Kutolewa kwenye mashindano Biashara united ni uzembe wa TFF na Waziri mwenye dhamana

Biashara hata kwenye semina elekezi iliyoendeshwa kwa vilabu vi 4 vilivyoshiriki kimataifa iliyoendeshwa na TFF hawakutuma muwakilishi wakidai hawana nauli.

We unaona hii timu iko serious?
Daa Bado TFF kama mlezi hakufatilia mwenendo wa Hawa jamaa akakaa kimya tu Ili Hali timu haieleweki

Yaani hapa TFF hakwepi lawama kama mlezi kutofatilia mwenendo wa Hawa jamaa kimataifa
 
Watanzania wamezoea lawama zisizo na msingi
TFF kama mlezi lawama lazima maana biashara alikuwa na viashiria vyote vya kushindwa kwenda anzia Iyo kuhudhuria semina, njoo mechi ya kwanza bado TFF hata hastuki

Pumbav sana wajiuzuru hao
 
Achen siasa za kishamba wizara na tff wanahusika vip apo wenye changamoto ni wao wenyewe biashara
Hapana! Serikali kwa haya masuala ya kimataifa inabidi iingilie kati, watu tunapigwa mitozo daily wanashindwa vipi kuisaidia timu? Au TFF ilishindwa nini kuikopesha Biashara halafu waje kuwakata kwenye fedha za udhamini wa ligu kuu? Mbona sasahivi udhamini wa ndani umeboreshwa maradufu?
 
Kutakuwa hakuna maana kwa tz kupewa nafasi nyingi, mtibwa yaliwakuta leo yanajirudia
 
Yaani kuna watu wa ajabu sana kama waliweza mpeleka konki likwidi na wenzie misri walishindwa vipi isafirisha biashara kwa kuikopesha?
 
Hivi TFF inaendeshwa kama familia? Kwamba hela inatoka tu baba akifurahi......
Au kama taasisi, wanakuwa na budget ya mwaka mzima?
 
Ilitakiwa afanyaje?
Afatilie mwenendo wa biashara maana tayari Alisha kuwa na mawenge tangu kikao cha maandalizi, safari ya kwanza Ili ingetokea shida kama hii (angetafuta plan B mapema)

Hata hii kuwakodia ndage ni wazo la waziri mkuu, bado TFF hawakuwa na wazo
Wao kama walezi kazi yao ni Ipi?
 
Hivi TFF inaendeshwa kama familia? Kwamba hela inatoka tu baba akifurahi......
Au kama taasisi, wanakuwa na budget ya mwaka mzima?
Kwamba budget huwa ujapangwa bila kuwa na kifungu cha dharura

Wangetumia kifungu cha dharura na Hawa mabwana wangerudisha kupitia viingilio na mapato mengine
 
Mkuu unaujua wajibu na majukumu ya TFF lakini....?
Hilo wala sio jukumu lake kutatua matatizo ya kiuchumi ya ndani ya Club, mazoea ya kuishi kijamaa ndio yanatuponza.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Hapana mkuu, wangeenda hata taasisi za fedha halafu tff akawa ndio mdhamana, biashara kamwe hawezi mkimbia tff, tff alipaswa kuhakikisha biashara anacheza hii mechi kwa gharama na njia zozote
 
Sioni kosa la TFF, ila kwa kuwa tumeamua kujifariji wacha tuwatupie lawama hao.....
Kwahiyo club kukosa nauli ni dharura? Kwanini walikubali kwenda kimataifa wakijua hawana hela.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Ila haijatangazwa rasmi kwamba wametolewa ni porojo za humu mitandaoni tu. Tunasubiri kusikia CAF wanasema nini.
 
Hapana mkuu, wangeenda hata taasisi za fedha halafu tff akawa ndio mdhamana, biashara kamwe hawezi mkimbia tff, tff alipaswa kuhakikisha biashara anacheza hii mechi kwa gharama na njia zozote
Taasisi haziendi hivyo mkuu, biashara kama club wanabeba asilimia 95 ya lawama.....wasijifariji.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unaujua wajibu na majukumu ya TFF lakini....?
Hilo wala sio jukumu lake kutatua matatizo ya kiuchumi ya ndani ya Club, mazoea ya kuishi kijamaa ndio yanatuponza.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
Unaelewa nacho zungumza ama

TFF ni mlezi wa vilabu, Hawa biashara ni wapya kimataifa tangu mwanzo walisha onesha uzembe kwenye mambo yao

TFF alitakiwa kama mlezi alitakiwa wasaidia huku akiwaangalia kwa karibu kama wataferi (asaidie Ana awasiliane na wizara husika kusaidia)

Jukumu la TFF kwenye haya mashindano ni lipi?
 
Doh...
Mkuu TFF waje wawasaidie kutembeza bakuli?
Maana japo lipo wazi ila wanaficha tatizo kubwa ni uchumi.
Hayo ni mambo ya ndani TFF hawezi ingilia masuala ya budget ya timu kamwe....
Kuna mambo ambayo ni majukumu ya tff kwa vilabu ila sio hili.....
VIONGOZI WA BIASHARA NI WAZEMBE,WAJIUDHURU.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Doh...
Mkuu TFF waje wawasaidie kutembeza bakuli?
Maana japo lipo wazi ila wanaficha tatizo kubwa ni uchumi.
Hayo ni mambo ya ndani TFF hawezi ingilia masuala ya budget ya timu kamwe....
Kuna mambo ambayo ni majukumu ya tff kwa vilabu ila sio hili.....
VIONGOZI WA BIASHARA NI WAZEMBE,WAJIUDHURU.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
Wapi nimesema TFF wasaidie kutembeza bakuri, nimesema TFF kama mlezi alitakiwa wafatilia hawa maana walisha onesha uzembe na kama angegundua mapema angewalipia na angekuja wakata kwenye mapato yao ya viingilio

Viongozi wa biashara kuwa wazembe sio la kuuliza na viongozi wa TFF kama walezi nao hawakwepi lawama
 
Aseee....
Awalipie aje awakate?.....
Ile ni taasisi ina utaratibu wake mkuu

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
FCaEmwnXsAUWxaQ
 
Katika hali yoyote ile inahuzunisha sana na ni aibu kubwa mno.Tunapoteza taswira iliyo njema sana.
 
Back
Top Bottom