Kutovunjwa hoteli ya Desderia na Mikakati ya Serikali ya Magufuli

Kutovunjwa hoteli ya Desderia na Mikakati ya Serikali ya Magufuli

Hana nia njema huyu jiwe zaidi ya kutengeneza mazingira ya kusalia madarakani mpk atakapo rest in peace!

Ndiyo maana unaona anachukia upinzani na wapinzani kuliko maelezo.
I feel you my friend!

Kufikia hitimisho ulilofikia ni haki yako. Lakini kuna mengi ukiyafahamu sitoshangaa ukibadilisha mtazamo wako.
 
Nakubaliana na mtoa mada pia Kwa mtazamo wangu naona magufuli amechoshwa na dhambi alizofanya Kwa wapinzani, sikuzote hapa duniani tenda mema Kwa watu na baraka zitakufuata
Siyo kwamba kachoshwa. Bali ameona hazikumlipa (hazikumsaidia) ktk kuwafanya wapiga kura wampende. Alichukiwa na kupigwa kumbo. Bila dola hivi Sasa angekuwa analima CHATO.

Sasa ameamua oubadili mbinu, ili lengo lake la kubadili katiba na kusalia madarakani litimie.
 
Nilihisi kuna jambo umeficha, nikataka kuuliza, but nikaamua kukaa kimya baada ya kuona sina maneno "laini" ya kutumia kwenye swali langu kwako.

Anyway, kumbe I was correct, na hili hapo juu ndilo jibu la swali langu nililotaka kukuuliza.

Huyu Mzee JPM ana moyo wa kipekee sana. Tuendako atashangaza watu, wengine wetu tutafurahi zaidi. Hizi maneno za tujitegemee anamaanisha.
 
Siyo kwamba kachoshwa. Bali ameona hazikumlipa (hazikumsaidia) ktk kuwafanya wapiga kura wampende. Alichukiwa na kupigwa kumbo. Bila dola hivi Sasa angekuwa analima CHATO.

Sasa ameamua oubadili mbinu, ili lengo lake la kubadili katiba na kusalia madarakani litimie.
Aweza kubadili katiba, lakini uwezekano ni kiduchu sana! Paranoia ndio nyingi!
 
Sugu alipata eneo kisheria wangevunja wangemlipa mara kumi ya thamani
 
Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali.

Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba" Freeman Mbowe ili asiweze kucheza mpira na hatimaye atolewe nje ya uwanja. Mbowe aliwekeza katika kilimo cha kisasa akitumia "Greenhouse". Uwekezaji huo ulivunjiliwa mbali kwa "kigezo" cha kuharibu chanzo cha maji, kama ilivyokuwa kwa hoteli ya Desderia.

Kipindi hicho nchi ilizizima kwa watendaji mbalimbali kila mmoja kujaribu kumpiku mwenzie, katika kuwatesa wapinzani, kuwaumiza, kuwadhibiti, na hata "kuwapoteza", ili kumfurahisha bwana mkubwa.

Wakati huo hatukumsikia mkulu akilia "Poo", bali tuliona vitendo hivyo vikishika kasi. Lengo? Kuua upinzani.

Kwa hiyo hii kali ya Desderia inatufanya tujiulize kulikoni?

Kuna hoja ya pili hapa. Miaka 5 ya kwanza, Rais Magufuli alionesha wazi chuki yake kwa wafanyabiashara kwa ujumla. Watendaji nao wakaunga mabehewa kwa kila mmoja kugeuka mtaalamu wa uwekezaji. Mwekezaji kuwekwa ndani masaa 48 ikawa jambo la kawaida. Adha za wapinzani ziliwasibu pia wawekezaji.

Mojawapo ya sera mbovu kabisa za JPM, ni kuhusu sera ya kodi, ambayo hata Rais Mwinyi wa Zanzibar kaikosoa hivi karibuni. Kwamba kupandisha kodi kunaleta madhara zaidi kuliko faida.

Magufuli mwenyewe ameazimia kufanya marekebisho katika kuvutia wawekezaji, kuwa na sera tofauti ya kodi, nk. Tumeshuhudia waziri wa fedha akichukua hatua kali kwa maafisa wa TRA. Inaonekana kale ka ushuzi ka "wanaofunga biashara ni wapiga dili", hata wao kamewachosha sasa.

Lakini inaonekana watendaji bado wanafikiria miaka 5 iliyopita, wakidhani kuharibu chochote kinachomilikiwa na mpinzani, ndio "maendeleo", tena ambayo "hayana vyama"

Kwa hili la Desderia, inaonekana Magufuli anakusudia kuua ndege angalau wawili kwa jiwe moja.

Kwanza kujifanya ni rafiki wa wapinzani. Hili limedhihirika pia kwa kauli ya Sugu "kumshukuru" mkulu, kurejewa kila kona, na wengine kutabiri Sugu atavuka mpaka na kuingia kwa Waggaggakikikoko.

Lakini inaonekana serikali ya Magufuli ni kama imeshituka katika mkakati wake wa "kuua" upinzani. Mojawapo ni ugunduzi kwamba kumbe kuna idadi ya wapinzani inahitajika bungeni. Ikalazimika kuibuka na mkakati wa COVID-19. Hivyo kwa pande hiyo karudisha majeshi nyuma. Pia hii "negative publicity" ya Lema na Lissu, ingeimarishwa zaidi kama Desderia "angeuwawa". Kwamba kweli wapinzani wanaandamwa.

Pili ni kukwepa sifa mbaya na kujiharibia katika mkakati wa kuvutia wawekezaji. Huko nyuma hakuyaona hayo? Watendaji walipodhalilisha wawekezaji kila kona ya nchi.
Tujadili
Nasikitika kusema watanzania hatuko halisi katika mengi,Bila kubadilika kwa dhati,hali yetu kama taifa itazidi kuwa mbaya mno.
 
Huyu Mzee JPM ana moyo wa kipekee sana. Tuendako atashangaza watu, wengine wetu tutafurahi zaidi. Hizi maneno za tujitegemee anamaanisha.
Sikushangai kwa huu mtazamo, nimeongea na wengi wanaoishi nje ya nchi huu wako ndio msimamo wao pia, waswahili wana msemo wao "utamu wa ngoma uingie uicheze"

Karibuni.
 
Siyo kwamba kachoshwa. Bali ameona hazikumlipa (hazikumsaidia) ktk kuwafanya wapiga kura wampende. Alichukiwa na kupigwa kumbo. Bila dola hivi Sasa angekuwa analima CHATO.

Sasa ameamua oubadili mbinu, ili lengo lake la kubadili katiba na kusalia madarakani litimie.
Kwa kuongezea

Sisi tuliobahatika kuona utawala wa Rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli tunaona tofauti Sana namna Magufuli anavyotanguliza maslahi ya nchi.

Ijapokuwa sio perfect 100%, lakini kulinganisha anachofanya na viongozi wa nchi zingine wanachofanya "patriotism" inatia moyo Sana kwamba at last we have a president who portrays himself as a protector of our natural wealth.

Kunaweza kuwa na shida kwenye methodologies, lakini dhumuni lake ni mujarabu Sana. Mungu amsaidie afanikiwe!
 
Mkuu

Hoja zako Matata Sana. Lakini JPM inaonesha anajua Sana like an intelligent person with a special agenda.

It is interesting to examine and scrutinize what, why, where, when and how he executes decisions. Simply unpredictable.

#WhereIsPrinceMakonda?
Ahsante sana mkuu, ila natofautiana nawe. Kama Magufuli angekuwa kweli "very intelligent", asingeirejesha nchi katika maabara ya majaribio ambayo Nyerere na waliomfuata walishayafanya na matokeo yanajulikana. Kudharau sekta binafsi na kuivuruga kabisa, baada ya uwekezaji mkubwa uliofanyika, huku kila mtu mwwnye akili za kawaida tu alitambua hilo, sio kuonesha "intelligence" ya pekee. Haikuhitaji miaka 5 ya kubomoa ili ajenge tena.

Unawezaje kurundika tenda zote TBA? Au kutumia majeshi?

Lakini nakubali kwamba JPM ana uwezo mkubwa wa kukomaa hata kama kitu kinaumiza wengi . Mfano bomoabomoa, kubomoa maghorofa, makanisa, misikiti bila hoja za msingi, tena kwa kutumia sheria ya enzi za mwanzo za ukoloni, unawamaskiniza raia wako bila huruma? Aaaa, hapo hapana
 
I hear you.

Idea zipo Sawa Ila methodologies zina shida. Wanaopaswa kumsaidia wamsaidie ipasavyo!
 
Magufuli yupo smart sana!

Very humble president our country has ever had. When his term ends that's when we'll understand.
Aaaah wapi, watakaomkumbuka ni wale aliowapa nafasi za ulaji.
 
Hata mtoto wa darasa la 5 anaweza kuandika vizuri na kueleweka anachotaka kusema kuliko wewe, haueleweki unachanganya mambo, mtu akisoma mpaka mwisho unasubiri kile ulichotaka kukisema hakionekani ni kama vile bado haujamalizia kuandika, ...
 
Basi bado hujamsoma vizuri jiwe. The man is arrogant and self-important.
I could be wrong!
But he has categorically painted on the wall that no one will attract richness based on his/her public office.
 
Ijapokuwa sio perfect 100%, lakini kulinganisha anachofanya na viongozi wa nchi zingine wanachofanya "patriotism" inatia moyo Sana kwamba at last we have a president who portrays himself as a protector of our natural wealth.
Huo uzalendo huwa ndiyo kichaka wanavhotumia madikteta wengi kusalia madarakani.

Uhuru, haki na Maendeleo ya watu ndiyo mambo tunayahitaji watanzania kwa Sasa.
 
Back
Top Bottom