Kumekuwa na utaratibu wa kutozwa fedha kwa wanafunzi wanaoenda kwenye taasisi mbalimbali za serikali kujifunza kwa vitendo. Hii ni sehemu ya kujifunza na pia kusaidia majukumu ya taasisi husika kwa kipindi fulani.
Badala yake, wanafunzi ndio wanaoombwa pesa nyingi ili kupata nafasi hiyo. Utaratibu wa kulipa ni kwa siku, wiki, na hata kwa mwezi. Mfano: mwanafunzi anaombwa kulipa elfu tano kwa siku kwa muda wa miezi mitatu na zaidi.
Je, serikali imezingatia hali za wanafunzi kama:
- Kipato cha mwanafunzi, ikiwa hana chanzo kingine zaidi ya wazazi maskini.
- Jukumu la ulipaji ada chuoni, ambapo hulipa ada sawa akiwa darasani.
- Gharama za nauli na chakula.
- Majukumu anayopatiwa.
Sasa tujiulize sote: je, suala hili ni sahihi kwa kundi hili linalohitaji jicho la upekee sana ili kutimiza ndoto na malengo ya kuijenga kesho bora? Ikiwa kijana anasoma kwa mateso na gharama nyingi, na baada ya hapo anarudi kuungana na jamii inayohitaji ajiajiri, mtaji unatoka wapi ikiwa alimaliza fedha kutafuta nafasi ya kujifunza kwa vitendo?