Kutovunjwa hoteli ya Desderia na Mikakati ya Serikali ya Magufuli

Mindi

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2008
Posts
3,523
Reaction score
4,998
Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali.

Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba" Freeman Mbowe ili asiweze kucheza mpira na hatimaye atolewe nje ya uwanja. Mbowe aliwekeza katika kilimo cha kisasa akitumia "Greenhouse". Uwekezaji huo ulivunjiliwa mbali kwa "kigezo" cha kuharibu chanzo cha maji, kama ilivyokuwa kwa hoteli ya Desderia.

Kipindi hicho nchi ilizizima kwa watendaji mbalimbali kila mmoja kujaribu kumpiku mwenzie, katika kuwatesa wapinzani, kuwaumiza, kuwadhibiti, na hata "kuwapoteza", ili kumfurahisha bwana mkubwa.

Wakati huo hatukumsikia mkulu akilia "Poo", bali tuliona vitendo hivyo vikishika kasi. Lengo? Kuua upinzani.

Kwa hiyo hii kali ya Desderia inatufanya tujiulize kulikoni?

Kuna hoja ya pili hapa. Miaka 5 ya kwanza, Rais Magufuli alionesha wazi chuki yake kwa wafanyabiashara kwa ujumla. Watendaji nao wakaunga mabehewa kwa kila mmoja kugeuka mtaalamu wa uwekezaji. Mwekezaji kuwekwa ndani masaa 48 ikawa jambo la kawaida. Adha za wapinzani ziliwasibu pia wawekezaji.

Mojawapo ya sera mbovu kabisa za JPM, ni kuhusu sera ya kodi, ambayo hata Rais Mwinyi wa Zanzibar kaikosoa hivi karibuni. Kwamba kupandisha kodi kunaleta madhara zaidi kuliko faida.

Magufuli mwenyewe ameazimia kufanya marekebisho katika kuvutia wawekezaji, kuwa na sera tofauti ya kodi, nk. Tumeshuhudia waziri wa fedha akichukua hatua kali kwa maafisa wa TRA. Inaonekana kale ka ushuzi ka "wanaofunga biashara ni wapiga dili", hata wao kamewachosha sasa.

Lakini inaonekana watendaji bado wanafikiria miaka 5 iliyopita, wakidhani kuharibu chochote kinachomilikiwa na mpinzani, ndio "maendeleo", tena ambayo "hayana vyama"

Kwa hili la Desderia, inaonekana Magufuli anakusudia kuua ndege angalau wawili kwa jiwe moja.

Kwanza kujifanya ni rafiki wa wapinzani. Hili limedhihirika pia kwa kauli ya Sugu "kumshukuru" mkulu, kurejewa kila kona, na wengine kutabiri Sugu atavuka mpaka na kuingia kwa Waggaggakikikoko.

Lakini inaonekana serikali ya Magufuli ni kama imeshituka katika mkakati wake wa "kuua" upinzani. Mojawapo ni ugunduzi kwamba kumbe kuna idadi ya wapinzani inahitajika bungeni. Ikalazimika kuibuka na mkakati wa COVID-19. Hivyo kwa pande hiyo karudisha majeshi nyuma. Pia hii "negative publicity" ya Lema na Lissu, ingeimarishwa zaidi kama Desderia "angeuwawa". Kwamba kweli wapinzani wanaandamwa.

Pili ni kukwepa sifa mbaya na kujiharibia katika mkakati wa kuvutia wawekezaji. Huko nyuma hakuyaona hayo? Watendaji walipodhalilisha wawekezaji kila kona ya nchi.
Tujadili
 
Mkuu

Hoja zako Matata Sana. Lakini JPM inaonesha anajua Sana like an intelligent person with a special agenda.

It is interesting to examine and scrutinize what, why, where, when and how he executes decisions. Simply unpredictable.

#WhereIsPrinceMakonda?
 
Hii issue ya Desderia Sugu ashukuru Mungu iligundulika mapema hivyo taarifa zake zikasambaa na kuharibu mipango yao wavunjaji.

Vinginevyo ingedondoshwa kama ilivyodondoshwa Billicanas pale city centre tena bila kufuata sheria yoyote, huu utawala wa huyu jamaa hakika kila mmoja wetu amelia kilio chake.
 
Mada hii AGAIN bado inaongelea utukufu wa no 1 ILA mtoa hoja haangalii upande wa pili wa story,Nchi inahitaji taasisi imara na huru sio strong no 1,hii issue ya Mr.Sugu ni ya kisheria ni mahakama ndio ingetoa hukumu au angalizo SIO no 1,watanzania tuamke kwa kutumia elimu yetu kutambua kuwa sio sahihi kwa president kuingilia issues za kisheria.
 
Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali.

Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba" Freeman Mbowe ili asiweze kucheza mpira na hatimaye atolewe nje ya uwanja. Mbowe aliwekeza katika kilimo cha kisasa akitumia "Greenhouse". Uwekezaji huo ulivunjiliwa mbali kwa "kigezo" cha kuharibu chanzo cha maji, kama ilivyokuwa kwa hoteli ya Desderia.

Kipindi hicho nchi ilizizima kwa watendaji mbalimbali kila mmoja kujaribu kumpiku mwenzie, katika kuwatesa wapinzani, kuwaumiza, kuwadhibiti, na hata "kuwapoteza", ili kumfurahisha bwana mkubwa.

Wakati huo hatukumsikia mkulu akilia "Poo", bali tuliona vitendo hivyo vikishika kasi. Lengo? Kuua upinzani.

Kwa hiyo hii kali ya Desderia inatufanya tujiulize kulikoni?

Kuna hoja ya pili hapa. Miaka 5 ya kwanza, Rais Magufuli alionesha wazi chuki yake kwa wafanyabiashara kwa ujumla. Watendaji nao wakaunga mabehewa kwa kila mmoja kugeuka mtaalamu wa uwekezaji. Mwekezaji kuwekwa ndani masaa 48 ikawa jambo la kawaida. Adha za wapinzani ziliwasibu pia wawekezaji.

Mojawapo ya sera mbovu kabisa za JPM, ni kuhusu sera ya kodi, ambayo hata Rais Mwinyi wa Zanzibar kaikosoa hivi karibuni. Kwamba kupandisha kodi kunaleta madhara zaidi kuliko faida.

Magufuli mwenyewe ameazimia kufanya marekebisho katika kuvutia wawekezaji, kuwa na sera tofauti ya kodi, nk. Tumeshuhudia waziri wa fedha akichukua hatua kali kwa maafisa wa TRA. Inaonekana kale ka ushuzi ka "wanaofunga biashara ni wapiga dili", hata wao kamewachosha sasa.

Lakini inaonekana watendaji bado wanafikiria miaka 5 iliyopita, wakidhani kuharibu chochote kinachomilikiwa na mpinzani, ndio "maendeleo", tena ambayo "hayana vyama"

Kwa hili la Desderia, inaonekana Magufuli anakusudia kuua ndege angalau wawili kwa jiwe moja.

Kwanza kujifanya ni rafiki wa wapinzani. Hili limedhihirika pia kwa kauli ya Sugu "kumshukuru" mkulu, kurejewa kila kona, na wengine kutabiri Sugu atavuka mpaka na kuingia kwa Waggaggakikikoko.

Lakini inaonekana serikali ya Magufuli ni kama imeshituka katika mkakati wake wa "kuua" upinzani. Mojawapo ni ugunduzi kwamba kumbe kuna idadi ya wapinzani inahitajika bungeni. Ikalazimika kuibuka na mkakati wa COVID-19. Hivyo kwa pande hiyo karudisha majeshi nyuma. Pia hii "negative publicity" ya Lema na Lissu, ingeimarishwa zaidi kama Desderia "angeuwawa". Kwamba kweli wapinzani wanaandamwa.

Pili ni kukwepa sifa mbaya na kujiharibia katika mkakati wa kuvutia wawekezaji. Huko nyuma hakuyaona hayo? Watendaji walipodhalilisha wawekezaji kila kona ya nchi.
Tujadili
Mkuu umeandika vizuri,hii hotel,hata kipindi Cha campaign ndo ulikuwa wimbo KWA Tim pinzani ya mh sugu, imesemwa wee ,ila yote KWA yote tushukuru mungu KWA kila Jambo,
 
Plotters wa Namba moja sijui hata wanafikiri nini, Nina shaka sio experienced kabisa matukio mengi wanafanya blender na kumuweka Njia panda Mtukufu. Wala Vumbi la Chaki aina ya KM na Mzee wa jalalani Sio watu wa kuwaamini wamejaa theory kiasi kwamba kuwatoa Jalalani haraka na kuwapa access kubwa ya information ni hatari sana, Wapo wazee wetu waliokulia ikulu kama Ukiambiwa fanya ivi ukakataa utapigwa tu they know well trendings
Kuna maamuzi yanafanywa ambayo huwaweka matatani Top officials mifumo yote lazima iwe balanced, Hakuna mkubwa kuliko system
 
Mleta mada nakubaliana nawe. Lkn na mm naongeza assumption yangu kuwa -yawezekana jiwe anajikomba kwa WanaMbeya kwa kujifanya anamtetea "rais" wao Sugu.

Kwasabb huyu huyu jiwe ndiye aliyemtuma Mnyeti kuharibu miundombinu ya kilimo Cha maua Cha Mbowe na kisha kumpatia uRC.
 
Magufuli yupo smart sana!

Very humble president our country has ever had. When his term ends that's when we'll understand.
Sexless nakuelewa mpenzi wangu!

Nikija TZ ukiwapo tuonane nikujuze nia njema ya huyu Baba kwenye nchi hii.

Mungu atujalie afya na uzima. insha'Allah!
 
Magufuli yupo smart sana!

Very humble president our country has ever had. When his term ends that's when we'll understand.

Nawasoma vizuri sana.

Huyu JPM approach yake ni another level. Inasemwa 2023 atatuletea katiba pendekezwa ya Jaji Warioba. Kwa sasa Nami nifunge domo langu nikisubiri yajayo ya 2023.
 
Magufuli atapita Tanzania itabaki, itakuwa muhimu sana kama Magufuli atatuachia taasisi imara ili nchi iendeshwe kwa kufuata utaratibu sio kufuata mawazo ya mtu kutegemeana siku hiyo kaamkaje. Atuachie mahakama imara, majeshi, DPP n.k bila hivyo akiondoka yeye tutarudi sifuri
 
Nakubaliana na mtoa mada pia Kwa mtazamo wangu naona magufuli amechoshwa na dhambi alizofanya Kwa wapinzani, sikuzote hapa duniani tenda mema Kwa watu na baraka zitakufuata
 
Kama aliweza vunja za Mbowe, kimara Hadi watoto wanalala chini ya miembe Kama wakimbizi. Hilo la Sugu ni malaika gani huyo amemshukia.
 
Nawasoma vizuri sana.

Huyu JPM approach yake ni another level. Inasemwa 2023 atatuletea katiba pendekezwa ya Jaji Warioba. Kwa sasa Nami nifunge domo langu nikisubiri yajayo ya 2023.
Nilihisi kuna jambo umeficha, nikataka kuuliza, but nikaamua kukaa kimya baada ya kuona sina maneno "laini" ya kutumia kwenye swali langu kwako.

Anyway, kumbe I was correct, na hili hapo juu ndilo jibu la swali langu nililotaka kukuuliza.
 
nikujuze nia njema ya huyu Baba kwenye nchi hii.
Hana nia njema huyu jiwe zaidi ya kutengeneza mazingira ya kusalia madarakani mpk atakapo rest in peace!

Ndiyo maana unaona anachukia upinzani na wapinzani kuliko maelezo.
 
Back
Top Bottom