unge halijavunjwa, limeahirishwa tu,
Sasa Nini kimekengwa hapo?
Wataitwa tena kupitisha miswada tatika kipindi cha kuanzia 27 July hadi 3 Agosti 2025.
Leo hakutaka kutangaza wamekubali No Reforms No Election, lakini miswada ya dharura ya mabadiliko inategemea kutua bungeni kabla halijavunjwa rasmi tarehe 3 Agosti 2025.
TOKA MAKTABA :
Habari kwa kina :
Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo leo, Juni 23,2025 wakati akihutubia hotuba ya kulifunga baraza hilo huko Chukwani, Zanzibar, ambapo alisema ukomo wa Baraza la 10 utafikia mwisho Agosti 13 2025, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.
Amesema kwa mujibu wa Kifungu cha 91(2)(a) cha Sheria ya Zanzibar ya mwaka 1984, anayo mamlaka ya kuongeza muda wa Baraza hilo
Wakili msomi Edson Kilatu aliye pia mchambuzi wa maswala ya sera na katiba anatupitisha exclusively kuchambua mamlaka ya rais wa Jamhuri ya Muungano na pia rais wa SMZ katika kurefusha ukomo wa bunge au Baraza la Wawakilishi :
26 June 2025
BUNGE LA MUUNGANO DODOMA
Kwa upande wa Bunge la Dodoma je hali ipoje kisheria na kikatiba, wakili msomi anafafanua
View: https://m.youtube.com/watch?v=109seI462uQ
Wakili msomi Edson Kilatu : ibara ya 65 ya katiba ya 1977 kuhusu Bunge la Muungano kuvunjwa, bunge huvunjwa ikiwa limemaliza miaka 5 , pia ibara ya 90 inaweza kuvunjwa kabla ya wakati au ibara ya 91 kurefusha muda Bunge la Dodoma na la Baraza la Wawakilishi haitakiwi kutofautiana hivyo inawezekana Bunge la Dodoma kuongezewa muda ...
ikiwa ...
(3)
Muda wa maisha ya Bunge ukimalizika Bunge litahesabiwa kuwa limevunjwa;
isipokuwa kwamba muda huo ukiisha wakati wowote ambapo Jamhuri
ya Muungnao iko katika vita Bunge laweza mara
kwa mara kuongeza muda huo uliotajwa katika ibara
ya 65 ya Katiba hii kwa muda usiozidi miezi kumi na
miwili mara kwa mara lakini maisha ya Bunge hayawezi
kuongezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ndogo
hii kwa muda unaozidi miaka mitano.
(4) Kukitokea hali ya
hatari au kama
kuna hali ya
hatari ambayo Rais anaona inasababisha kuitisha
Mkutano wa Bunge na iwapo wakati huo Bunge limevunjwa na matokeo ya kura zilizo nyingi za Uchaguzi Mkuu hayajatangazwa basi Rais aweza kutoa Taarifa Maalum ya kuitisha Mkutano wa Bunge na kuagiza kwamba Spika na watu wote waliokuwa
Wabunge mara tu kabla Bunge halijavunjwa wahudhurie Mkutano huo wa Bunge na watu hao pamoja na huyo Spika, watahesabiwa kuwa ndio
Wajumbe wa Bunge kwa madhumuni ya Mkutano
huo na watahesabiwa hivyo mpaka usiku wa manane wa siku yatakapotangazwa matokeo ya kura zilizo nyingi za Uchaguzi Mkuu.
91.-(1) Rais atalihutubia Bunge Jipya katika Mkutano wake wa Kwanza na kulifungua rasmi
Bunge hilo.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ndogo ya
(1), Rais aweza wakati wowote kulihutubia Bunge
Rais aweza kulihutubia Bunge
Sheria ya 1984 Na. 15 ib.
14