Kutovunjwa hoteli ya Desderia na Mikakati ya Serikali ya Magufuli

Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali.

Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba" Freeman Mbowe ili asiweze kucheza mpira na hatimaye atolewe nje ya uwanja. Mbowe aliwekeza katika kilimo cha kisasa akitumia "Greenhouse". Uwekezaji huo ulivunjiliwa mbali kwa "kigezo" cha kuharibu chanzo cha maji, kama ilivyokuwa kwa hoteli ya Desderia.

Kipindi hicho nchi ilizizima kwa watendaji mbalimbali kila mmoja kujaribu kumpiku mwenzie, katika kuwatesa wapinzani, kuwaumiza, kuwadhibiti, na hata "kuwapoteza", ili kumfurahisha bwana mkubwa.

Wakati huo hatukumsikia mkulu akilia "Poo", bali tuliona vitendo hivyo vikishika kasi. Lengo? Kuua upinzani.

Kwa hiyo hii kali ya Desderia inatufanya tujiulize kulikoni?

Kuna hoja ya pili hapa. Miaka 5 ya kwanza, Rais Magufuli alionesha wazi chuki yake kwa wafanyabiashara kwa ujumla. Watendaji nao wakaunga mabehewa kwa kila mmoja kugeuka mtaalamu wa uwekezaji. Mwekezaji kuwekwa ndani masaa 48 ikawa jambo la kawaida. Adha za wapinzani ziliwasibu pia wawekezaji.

Mojawapo ya sera mbovu kabisa za JPM, ni kuhusu sera ya kodi, ambayo hata Rais Mwinyi wa Zanzibar kaikosoa hivi karibuni. Kwamba kupandisha kodi kunaleta madhara zaidi kuliko faida.

Magufuli mwenyewe ameazimia kufanya marekebisho katika kuvutia wawekezaji, kuwa na sera tofauti ya kodi, nk. Tumeshuhudia waziri wa fedha akichukua hatua kali kwa maafisa wa TRA. Inaonekana kale ka ushuzi ka "wanaofunga biashara ni wapiga dili", hata wao kamewachosha sasa.

Lakini inaonekana watendaji bado wanafikiria miaka 5 iliyopita, wakidhani kuharibu chochote kinachomilikiwa na mpinzani, ndio "maendeleo", tena ambayo "hayana vyama"

Kwa hili la Desderia, inaonekana Magufuli anakusudia kuua ndege angalau wawili kwa jiwe moja.

Kwanza kujifanya ni rafiki wa wapinzani. Hili limedhihirika pia kwa kauli ya Sugu "kumshukuru" mkulu, kurejewa kila kona, na wengine kutabiri Sugu atavuka mpaka na kuingia kwa Waggaggakikikoko.

Lakini inaonekana serikali ya Magufuli ni kama imeshituka katika mkakati wake wa "kuua" upinzani. Mojawapo ni ugunduzi kwamba kumbe kuna idadi ya wapinzani inahitajika bungeni. Ikalazimika kuibuka na mkakati wa COVID-19. Hivyo kwa pande hiyo karudisha majeshi nyuma. Pia hii "negative publicity" ya Lema na Lissu, ingeimarishwa zaidi kama Desderia "angeuwawa". Kwamba kweli wapinzani wanaandamwa.

Pili ni kukwepa sifa mbaya na kujiharibia katika mkakati wa kuvutia wawekezaji. Huko nyuma hakuyaona hayo? Watendaji walipodhalilisha wawekezaji kila kona ya nchi.
Tujadili

Nadhani ameanza kutambua kuna maisha baada ya uRais.

Miaka mitano itapita kwa kasi ya ajabu,hakuna sababu ya msingi ya kuumiza waTanzania kwa kisingizio au hoja dhaifu za ulinzi wa mazingira.

Ukienda Serengeti mto Grumeti kuna mwekezaji kajenga hotel ukingoni mwa mto Nyumbu wakivuka mto mgeni anawaona akiwa chumbani.Hizi hoja za Nemc sijui blah blah hazina tofauti nyundo za TRA au kubambikiwa kesi za utakatishaji fedha au uhujumu uchumi.

Hoja hizi zilitumiwa sana na Mh Lissu kipindi cha kampeni kama tungekuwa na Tume huru hakika tungekuwa na hadithi nyingine wakati huu.
 
Huo uzalendo huwa ndiyo kichaka wanavhotumia madikteta wengi kusalia madarakani.

Uhuru, haki na Maendeleo ya watu ndiyo mambo tunayahitaji watanzania kwa Sasa.
Hili la Magufuli kulazimisha urais baada ya 2025 ni agenda mahsusi kumchafua.

Mungu atujalie zawadi ya uzima tuione 2025. Tujue ukweli.
 
I feel you my friend!

Kufikia hitimisho ulilofikia ni haki yako. Lakini kuna mengi ukiyafahamu sitoshangaa ukibadilisha mtazamo wako.
Ebu yazungumze ili tubadili mitazamo yetu
 
I could be wrong!
But he has categorically painted on the wall that no one will attract richness based on his/her public office.
That's why he keeps on paralyzing systems and avenues of economy.

So you think we are happy with him? The leader who is embracing and upholding poverty!!!!?
 
Magufuli statistical acceptability
50% likes him
30% hates him
20% are undecided

Mbaya zaidi hakuna mbadala wa ukweli kumng'oa Magufuli!
 
Mungu atujalie zawadi ya uzima tuione 2025. Tujue ukweli.
Nilidhani kuna mikakati maalumu ya kumzuia. Kumbe tunamwachia Mungu!!???

Mambo ya siasa yaliyojaa ushetani na Mungu wapi na wapi?
 
Magufuli statistical acceptability
50% likes him
30% hates him
20% are undecided

Mbaya zaidi hakuna mbadala wa ukweli kumng'oa Magufuli!
What is your credible and reliable source for these statistics?
 
Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali.

Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba" Freeman Mbowe ili asiweze kucheza mpira na hatimaye atolewe nje ya uwanja. Mbowe aliwekeza katika kilimo cha kisasa akitumia "Greenhouse". Uwekezaji huo ulivunjiliwa mbali kwa "kigezo" cha kuharibu chanzo cha maji, kama ilivyokuwa kwa hoteli ya Desderia.

Kipindi hicho nchi ilizizima kwa watendaji mbalimbali kila mmoja kujaribu kumpiku mwenzie, katika kuwatesa wapinzani, kuwaumiza, kuwadhibiti, na hata "kuwapoteza", ili kumfurahisha bwana mkubwa.

Wakati huo hatukumsikia mkulu akilia "Poo", bali tuliona vitendo hivyo vikishika kasi. Lengo? Kuua upinzani.

Kwa hiyo hii kali ya Desderia inatufanya tujiulize kulikoni?

Kuna hoja ya pili hapa. Miaka 5 ya kwanza, Rais Magufuli alionesha wazi chuki yake kwa wafanyabiashara kwa ujumla. Watendaji nao wakaunga mabehewa kwa kila mmoja kugeuka mtaalamu wa uwekezaji. Mwekezaji kuwekwa ndani masaa 48 ikawa jambo la kawaida. Adha za wapinzani ziliwasibu pia wawekezaji.

Mojawapo ya sera mbovu kabisa za JPM, ni kuhusu sera ya kodi, ambayo hata Rais Mwinyi wa Zanzibar kaikosoa hivi karibuni. Kwamba kupandisha kodi kunaleta madhara zaidi kuliko faida.

Magufuli mwenyewe ameazimia kufanya marekebisho katika kuvutia wawekezaji, kuwa na sera tofauti ya kodi, nk. Tumeshuhudia waziri wa fedha akichukua hatua kali kwa maafisa wa TRA. Inaonekana kale ka ushuzi ka "wanaofunga biashara ni wapiga dili", hata wao kamewachosha sasa.

Lakini inaonekana watendaji bado wanafikiria miaka 5 iliyopita, wakidhani kuharibu chochote kinachomilikiwa na mpinzani, ndio "maendeleo", tena ambayo "hayana vyama"

Kwa hili la Desderia, inaonekana Magufuli anakusudia kuua ndege angalau wawili kwa jiwe moja.

Kwanza kujifanya ni rafiki wa wapinzani. Hili limedhihirika pia kwa kauli ya Sugu "kumshukuru" mkulu, kurejewa kila kona, na wengine kutabiri Sugu atavuka mpaka na kuingia kwa Waggaggakikikoko.

Lakini inaonekana serikali ya Magufuli ni kama imeshituka katika mkakati wake wa "kuua" upinzani. Mojawapo ni ugunduzi kwamba kumbe kuna idadi ya wapinzani inahitajika bungeni. Ikalazimika kuibuka na mkakati wa COVID-19. Hivyo kwa pande hiyo karudisha majeshi nyuma. Pia hii "negative publicity" ya Lema na Lissu, ingeimarishwa zaidi kama Desderia "angeuwawa". Kwamba kweli wapinzani wanaandamwa.

Pili ni kukwepa sifa mbaya na kujiharibia katika mkakati wa kuvutia wawekezaji. Huko nyuma hakuyaona hayo? Watendaji walipodhalilisha wawekezaji kila kona ya nchi.
Tujadili
Kwani JPM aliongeza kodi yeyote katika kipindi chake cha kwanza??? Au ni wimbo wa "Saccos" kuhusu enforcement ya sheria za kodi na nidhamu kwa wafanyakazi kuongezeka au Wewe unapendelea watoza kodi wala rushwa na wazembe
 
Mada hii AGAIN bado inaongelea utukufu wa no 1 ILA mtoa hoja haangalii upande wa pili wa story,Nchi inahitaji taasisi imara na huru sio strong no 1,hii issue ya Mr.Sugu ni ya kisheria ni mahakama ndio ingetoa hukumu au angalizo SIO no 1,watanzania tuamke kwa kutumia elimu yetu kutambua kuwa sio sahihi kwa president kuingilia issues za kisheria.
Watanzania wanapenda/wanatamani kujenga taasisi.

Lakini hawapo tayari ku-sacrifice ili taasisi ziimarike!

Mkuu ujenzi wa taasisi ni vita maana kuna watu watapoteza "ulaji" wao! Migogoro iliyomuondoa Membe CCM ni ushahidi mmoja WA kujenga taasisi.

How many bold people do we have in our country who are ready to relinquish their personal benefits for the country success? Hiyo bado hujatupiwa Jini kipande ukafie mbele ili watu waneemeshe matumbo Yao.

Most of Tanzanian high profile leaders are just selfish aka wajumbe!
 
Mtu anayepata zaidi ya 10@month huyo halii njaa bali analeta uchuro.
10 millions/month kwa uchumi huu? (i.e. us$ 4000?)

ha ha ha 🤣 wanawachota akili nanyi mnaamini. Sad!
 
I hear you.

Idea zipo Sawa Ila methodologies zina shida. Wanaopaswa kumsaidia wamsaidie ipasavyo!
Sishauriki. Ukinishauri ndiyo umeharibu. Hata kama unaishi nje ya nchi ulitakiwa kujitahidi kufuatilia miaka mitano ya kwanza, usingepata shida sana.
 
Perceptions is a challenge.
You know what, challenge is accepted!
 
What is your credible and reliable source for these statistics?

Very much expected question for obvious answers.

Please do not expect holy answers from anyone including me. Take some trouble, use your research skill to gather information from government and non governmental departments. Then extend that endeavour to gather information from international organizations.

My conclusion is simple, Magufuli regime hasn't promoted growth of democratic quarters. This isn't a mistake, it's purposefully default. In commerce we term it "opportunity cost". Is it right or wrong? Judge for yourself.
 
Nilidhani kuna mikakati maalumu ya kumzuia. Kumbe tunamwachia Mungu!!???

Mambo ya siasa yaliyojaa ushetani na Mungu wapi na wapi?

Utawala wa nchi na Mambo yake Mungu mwenyewe aliruhusu!

Usome kitabu cha 1 Samuel 8-12 kwa kuanzia. Usome kwa utuo uelewe kwa undani.

Best wishes
 
Mkuu

Hoja zako Matata Sana. Lakini JPM inaonesha anajua Sana like an intelligent person with a special agenda.

It is interesting to examine and scrutinize what, why, where, when and how he executes decisions. Simply unpredictable.

#WhereIsPrinceMakonda?
mtaishi Kama mashetani - JPM 2016
 
mtaishi Kama mashetani - JPM 2016

Yeah

He said and it is happening!

Was it a lie? No, it wasn't!

Recently he said, yeyote atakaye kula pesa za umma, Naye ajiandae kuliwa. Na tunaona wakubwa "wanaliwa".

He does what he says...so proud of him!

Can we safely say Magufuli is an angel, no we cannot say that. He is a human and he is bound to make mistakes during his tenure!
 
I feel you my friend!

Kufikia hitimisho ulilofikia ni haki yako. Lakini kuna mengi ukiyafahamu sitoshangaa ukibadilisha mtazamo wako.
Mkuu kumpiga mpizani risasi 30 Ni opportunity cost, you must be joking
 
Sina ushahidi wa mashambulizi ya risasi kuwa ni maelekezo ya Rais Magufuli. Kama unao ushahidi, go ahead and make your case!

Nijuavyo, from biblical time watawala wa Dunia hii -presidents, kings, queen- are entitled with licence to kill.

Take it or leave it.
 
Back
Top Bottom