Kutumika Mbwa kwenye uokoaji Syria na Uturuki

Kutumika Mbwa kwenye uokoaji Syria na Uturuki

Mbwa bado anaonekana ni kiumbe chenye msaada sana kwa binadamu. Kwa sasa Mbwa anatumia sana kwenye nchi ambazo zimepata majanga ya tetemeko Hivi karibuni yaani Syria na Uturuki.

Najiuliza nchi hizi ni za kiislamu vipi kuruhusu Mbwa atumike wakati kwa uislamu Mbwa ni najisi. Nauliza tu kupata uelewa siyo vita.
Nyie mafarisayo muwe mnauliza basi jmni sio kila siku kuamka na kuudhihaki Uislamu ilihali ww umemezeshwa ujinga mtupu

Mbwa kutumika kwenye shughuli kma hizo hakuna shida yyte mna kwa apo ameonekana ni kiumbe ambae anaweza kusaidia uokoaji
Mbwa anaruhusiwa kutumika kwenye uwindaji pia lkn kilichokatazwa ni kule kucheza na mbwa na kuwakumbatia kma watoto
We huoni kinyaa mbwa akikuramba ? Tuanze hpa kwanza
 
Kwa hiyo uko uturuki wanapokwenda kunusa na kulambalamba kuokoa manusura , mji mzima unabidi utawazwe mara saba?, akilamba manusura inabidi naye akatawazwe mara saba?

Baniani mbaya kiatu chake dawa
Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapa hatukulaumu
 
sheikh wangu mbwa Hana unajisi wowote,si mate Wala maji ya pua,ndiyo maana wwngine hadithi hatuzitaki,zinazua mengi.

QUR'AN 5:4

Wanakuuliza wamehalalishiwa nini?..sema mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na 'mlichowafundisha WANYAMA kuwinda....'
Yani ata huyu kafiri alotoa hii post anajua kua mbwa ni najisi ww umekaza fuvu lako eti unakataaa pole sanaaa we mjinga mpotofu
 
Yani ata huyu kafiri alotoa hii post anajua kua mbwa ni najisi ww umekaza fuvu lako eti unakataaa pole sanaaa we mjinga mpotofu
Huyo Kama ni kadiri na anajua mbwa ni nahisi basi anajua hivyo kwa kuwa waislam wanasema hivyo,lakini Qur'an 5:4 inasemaje!?
 
Yani ata huyu kafiri alotoa hii post anajua kua mbwa ni najisi ww umekaza fuvu lako eti unakataaa pole sanaaa we mjinga mpotofu
Matusi Tena sheikh wangu!!!?..wajinga na wapotofu ni wewe na wenzako mnaofuata maneno ya watu na kumzulia Allah uwongo Kisha mkasema haya yanatoka kwa Allah
 
Sijui mwenzetu uko madhehebu gani lakini kwa waislamu mate ya mbwa ni najisi. Lakini imeruhusiwa kufuga mbwa kwa ajili ya ulinzi.

Hebu tuambie huyo shekhe wako aliyekwambia kuwa mbwa siyo najisi.
Mimi nimetoka Aya ya Qur'an 5:4,kwenye uislam kila Jambo ni halali mpaka liharamishwe,mwenye kuharamisha ni Allah sw pekee kupitia Qur'an,siyo sheikh Wala mufti
 
Huwa nina kawaida moja kama nikiona tunaanza kupoteza muda basi nakubali kushindwa mjadala, kwa mtindo huu unaokwenda nao tunaelekea huko.
Mjadala huwezi,endelea tu na shughuli zako,kajadiliane na wenzio wanaotia matusi kwenye mjadala
 
Unajua unajisi wa mbwa unakuja vipi, au ukoje? Unajua kama ni ruksa kufuga mbwa?

Mbwa mwenyewe hawezi kusemwa ni najisi kwa kutokuwa na dalili ya hilo, isipokuwa mate yake na majimaji ya puani mwake yanachukuliwa ni najisi ki-Shariy’ah ikiwa ni wa kufuga au vinginevyo kwa dalili iliyopatikana kutoka katika Hadiyth. Na kwa hivyo chombo chochote ambacho kitarambwa na mbwa kinapaswa kutwaharishwa kwa kuoshwa mara saba bila kutofautisha ni mbwa gani aliyekiramba, mojawapo kwa mchanga. Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kukitwahirisha chombo kilichorambwa na mbwa kunafanywa kwa kuosha mara saba, mojawapo kwa udongo” [Ahmad, Muslim, Abu Daawuwd na al-Bayhaqiy]

Na ikiwa ataramba chombo chenye chakula kikavu, kile chakula kilichoguswa na mdomo wa mbwa na kilicho pembezoni mwake kinatakiwa kitupwe, ama kilichobaki ni twahara kinaweza kubakishwa. Ama manyoya ya mbwa yakiwa makavu ni twahara. Sehemu iliyo najisi ya mbwa ni ule mdomo wake kwa ajili ya umandemande.

Hivyo, mtu kucheza na mbwa au kumpakata na kumfanya ni kichezeo, si jambo lenye kushauriwa kwa kupatikana uwezekano wa kunuswa au kurambwa nguo yake na maeneo ya kuswalia na sehemu mbalimbali za nyumba yake. Mbwa si kama paka, hivyo si jambo zuri watu kuiga tabia za wasio Waislamu na wao kuanza kufuga mbwa wa vichezeo na kuwafanya kama paka. Muislamu hata akibidi kuwa na mbwa wa ulinzi, anapaswa amweke nje ya nyumba; uani au sehemu ambayo si ndani ya nyumba ili kuepuka kutiliwa najisi vyombo, nguo na sehemu za kufanyia 'ibaadah.
SAwa shekhe lakini..Mbwa tunawaona wanatumika hawajafunikwa pia Wala midomo Yao sasa hiyo najisi Inaepukika vp wakati hao Mbwa wananussa mpaka sehemu manusura walipo
 
Kama hukubali kuhusu Hadithi za Mtume basi uislam wako una kasoro. Huwezi kuwa muislamu sahihi kisha ukatae hadithi za Mtume.
sheikh wangu mbwa Hana unajisi wowote,si mate Wala maji ya pua,ndiyo maana wwngine hadithi hatuzitaki,zinazua mengi.

QUR'AN 5:4

Wanakuuliza wamehalalishiwa nini?..sema mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na 'mlichowafundisha WANYAMA kuwinda....'
 
waislamu wanakwambia usitumie vya kafiri wakati hiyo simu na elimu ya kumtibu yeye imetoka huko.
hapo ndipo nilipowaona akili hakuna.
binadamu umepewa vyote duniani kuvitumia iweje usingizie mungu.
Unaushahid juu ya hili ulivyo kua mpumbavu hata Babu zetu walijitibia wenyewe
 
Kama hukubali kuhusu Hadithi za Mtume basi uislam wako una kasoro. Huwezi kuwa muislamu sahihi kisha ukatae hadithi za Mtume.
Una uhakika gani kuwa hizo ni hadithi za mtume kweli ikiwa mtu wake wa karibu (khalifa ummar)alizipiga marufuku,zimekusanywa na kandikwa miaka zaidi ya 150 baada ya mtume kufa,kwa nini mtume hakuagiza ziandikwe,kwa nini zinapingana/zua dhidi ya Qur'an!?
 
Mbwa bado anaonekana ni kiumbe chenye msaada sana kwa binadamu. Kwa sasa Mbwa anatumia sana kwenye nchi ambazo zimepata majanga ya tetemeko Hivi karibuni yaani Syria na Uturuki.

Najiuliza nchi hizi ni za kiislamu vipi kuruhusu Mbwa atumike wakati kwa uislamu Mbwa ni najisi. Nauliza tu kupata uelewa siyo vita.
Hawa jamaa wakibanwa njaa hata kitimoto anaruhusiwa kula.
 
Una uhakika gani kuwa hizo ni hadithi za mtume kweli ikiwa mtu wake wa karibu (khalifa ummar)alizipiga marufuku,zimekusanywa na kandikwa miaka zaidi ya 150 baada ya mtume kufa,kwa nini mtume hakuagiza ziandikwe,kwa nini zinapingana/zua dhidi ya Qur'an!?
Nimekuita kwenye mjadala unaniletea hoja ya vinamba namba, swala kwa mujibu wa quran iko wapi!?.

Umar amepinga hadithi za mtume? kuandikwa miaka 150 baada ya kufa kwa mtume kuna ubaya gani ikiwa wakati wake na wakati wa maswahaba hakukuwa na haja ya kufanya hivyo? kabla hujakimbilia kwenye hadithi kwanini haushangai quran kukusanywa baada ya kufa kwa mtume kwa miaka kadhaa?.
 
Back
Top Bottom