Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je, ni tatizo gani hili?

Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa. Je, ni tatizo gani hili?

Pole sana, punguza kula mivyakula migumu.
Usile kabisa mabumunda ya Wakinga, Ugali wa Kisukuma, Makande ya wapare, Macharari ya Wachagga, Mbalaga za Wanyakyusa na ule ugali wa ulezi unaopatikana Singida ni hatari kwa afya ya njia ya haja kubwa

BUJIBUJI mbona unapenda kuleta mzaha wakati mwenzio yupo seriuos? hebu acha bwana mwenzio apate msaada.
 
Pole kwa kuumwa.kuwa mwangalifu usije tapeliwa.Hilo yatizo ni kawaida linaitwa Haemorrhoids au Piles.Linatokana na mishipa inayoleta damu inayotokea tumboni kupitia mkunduni na kutoka nje kuminywa kwa muda mrefu.hasa kwa watu wanaokaa sn hasa madereva.hutengeneza buje na kuvimba na ukipata choo ngumu hupasuka na mavi yakigusa basi ni infection hapo.damu inatoka maumivu makali na hata homa...hakuna dawa ya kudumu ni kujitunza pale papone na pasipasuke tena.Kuna dawa inaitwa Pyloocain
 
mbona siwaelew wengine mnarumbana hapa badala ya kushauri ngoja viwapate
Mkuu Ngalewa wewe umeleta matatizo yako sasa unawaapiza watu yawakute badala ya wewe kuomba ushauri nini cha kufanya? Jaribu ukienda choo kaangalie sehemu ya haja yako kubwa kuna kijipele pembeni karaibu na tundu ya haja yako kubwa? kafanye utafiti kwanza huo kisha uje unipe feedback.

tatizo jingine wewe una matatizo ya Ukosefu wa kutopata choo laini hebu soma hapa chini

Namna ya kutibu ukosefu wa kutopata choo constipation


UKOSEFU wa kutopata choo laini ni tatizo sugu miongoni mwa watu wengi. Bila kujua kuwa ni tatizo ambalo linahitaji tiba ya haraka, watu wengi hupuuzia na kuona siyo tatizo kubwa na ni hali ya kawaida. Ukosefu wa choo wa muda mrefu, huwa ndiyo chanzo cha magonjwa mengine hatari.

Mtu anapokosa choo kikubwa kwa siku kadhaa, uchafu hujikusanya tumboni na unapokosa sehemu ya kutokea hukimbilia kwenye damu na kuingia kwenye mfumo mzima wa damu. Uchafu huo unapoingia kwenye mfumo wa damu huwa sumu na chanzo cha maradhi mengine ambayo hujitokeza baadae na kuanza kumuathiri mtu, bila kujua chanzo chake.

Kwa kawaida mtu unapaswa kupata choo cha uhakika japo mara moja kwa siku, kutegemeana na mlo wake wa kila siku, unapokosa choo kwa siku nzima ili hali una kula milo yote kwa siku, elewa una tatizo katika mfumo wako wa kusaga chakula hivyo unapaswa kuchukua hatua haraka.

MTU MWENYE TATIZO HILI ANA DALILI GANI?
Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa choo huwa na dalili kadhaa, ikiwemo kutumia nguvu na muda mwingi wakati wa kujisadia haja kubwa. Pili ulimi wake huwa na utandu mweupe na hutoa harufu mbaya mdomoni. Mtu huyu pia hukosa hamu ya chakula na wakati wote tumbo huwa limejaa.

NINI HUSABABISHA TATIZO?
Tatizo la ukosefu wa choo husababishwa zaidi na ulaji mbaya wa vyakula, kuacha kula matunda na mboga na staili mbaya ya maisha ikiwa ni pamoja na kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.

NINI KIFANYIKE?
Ili kuondoa tatizo kabla halijawa sugu, fanya moja miongoni mwa haya yafuatayo: Kunywa maji ya uvuguvugu asubuhi mapema, kisha tembea tembea, baada ya muda utasikia haja ya kwenda chooni. Ili usifanye haraka na upate muda wa kutosha kujiandaa kwenda kazini, amka mapema zaidi. Kula kiasi cha kutosha cha salad ya mboga mboga na juisi ya matunda halisi asubuhi kabla ya kula chochote.

Kila siku kabla ya kwenda kulala, kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali. Kunywa maji ya uvugu yaliyochanganywa na limau asubuhi na mapema kabla hujala kitu chochote. Kunywa ‘castor Oil’

muda mfupi kabla ya kwenda kulala. Ili kujiepusha kabisa na tatizo la ukosefu wa choo, jenga mazoea ya kunywa maji mengi, kula mboga na matunda kwa wingi kila siku na kuacha kabisa ulaji wa vyakula

vilivyoondolewa virutubisho kama vile mikate myeupe, ugali wa unga mweupe, keki vyakula vyenye sukari nyingi na vyakula vingine vitamu.
 
Last edited by a moderator:
sawa nitafanya kama ulivyonishauri yani huwa navusha hadi siku mbili au tatu bila kupata choo me huwa naenda mpaka yakibana na pia huwa najitahidi kunywa maji mengi
 
Jaribu kwenda medical center..inawezekana ni kichocho

huu uganga wa kienyeji sasa! huyu kachanika njia ya haja kubwa(ukiandika neno moja unapata ban! Sijui kiswahili kibovu, ila anus aaah safi tu!) inatakiwa anywe maji ya kutosha na vyakula laini. Pia asilazimishe haja.
 
Pole sana, punguza kula mivyakula migumu.
Usile kabisa mabumunda ya Wakinga, Ugali wa Kisukuma, Makande ya wapare, Macharari ya Wachagga, Mbalaga za Wanyakyusa na ule ugali wa ulezi unaopatikana Singida ni hatari kwa afya ya njia ya haja kubwa

mkuu mbona unatukosesha soko la mabumunda? Unataka ale zile takataka zatemeke?
 
Pole kwa kuumwa.kuwa mwangalifu usije tapeliwa.Hilo yatizo ni kawaida linaitwa Haemorrhoids au Piles.Linatokana na mishipa inayoleta damu inayotokea tumboni kupitia mkunduni na kutoka nje kuminywa kwa muda mrefu.hasa kwa watu wanaokaa sn hasa madereva.hutengeneza buje na kuvimba na ukipata choo ngumu hupasuka na mavi yakigusa basi ni infection hapo.damu inatoka maumivu makali na hata homa...hakuna dawa ya kudumu ni kujitunza pale papone na pasipasuke tena.Kuna dawa inaitwa Pyloochaemorrhoids ni painless bleeding. Ukiona kuna maumivu hiyo ni acutely thrombosed ambayo inahitaji operation haraka.! Yenye maumivu ni anal fissure ambazo hupona kwa kupunguza kutengeneza mavi magumu.
 
habari zunu wakuu mi nina ndugu yangu anatatizo anasema akiwa anajisaidia haja kubwa anasema kinyesi kinatoka na matone ya damu ingawa yeye anasema haoni dalili zozote za kuonesha anaumwa maana mpaka sasa hii wiki ya pili na kila nikimwambia aende hospitali anasema ni mzima , sasa mimi napata mashaka kwa sababu ni rafiki yangu nakuaga naye pamoja , je? kwa hali hiyo ni dalili ya ugonjwa gani?

Nawasilisha kwenu madoctor na wengine wanaojua
 
Kutoa kinyesi damu tu ni dalili ya ugonjwa inakuwaje anasema sio mgonjwa? Safula,na aina nyingine za minyoo na magonjwa ya tumbo hupelekea hilo tatizo,so kwa ushaur wangu amuone mtaalamu na mshaur wa mambo ya afya apate kuchunguzwa zaidi....


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
inakuwaje anasema sio mgonjwa? Safula,na aina nyingine za minyoo na magonjwa ya tumbo hupelekea hilo tatizo,hivyo kwa ushauri wangu amuone mtaalamu na mshauri wa mambo ya afya apate kuchunguzwa zaidi. TATIZO KUBWA YAWEZEKANA ANA VIDONDA VYA TUMBO
 
habari zunu wakuu mi nina ndugu yangu anatatizo anasema akiwa anajisaidia haja kubwa anasema kinyesi kinatoka na matone ya damu ingawa yeye anasema haoni dalili zozote za kuonesha anaumwa maana mpaka sasa hii wiki ya pili na kila nikimwambia aende hospitali anasema ni mzima , sasa mimi napata mashaka kwa sababu ni rafiki yangu nakuaga naye pamoja , je? kwa hali hiyo ni dalili ya ugonjwa gani?

Nawasilisha kwenu madoctor na wengine wanaojua

Wakati mwingine hii inasababishwa na diet tu, ajaribu kula matunda kama mapapai au ndizi mbivu. Wakati fulani unakuta ni kigumu sana na kinasabibisha michubuko kwenye njia. Hivyo ajaribu matunda hasa kama ndizi mbivu kila siku aangalie kama tatizo litaendelea aende hospitali.
 
mkuu inasababishwa na mlo mbaya na unywaji wa maji mbovu,,, mwambie ale mboga mboga kwa wingi maji mengi sana na pia asisahau matunda lazima kinyesi chake ni kigumu
 
Naomba ushauri na msaada kwani na baba yangu mdogo anatatizo akienda haja kubwa anajisaidia kinyesi damu pengine damu tu.

Naomba mnisaidie wadau nini tiba na cha kufanya ni nini?
 
Back
Top Bottom