posti ya goli wakati wa kona. Golikipa yeyote mzuri anajua wakati wa kona anatakiwa awe nyuma ya wachezaji wake wote kwani ni rahisi kwake kuupima mpira unaokuja kutoka kwenye kona na kuweza kukimbia mbele kwenye eneo lolote kuukoa. Ni vigumu sana kwa golikipa kukaa mbele ya wachezaji, au katikati na mpira ukajaa juu yake kama ilivyotokea leo; ni vigumu kurudi kinyume nyume kuuwahi mpira unaokuja kwenye posti. Hapa ndio uzuri wa goli hili ulipo.

Nje ya hapo, ni kweli tuna matatizo kwenye soka letu lakini inawezekana siyo tu tatizo la uchezaji lakini pia tatizo la kutokujua kanuni za mpira. Yeyote anayetaka kufundisha soka, kucheza au kushangilia soka ni vizuri ajifunze kanuni za msingi za mpira.

Unaweza kupata kanunizamchezo kwa kubonyeza hapa.
Umekuwa biased sana,..
Vipi kuhusu goli lililokataliwa la Ajib?
Ilikuwa offiside kweli au la..!?
Na kwa nini hukulielezea..??
 
Ata kwenye kampeni Nape alisikika akisema ata kwa bao la mkono mtashinda,

sasa kila mahali mnatafuta ushindi kwa bao la mkono,

Utakuwa ni mtu wa ajabu sana kukubaliana na lile bao la Yanga.
 
Mkuu tambwe aaaliiiuuuuvuuutaaa ule mpira nadhani liko wazi halina ubishi

mtamponza refa afungiwe bila kosa. Tambwe hakushika, sema mkono wakati anageuka ulikuwa umeenda sambamba na mpira. Ni bora ungesema Barthez kawapa simba goli sababu ya unazi wake kwa simba ningeelewa. Goli alilofungwa Barthez hata mtu anaejifunza ukipa hawezi fungwa!!!
 
Back
Top Bottom