Upekuzi101
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 478
- 1,025
17 March 2021 Rais John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano aliaga dunia. Pamoja na madhaifu yake kama binadamu ila ameacha legacy itakayodumu vizazi na vizazi. Ametuachia miradi mikubwa ya kimkakati ikiwepo SGR, bwala la Julius Nyerere, uboreshwaji wa huduma za kijamii ikiwepo shule barabara, maji na umeme.
Magufuli aliimarisha nidhamu katika utumishi wa umma na kutuongoza vyema wakati wa janga la korona.
Kwa machache hayo aliyoyafanya kwa Tanzania, ilikuwa ni heshima kwake japo serikali kutenga siku hii moja tu ya tarehe 17 March kila mwaka angalau kukumbuka na kuenzi yale mema yote aliyotuachia. Haieleweki kabisa mtu wa maana kama JPM kukosa heshima yake ndani ya nchi hii.
Mnafiki peke yake ndo anaweza kusema JPM hastahili heshima ya kumbukikizi kitaifa japo yote aliyoyoacha tunajiona.
Kuna nyakati inapaswa kuacha nongwa na kutoa heshima panopostahili. Kama baba wa Taifa anakumbukwa kwa harakati zake za kuleta uhuru wa kisiasa basi ni dhahiri kuwa John Pombe Magufuli alipambania uhuru wa kiuchumi kwa taifa letu na angalau matunda yanaonekana.
Tusipoyasema haya hata mawe barabarani yanaweza kusema mema ya huyu mwamba.
Kwa heshima kabisa niwatakie jioni njema na kumbukikizi ya kifo cha JPM. Tutakukumbuka kwa mema kamanda