Kutumika Mbwa kwenye uokoaji Syria na Uturuki

Mbwa bado anaonekana ni kiumbe chenye msaada sana kwa binadamu. Kwa sasa Mbwa anatumia sana kwenye nchi ambazo zimepata majanga ya tetemeko Hivi karibuni yaani Syria na Uturuki.
Najiuliza nchi hizi ni za kiislamu vipi kuruhusu Mbwa atumike wakati kwa uislamu Mbwa ni najisi. Nauliza tu kupata uelewa siyo vita.
Waarabu wanawinda kwa kutumia mbwa na mbwa akikamata mawindo ndipo mawindo ni halali na mbwa hugeuka haramu papo hapo....unafiki haunaga rangi
 
Maneno yaliyokusanywa miaka 200 baada ya mtume kufa unakuwa na uhakika gani ni ya mtume!?... Qur'an imesema yenyewe ni nyepesi kueleweka,wewe unadai ngumu kueleweka,unabishana nayo!?
Kama utauweza mjadala kwa hekma na maarifa na adabu na utii pasi na dharau na kejeli karibu.

Sisi tuna ahadi na allah subhaanah ya kuihifadhi dini yake na kuiepusha na kubadilishwa kama yalivyofanywa mafundisho yaliyotangulia kwa mitume wengine, na jambo la pili ni kuwa mapokeo yetu ya kiislamu yamelindwa na sanad huu ni mtiririko wa wapokezi na hapa kuna vigezo vigumu sana vimewekwa kuhakikisha habari iliyopokelewa ni sahihi, hassan, dhaifu au ya kutungwa.

Ukiyajua hayo sasa tutakuja kwenye malengo ya kuandikwa hadithi kwanini hazikuandikwa mwanzo zikaja kuandikwa baadae?.

Mwisho nikuulize wewe unaswali!? kama ndio umejuaje namna ya kuswali? wakati kwenye quran hakuna pahala pa muongozo wa namna ya kuswali?.

karibu.
 
Muislamu hata akibidi kuwa na mbwa wa ulinzi, anapaswa amweke nje ya nyumba; uani au sehemu ambayo si ndani ya nyumba ili kuepuka kutiliwa najisi vyombo, nguo na sehemu za kufanyia 'ibaadah.
Vipi najisi ya mipanya na mimende
 
Waarabu wanawinda kwa kutumia mbwa na mbwa akikamata mawindo ndipo mawindo ni halali na mbwa hugeuka haramu papo hapo....unafiki haunaga rangi
Ushahidi upo wapi ,,tunaaminije hizi porojo zako
 
Unajua unajisi wa mbwa unakuja vipi, au ukoje? Unajua kama ni ruksa kufuga mbwa?

Mbwa mwenyewe hawezi kusemwa ni najisi kwa kutokuwa na dalili ya hilo, isipokuwa mate yake na majimaji ya puani mwake yanachukuliwa ni najisi ki-Shariy’ah ikiwa ni wa kufuga au vinginevyo kwa dalili iliyopatikana kutoka katika Hadiyth. Na kwa hivyo chombo chochote ambacho kitarambwa na mbwa kinapaswa kutwaharishwa kwa kuoshwa mara saba bila kutofautisha ni mbwa gani aliyekiramba, mojawapo kwa mchanga. Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kukitwahirisha chombo kilichorambwa na mbwa kunafanywa kwa kuosha mara saba, mojawapo kwa udongo” [Ahmad, Muslim, Abu Daawuwd na al-Bayhaqiy]

Na ikiwa ataramba chombo chenye chakula kikavu, kile chakula kilichoguswa na mdomo wa mbwa na kilicho pembezoni mwake kinatakiwa kitupwe, ama kilichobaki ni twahara kinaweza kubakishwa. Ama manyoya ya mbwa yakiwa makavu ni twahara. Sehemu iliyo najisi ya mbwa ni ule mdomo wake kwa ajili ya umandemande.

Hivyo, mtu kucheza na mbwa au kumpakata na kumfanya ni kichezeo, si jambo lenye kushauriwa kwa kupatikana uwezekano wa kunuswa au kurambwa nguo yake na maeneo ya kuswalia na sehemu mbalimbali za nyumba yake. Mbwa si kama paka, hivyo si jambo zuri watu kuiga tabia za wasio Waislamu na wao kuanza kufuga mbwa wa vichezeo na kuwafanya kama paka. Muislamu hata akibidi kuwa na mbwa wa ulinzi, anapaswa amweke nje ya nyumba; uani au sehemu ambayo si ndani ya nyumba ili kuepuka kutiliwa najisi vyombo, nguo na sehemu za kufanyia 'ibaadah.
Mbwa anapokamata mawindo je mate hayawezi kugusa mawindo?
Iweje nyama iliyokamatwa na mbwa sio najisi?
 
Maneno yaliyokusanywa miaka 200 baada ya mtume kufa unakuwa na uhakika gani ni ya mtume!?... Qur'an imesema yenyewe ni nyepesi kueleweka,wewe unadai ngumu kueleweka,unabishana nayo!?
Hiyo Qur'an yenyewe ndio imeeleza kuwa mtume ameletwa kuwabainishia watu kile kilichoteremeshwa kwao.

"..... na tumekuteremshia wewe ukumbusho ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, na ili wapate kutafakari."
Qur'an 16:44
 
Kama utauweza mjadala kwa hekma na maarifa na adabu na utii pasi na dharau na kejeli karibu.

Sisi tuna ahadi na allah subhaanah ya kuihifadhi dini yake na kuiepusha na kubadilishwa kama yalivyofanywa mafundisho yaliyotangulia kwa mitume wengine, na jambo la pili ni kuwa mapokeo yetu ya kiislamu yamelindwa na sanad huu ni mtiririko wa wapokezi na hapa kuna vigezo vigumu sana vimewekwa kuhakikisha habari iliyopokelewa ni sahihi, hassan, dhaifu au ya kutungwa.

Ukiyajua hayo sasa tutakuja kwenye malengo ya kuandikwa hadithi kwanini hazikuandikwa mwanzo zikaja kuandikwa baadae?.

Mwisho nikuulize wewe unaswali!? kama ndio umejuaje namna ya kuswali? wakati kwenye quran hakuna pahala pa muongozo wa namna ya kuswali?.

karibu.
Swala kwa mujibu wa Qur'an nimedarisisha wiki hii nzima,Sasa hivi wenzio wananiuliza kuhusu hija...unajua khalifa ummar r.a historia yake na hadithi!?.. Qur'an ni wahyi jibril alileta,Hadith alileta nani huo wahyi!?..
 
Hiyo Qur'an yenyewe ndio imeeleza kuwa mtume ameletwa kuwabainishia watu kile kilichoteremeshwa kwao.

"..... na tumekuteremshia wewe ukumbusho ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, na ili wapate kutafakari."
Qur'an 16:44
Ukumbushi si ni Qur'an hapo!!
 
Swala kwa mujibu wa Qur'an nimedarisisha wiki hii nzima,Sasa hivi wenzio wananiuliza kuhusu hija...unajua khalifa ummar r.a historia yake na hadithi!?.. Qur'an ni wahyi jibril alileta,Hadith alileta nani huo wahyi!?..
Mpaka hapa wewe ni katika quraaniyyuun lakini tutakwenda sawa, leta ushahidi wa namna ya kuswali kwa mujibu wa quran wala hakuna haja ya wiki nzima leta sasa hivi hapa ushahidi wa namna ya kuswali kwa mujibu wa quran.

Ama suala la pili sisi tumeambiwa kuwa mtume swala na salaam ziwe juu yake hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake isipokuwa anachokizungumza ni wahyi, wewe hulijui hili? hautambui kuwa hadithi ni aina miongoni mwa aina za wahyi? haujui kuwa kuna maneno ya allah kama hadith qudsiyy nayo sio quran wala ukiyasoma hupati ajri kama ile ya kusoma quran?.

"wala yeye{mtume} hatamki kwa matamanio"
Qur'an 53:3

Dini yetu ya kiislamu imejengwa juu ya quran na sunnah, na uislamu ndio sunnah na sunnah ndio uislamu.
 
Mkuu kuna hulka ya watu kuvamia vitu ambavyo wana taarifa zake kwa juu juu tu.
Hebu jihabarishe ni katika mazingira gani mbwa anakuwa najisi.
So unajisi wa mbwa ni pale tu ambapo hana msaada au siyo?
 
Mafundisho ya uislamu yamebainisha tofauti baina ya mbwa mwenye mafunzo na mbwa koko tu mzururaji, huyu mwenye mafunzo akikamata kiwindwa kuna hukmu yake na huyu mbwa koko asiyeelewa lolote akikamata pia kuna hukmu yake, haya si mageni yametajwa kwenye uislamu.

Wala mkuu huwezi kupata upenyo wa kuusema uislamu kwa hoja hata siku moja, labda uamue tu mwenyewe kwa ubishi, ama dini ya kiislamu imeyataja yote hayo na wanawachuoni allah awarehemu wameyanukuu katika vitabu vyao vya mambo ya fiqhi huko kwenye milango ya الصيد و الذبائح.
 
Mpaka hapa wewe ni katika quraaniyyuun lakini tutakwenda sawa, leta ushahidi wa namna ya kuswali kwa mujibu wa quran wala hakuna haja ya wiki nzima leta sasa hivi hapa ushahidi wa namna ya kuswali kwa mujibu wa quran.

Ama suala la pili sisi tumeambiwa kuwa mtume swala na salaam ziwe juu yake hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake isipokuwa anachokizungumza ni wahyi, wewe hulijui hili? hautambui kuwa hadithi ni aina miongoni mwa aina za wahyi? haujui kuwa kuna maneno ya allah kama hadith qudsiyy nayo sio quran wala ukiyasoma hupati ajri kama ile ya kusoma quran?.

"wala yeye{mtume} hatamki kwa matamanio"
Qur'an 53:3

Dini yetu ya kiislamu imejengwa juu ya quran na sunnah, na uislamu ndio sunnah na sunnah ndio uislamu.
So mtume aliposema kwa wakeze 'chakula Cha Jana kilikua kitamu' huo ulikua wahyi!?
 
Mafundisho ya uislamu yamebainisha tofauti baina ya mbwa mwenye mafunzo na mbwa koko tu mzururaji, huyu mwenye mafunzo akikamata kiwindwa kuna hukmu yake na huyu mbwa koko asiyeelewa lolote akikamata pia kuna hukmu yake, haya si mageni yametajwa kwenye uislamu.

Wala mkuu huwezi kupata upenyo wa kuusema uislamu kwa hoja hata siku moja, labda uamue tu mwenyewe kwa ubishi, ama dini ya kiislamu imeyataja yote hayo na wanawachuoni allah awarehemu wameyanukuu katika vitabu vyao vya mambo ya fiqhi huko kwenye milango ya الصيد و الذبائح.
Naona baraza la ULAMAA mnachuana sio?
 
".....ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao.."

tuseme hauoni hicho kipande?.
QUR'AN 3:187
Na pale mwenyezi Mungu alipofungamana na waliopewa kitabu kuwa lazima 'mtabainishia' watu,Wala hamtokificha,walikitupa nyuma ya migongo yao,na wakanunua kwacho thamani duni...
Hapa watu wa kitabu walishushiwa 'wahyi(hadithi' kwa muktadha wako,maana walitakiwa wawabainishie watu!!...
 
Hakuna sehemu yeyote ambayo uislam unakataza kifuga mbwa bali kinacho katazwa ni kumshika shika hovyo baadhi ya sehemu zake hasa mdomoni.
 
Back
Top Bottom