Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali.
Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba" Freeman Mbowe ili asiweze kucheza mpira na hatimaye atolewe nje ya uwanja. Mbowe aliwekeza katika kilimo cha kisasa akitumia "Greenhouse". Uwekezaji huo ulivunjiliwa mbali kwa "kigezo" cha kuharibu chanzo cha maji, kama ilivyokuwa kwa hoteli ya Desderia.
Kipindi hicho nchi ilizizima kwa watendaji mbalimbali kila mmoja kujaribu kumpiku mwenzie, katika kuwatesa wapinzani, kuwaumiza, kuwadhibiti, na hata "kuwapoteza", ili kumfurahisha bwana mkubwa.
Wakati huo hatukumsikia mkulu akilia "Poo", bali tuliona vitendo hivyo vikishika kasi. Lengo? Kuua upinzani.
Kwa hiyo hii kali ya Desderia inatufanya tujiulize kulikoni?
Kuna hoja ya pili hapa. Miaka 5 ya kwanza, Rais Magufuli alionesha wazi chuki yake kwa wafanyabiashara kwa ujumla. Watendaji nao wakaunga mabehewa kwa kila mmoja kugeuka mtaalamu wa uwekezaji. Mwekezaji kuwekwa ndani masaa 48 ikawa jambo la kawaida. Adha za wapinzani ziliwasibu pia wawekezaji.
Mojawapo ya sera mbovu kabisa za JPM, ni kuhusu sera ya kodi, ambayo hata Rais Mwinyi wa Zanzibar kaikosoa hivi karibuni. Kwamba kupandisha kodi kunaleta madhara zaidi kuliko faida.
Magufuli mwenyewe ameazimia kufanya marekebisho katika kuvutia wawekezaji, kuwa na sera tofauti ya kodi, nk. Tumeshuhudia waziri wa fedha akichukua hatua kali kwa maafisa wa TRA. Inaonekana kale ka ushuzi ka "wanaofunga biashara ni wapiga dili", hata wao kamewachosha sasa.
Lakini inaonekana watendaji bado wanafikiria miaka 5 iliyopita, wakidhani kuharibu chochote kinachomilikiwa na mpinzani, ndio "maendeleo", tena ambayo "hayana vyama"
Kwa hili la Desderia, inaonekana Magufuli anakusudia kuua ndege angalau wawili kwa jiwe moja.
Kwanza kujifanya ni rafiki wa wapinzani. Hili limedhihirika pia kwa kauli ya Sugu "kumshukuru" mkulu, kurejewa kila kona, na wengine kutabiri Sugu atavuka mpaka na kuingia kwa Waggaggakikikoko.
Lakini inaonekana serikali ya Magufuli ni kama imeshituka katika mkakati wake wa "kuua" upinzani. Mojawapo ni ugunduzi kwamba kumbe kuna idadi ya wapinzani inahitajika bungeni. Ikalazimika kuibuka na mkakati wa COVID-19. Hivyo kwa pande hiyo karudisha majeshi nyuma. Pia hii "negative publicity" ya Lema na Lissu, ingeimarishwa zaidi kama Desderia "angeuwawa". Kwamba kweli wapinzani wanaandamwa.
Pili ni kukwepa sifa mbaya na kujiharibia katika mkakati wa kuvutia wawekezaji. Huko nyuma hakuyaona hayo? Watendaji walipodhalilisha wawekezaji kila kona ya nchi.
Tujadili
Hii issue ya Desderia Sugu ashukuru Mungu iligundulika mapema taarifa zake zikasambaa na kuharibu mipango yao wavunjaji.
Mkuu umeandika vizuri,hii hotel,hata kipindi Cha campaign ndo ulikuwa wimbo KWA Tim pinzani ya mh sugu, imesemwa wee ,ila yote KWA yote tushukuru mungu KWA kila Jambo,Tukio la hivi karibuni la Rais Magufuli kutoa agizo la kuzuia "uvunjwaji" wa hoteli kubwa ya nyota tatu, inayomilikiwa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya, maarufu "Sugu", linaibua hoja mbalimbali.
Tukirejea miaka 5 ya kwanza ya Magufuli, DC Sabaya wa Hai, anaonekana alipewa "kazi" maalum ya "kumkaba" Freeman Mbowe ili asiweze kucheza mpira na hatimaye atolewe nje ya uwanja. Mbowe aliwekeza katika kilimo cha kisasa akitumia "Greenhouse". Uwekezaji huo ulivunjiliwa mbali kwa "kigezo" cha kuharibu chanzo cha maji, kama ilivyokuwa kwa hoteli ya Desderia.
Kipindi hicho nchi ilizizima kwa watendaji mbalimbali kila mmoja kujaribu kumpiku mwenzie, katika kuwatesa wapinzani, kuwaumiza, kuwadhibiti, na hata "kuwapoteza", ili kumfurahisha bwana mkubwa.
Wakati huo hatukumsikia mkulu akilia "Poo", bali tuliona vitendo hivyo vikishika kasi. Lengo? Kuua upinzani.
Kwa hiyo hii kali ya Desderia inatufanya tujiulize kulikoni?
Kuna hoja ya pili hapa. Miaka 5 ya kwanza, Rais Magufuli alionesha wazi chuki yake kwa wafanyabiashara kwa ujumla. Watendaji nao wakaunga mabehewa kwa kila mmoja kugeuka mtaalamu wa uwekezaji. Mwekezaji kuwekwa ndani masaa 48 ikawa jambo la kawaida. Adha za wapinzani ziliwasibu pia wawekezaji.
Mojawapo ya sera mbovu kabisa za JPM, ni kuhusu sera ya kodi, ambayo hata Rais Mwinyi wa Zanzibar kaikosoa hivi karibuni. Kwamba kupandisha kodi kunaleta madhara zaidi kuliko faida.
Magufuli mwenyewe ameazimia kufanya marekebisho katika kuvutia wawekezaji, kuwa na sera tofauti ya kodi, nk. Tumeshuhudia waziri wa fedha akichukua hatua kali kwa maafisa wa TRA. Inaonekana kale ka ushuzi ka "wanaofunga biashara ni wapiga dili", hata wao kamewachosha sasa.
Lakini inaonekana watendaji bado wanafikiria miaka 5 iliyopita, wakidhani kuharibu chochote kinachomilikiwa na mpinzani, ndio "maendeleo", tena ambayo "hayana vyama"
Kwa hili la Desderia, inaonekana Magufuli anakusudia kuua ndege angalau wawili kwa jiwe moja.
Kwanza kujifanya ni rafiki wa wapinzani. Hili limedhihirika pia kwa kauli ya Sugu "kumshukuru" mkulu, kurejewa kila kona, na wengine kutabiri Sugu atavuka mpaka na kuingia kwa Waggaggakikikoko.
Lakini inaonekana serikali ya Magufuli ni kama imeshituka katika mkakati wake wa "kuua" upinzani. Mojawapo ni ugunduzi kwamba kumbe kuna idadi ya wapinzani inahitajika bungeni. Ikalazimika kuibuka na mkakati wa COVID-19. Hivyo kwa pande hiyo karudisha majeshi nyuma. Pia hii "negative publicity" ya Lema na Lissu, ingeimarishwa zaidi kama Desderia "angeuwawa". Kwamba kweli wapinzani wanaandamwa.
Pili ni kukwepa sifa mbaya na kujiharibia katika mkakati wa kuvutia wawekezaji. Huko nyuma hakuyaona hayo? Watendaji walipodhalilisha wawekezaji kila kona ya nchi.
Tujadili
Sexless nakuelewa mpenzi wangu!Magufuli yupo smart sana!
Very humble president our country has ever had. When his term ends that's when we'll understand.
Magufuli yupo smart sana!
Very humble president our country has ever had. When his term ends that's when we'll understand.
Shetani katu hawezi kuwa malaika.Tunabadilika kuelekea kuzuri zaidi....
Nilihisi kuna jambo umeficha, nikataka kuuliza, but nikaamua kukaa kimya baada ya kuona sina maneno "laini" ya kutumia kwenye swali langu kwako.Nawasoma vizuri sana.
Huyu JPM approach yake ni another level. Inasemwa 2023 atatuletea katiba pendekezwa ya Jaji Warioba. Kwa sasa Nami nifunge domo langu nikisubiri yajayo ya 2023.
Hana nia njema huyu jiwe zaidi ya kutengeneza mazingira ya kusalia madarakani mpk atakapo rest in peace!nikujuze nia njema ya huyu Baba kwenye nchi hii.