Kutovunjwa bunge Leo Hadi hapo August, ni ishara ya kufanyika reforms kupata katiba mpya?

Kutovunjwa bunge Leo Hadi hapo August, ni ishara ya kufanyika reforms kupata katiba mpya?

Salaam!

Bunge halijavunjwa, limeahirishwa tu,

Sasa Nini kimelengwa hapo?

Ni kudhibiti wahamaji au ni mpango wa reforms kupata tume huru ya uchaguzi?

Karibuni 🙏
Bunge letu ni dhaifu mno, limetekwa mazima. Limekuwa bunge la serikali, hapa duniani hakuna bunge bovu kama hili
 
Sasa wewe unadhani litakuwa halijavunjwa kwa sababu gani???obviously hiyo ndio sababu ni lazima wawe cautious.Huwezi jua CDM huo msimamo wao unamanisha nini maana sio hali ya kawaida chama kikubwa cha upinzani kususia uchaguzu halafu ukabaki salama.
Ninamshangaa Zitto anapolinganisha ushawishi wa CDM huku bara dhidi ya ule wa ICT kule zanziba_hajui kuwa Zanzibar watu ni wachache unuweza kuwa handle kuliko huku.
Dogo ebu fuatilia taratibu za uvunjaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikoje miaka yote na muache kutuonesha ujinga na upumbavu wenu hapa JF.
 
Salaam!

Bunge halijavunjwa, limeahirishwa tu,

Sasa Nini kimelengwa hapo?

Ni kudhibiti wahamaji au ni mpango wa reforms kupata tume huru ya uchaguzi?

Karibuni 🙏
Yeriko Nyerere Jasusi la kidigitali anaweza kutudadavukia kinaga ubaga kwa nn mambo haya.
 
Mimi nina hakika CCM hatuwezi kuhalalisha uchaguzi Mkuu kwa kutumia CHAUMA na ACT Wazalendo.

Jumuiya za ndani ya nchi na za kimataifa zinakitambua CHADEMA kuwa ndiyo Chama kikuu Cha upinzani.

Jumuiya hizo pia zinatambua kuwa taratibu za uchaguzi haziko sawa.

Ikumbukwe kuwa Magufuli,pamoja na ubabe wake,lakini alihakikisha Chadema kinashiriki uchaguzi Mkuu.Hii ni kwa sababu katika nchi yoyote jambo linaloangaliwa kwa unzito mkubwa na wananchi na Jumuiya za kimataifa ni uchaguzi Mkuu.

Tujiulize kama nchi tunaweza kumudu uchaguzi utakaogharimu fedha yote halafu ustambuliwe na Watanzania walio wengi na Jumuiya ya kimataifa.Ni sawa na kupanda shamba kubwa na usivune chochote.

Madhara yake ni kutengwa na Jumuiya ya kimataifa,kukosa uwekezaji,kukosa misaada na mikopo.Hatuwezi kumudu kujiendesha bila misaada au mikopo.
Mapato yetu bado yako chini mno.
 
Back
Top Bottom