Kutokuwepo na siku ya kumbukizi ya kifo cha JPM tarehe 17 Machi kila mwaka ni dhihaka kwa taifa

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
478
Reaction score
1,025
17 March 2021 Rais John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano aliaga dunia. Pamoja na madhaifu yake kama binadamu ila ameacha legacy itakayodumu vizazi na vizazi. Ametuachia miradi mikubwa ya kimkakati ikiwepo SGR, bwala la Julius Nyerere, uboreshwaji wa huduma za kijamii ikiwepo shule barabara, maji na umeme.

Magufuli aliimarisha nidhamu katika utumishi wa umma na kutuongoza vyema wakati wa janga la korona.

Kwa machache hayo aliyoyafanya kwa Tanzania, ilikuwa ni heshima kwake japo serikali kutenga siku hii moja tu ya tarehe 17 March kila mwaka angalau kukumbuka na kuenzi yale mema yote aliyotuachia. Haieleweki kabisa mtu wa maana kama JPM kukosa heshima yake ndani ya nchi hii.

Mnafiki peke yake ndo anaweza kusema JPM hastahili heshima ya kumbukikizi kitaifa japo yote aliyoyoacha tunajiona.

Kuna nyakati inapaswa kuacha nongwa na kutoa heshima panopostahili. Kama baba wa Taifa anakumbukwa kwa harakati zake za kuleta uhuru wa kisiasa basi ni dhahiri kuwa John Pombe Magufuli alipambania uhuru wa kiuchumi kwa taifa letu na angalau matunda yanaonekana.

Tusipoyasema haya hata mawe barabarani yanaweza kusema mema ya huyu mwamba.

Kwa heshima kabisa niwatakie jioni njema na kumbukikizi ya kifo cha JPM. Tutakukumbuka kwa mema kamanda
 
Magufuli hajafa alipalizwa
 
Si afadhali hata useme tuwe na kumbukumbu ya Mzee Ruksa aliyetkuta tukitembea uchi akatuvisha kuliko hilo shetani lenu la Chato
 
Anza kiifanya hapo nyumbani kwako wengine watafuata taratibu mkuu.
 
Huyo shetani ndiye aliyeharibu na kuiba kura 2019 na 2020 kuliko Rais ye yote aliyemtangulia! Huyo ndiye aliyevuruga demokrasia nchini!

Hivyo hastahili heshima yo yote!
 
Kifo ni kifo, hata mkifanya kumbukizi mwezi mzima haibadili chochote
 
Acha upuuzi. Unadhani kusimamisha siku nzima watu wasifanye kazi ni jambo dogo kwa uchumi wa nchi? Nyerere na Karume wanatosha.
Tunasimamishaga nchi kwa mambo mangapi? La JPM ndo litakuwa la ajabu? Acheni nongwa wanyalukolo...
 
Ukiona hawajafanya Kumbukizi FANYA WEWE.


View: https://www.youtube.com/watch?v=2MOqRexLKJc
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…