nilijua ni mm mwenyewe napata hii changamoto!Ni muda mrefu sasa, yapata mwezi mfumo wa TMS Check wa polisi kitengo cha usalama barabarani haupo hewani. Hii inapelekea usumbufu kwa dereva kwa kutoweza kuangalia mwenyewe kama ameandikiwa fine ama lah. Hii hupelekea dereva kupata adha awapo barabarani ya kusimamishwa na trafic barabarani na kuambiwa kuwa anadaiwa anatakiwa alipe deni husika papo hapo ili aweze kuachiwa na kuondoka. Tunaomba wahusika watatue hilo tatizo mapema mana ishakuwa kero sasa..
Tuma plate number au namba ya leseni ,nijaribu kukuchekianilijua ni mm mwenyewe napata hii changamoto!
Wao wanatumia zile mashine zao (POS) kuangalia deni, na pia zile camera zao wanazotega pembezoni mwa barabara.Sasa hao traffic police wanapokusimamisha wakakuambia unadaiwa wanatumia Mfumo Gani?.. Otherwise sema kama wameshaanza kubambikiza watu kesi
Aisee hii app nimeijulia kwenye uzi huu tuseme tu jamaa aliyeidizain Kama NI mbongo apewe mauwa yake...Sasa nimeitumia karibu kila angle ..na mashaka kwenye parking fee mi sijawahio kuwa na Deni Ila Hari linasoma Deni... Ni nzuri kwa kweli maji umeme token kilankitu kimeungwa nadhani itakuja kuwa app ya muhimu zaidi kwenye simu...ndio maana naipenda jfunaweza kutumia app ya gepg tanzania pia na ukapata jawabu.