Kutumika Mbwa kwenye uokoaji Syria na Uturuki

Kutumika Mbwa kwenye uokoaji Syria na Uturuki

Unajua unajisi wa mbwa unakuja vipi, au ukoje? Unajua kama ni ruksa kufuga mbwa?

Mbwa mwenyewe hawezi kusemwa ni najisi kwa kutokuwa na dalili ya hilo, isipokuwa mate yake na majimaji ya puani mwake yanachukuliwa ni najisi ki-Shariy’ah ikiwa ni wa kufuga au vinginevyo kwa dalili iliyopatikana kutoka katika Hadiyth. Na kwa hivyo chombo chochote ambacho kitarambwa na mbwa kinapaswa kutwaharishwa kwa kuoshwa mara saba bila kutofautisha ni mbwa gani aliyekiramba, mojawapo kwa mchanga. Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kukitwahirisha chombo kilichorambwa na mbwa kunafanywa kwa kuosha mara saba, mojawapo kwa udongo” [Ahmad, Muslim, Abu Daawuwd na al-Bayhaqiy]

Na ikiwa ataramba chombo chenye chakula kikavu, kile chakula kilichoguswa na mdomo wa mbwa na kilicho pembezoni mwake kinatakiwa kitupwe, ama kilichobaki ni twahara kinaweza kubakishwa. Ama manyoya ya mbwa yakiwa makavu ni twahara. Sehemu iliyo najisi ya mbwa ni ule mdomo wake kwa ajili ya umandemande.

Hivyo, mtu kucheza na mbwa au kumpakata na kumfanya ni kichezeo, si jambo lenye kushauriwa kwa kupatikana uwezekano wa kunuswa au kurambwa nguo yake na maeneo ya kuswalia na sehemu mbalimbali za nyumba yake. Mbwa si kama paka, hivyo si jambo zuri watu kuiga tabia za wasio Waislamu na wao kuanza kufuga mbwa wa vichezeo na kuwafanya kama paka. Muislamu hata akibidi kuwa na mbwa wa ulinzi, anapaswa amweke nje ya nyumba; uani au sehemu ambayo si ndani ya nyumba ili kuepuka kutiliwa najisi vyombo, nguo na sehemu za kufanyia 'ibaadah.
Jambo la kushukuru sana kwa ufafanuzi huu
Watu wajifunze bila jazba
 
Kama shida ni 'yubayyin' basi Hilo neno lipo pia kwenye 3:187......
Sawa.

"Na kumbuka pale allah alipochukua ahadi na wale waliopewa kitabu kuwa: naapa mtawabainishia watu na wala hamtokificha, basi walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwa kitabu hicho thamani ndogo{ya dunia} basi ni kiovu hicho walichokinunua.."
Qur'an 3:187

Sasa nifahamishe hizi habari za mayahudi na wakristo zinahusiana vipi na mada yetu.
 
waislamu wanakwambia usitumie vya kafiri wakati hiyo simu na elimu ya kumtibu yeye imetoka huko.
hapo ndipo nilipowaona akili hakuna.
binadamu umepewa vyote duniani kuvitumia iweje usingizie mungu.
 
QUR'AN 3:187
Na pale mwenyezi Mungu alipofungamana na waliopewa kitabu kuwa lazima 'mtabainishia' watu,Wala hamtokificha,walikitupa nyuma ya migongo yao,na wakanunua kwacho thamani duni...
Hapa watu wa kitabu walishushiwa 'wahyi(hadithi' kwa muktadha wako,maana walitakiwa wawabainishie watu!!...
Mkuu hili jambo la kujifanya huelewi nilikutahadharisha mwanzo wa mjadala, hao watu wa kitabu walilazimishwa na hiyo ahadi kuwa watawafundisha watu taurati na injili wala wasifiche mengine na wakafundisha mengine, walichokifanya wakaficha mafundisho ya mitume wao kwa thamani ndogo ya maisha ya dunia wakaenda kinyume na ahadi.

Aya imebainisha hao ni mayahudi na wakristo sisi mada yetu inamuhusu mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake, iweje maneno yao yawe hadithi na ilhali wao sio mitume? au ufahamu wako umeupeleka wapi mkuu?.

Lakini pia bado nasubiri uniletee ushahidi wa namna ya kuswali kwa mujibu wa quran pekee.

Karibu zonda
 
waislamu wanakwambia usitumie vya kafiri wakati hiyo simu na elimu ya kumtibu yeye imetoka huko.
hapo ndipo nilipowaona akili hakuna.
binadamu umepewa vyote duniani kuvitumia iweje usingizie mungu.
Acha kupotosha
Wapi wamesema haya maneno
Kama una chuki binafsi na waislam Sema ila usitunge uongo haukusaidii
 
Mbwa bado anaonekana ni kiumbe chenye msaada sana kwa binadamu. Kwa sasa Mbwa anatumia sana kwenye nchi ambazo zimepata majanga ya tetemeko Hivi karibuni yaani Syria na Uturuki.

Najiuliza nchi hizi ni za kiislamu vipi kuruhusu Mbwa atumike wakati kwa uislamu Mbwa ni najisi. Nauliza tu kupata uelewa siyo vita.
Aliyekwambia mbwa ni haramu nani
 
Mkuu hili jambo la kujifanya huelewi nilikutahadharisha mwanzo wa mjadala, hao watu wa kitabu walilazimishwa na hiyo ahadi kuwa watawafundisha watu taurati na injili wala wasifiche mengine na wakafundisha mengine, walichokifanya wakaficha mafundisho ya mitume wao kwa thamani ndogo ya maisha ya dunia wakaenda kinyume na ahadi.

Aya imebainisha hao ni mayahudi na wakristo sisi mada yetu inamuhusu mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake, iweje maneno yao yawe hadithi na ilhali wao sio mitume? au ufahamu wako umeupeleka wapi mkuu?.

Lakini pia bado nasubiri uniletee ushahidi wa namna ya kuswali kwa mujibu wa quran pekee.

Karibu zonda
QUR'AN 16:89,2:185 kwamba Qur'an 'inabainisha kila kitu'...na
 
Sawa.

"Na kumbuka pale allah alipochukua ahadi na wale waliopewa kitabu kuwa: naapa mtawabainishia watu na wala hamtokificha, basi walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwa kitabu hicho thamani ndogo{ya dunia} basi ni kiovu hicho walichokinunua.."
Qur'an 3:187

Sasa nifahamishe hizi habari za mayahudi na wakristo zinahusiana vipi na mada yetu.
Shida yako 'yubayyin'...Soma Tena 16:89,2:185
 
Huwa nina kawaida moja kama nikiona tunaanza kupoteza muda basi nakubali kushindwa mjadala, kwa mtindo huu unaokwenda nao tunaelekea huko.
QUR'AN 16:89,2:185 kwamba Qur'an 'inabainisha kila kitu'...na
 
Kama utauweza mjadala kwa hekma na maarifa na adabu na utii pasi na dharau na kejeli karibu.

Sisi tuna ahadi na allah subhaanah ya kuihifadhi dini yake na kuiepusha na kubadilishwa kama yalivyofanywa mafundisho yaliyotangulia kwa mitume wengine, na jambo la pili ni kuwa mapokeo yetu ya kiislamu yamelindwa na sanad huu ni mtiririko wa wapokezi na hapa kuna vigezo vigumu sana vimewekwa kuhakikisha habari iliyopokelewa ni sahihi, hassan, dhaifu au ya kutungwa.

Ukiyajua hayo sasa tutakuja kwenye malengo ya kuandikwa hadithi kwanini hazikuandikwa mwanzo zikaja kuandikwa baadae?.

Mwisho nikuulize wewe unaswali!? kama ndio umejuaje namna ya kuswali? wakati kwenye quran hakuna pahala pa muongozo wa namna ya kuswali?.

karibu.
Namshukuru Allah kwa neema ya Sunnah.
 
waislamu wanakwambia usitumie vya kafiri wakati hiyo simu na elimu ya kumtibu yeye imetoka huko.
hapo ndipo nilipowaona akili hakuna.
binadamu umepewa vyote duniani kuvitumia iweje usingizie mungu.
Leta andiko linalo sema hivyo.
 
Mbwa bado anaonekana ni kiumbe chenye msaada sana kwa binadamu. Kwa sasa Mbwa anatumia sana kwenye nchi ambazo zimepata majanga ya tetemeko Hivi karibuni yaani Syria na Uturuki.

Najiuliza nchi hizi ni za kiislamu vipi kuruhusu Mbwa atumike wakati kwa uislamu Mbwa ni najisi. Nauliza tu kupata uelewa siyo vita.
Mbwa aliyrpewa mafunzo,kama uindaji na kazi ya uokoaji na mafunzo mengine yenye faida,anaruhusiwa.
 
waislamu wanakwambia usitumie vya kafiri wakati hiyo simu na elimu ya kumtibu yeye imetoka huko.
hapo ndipo nilipowaona akili hakuna.
binadamu umepewa vyote duniani kuvitumia iweje usingizie mungu.
Nani alikwambia kuwa waislamu wameambiwa wasitumie vya kafiri? Hiyo ni generalised statement. Enzi za Mtume walikuweko manasara (christians) na mayahudi (jews) na walikuwa wakifanya biashara hapo Makka, sasa ingekuwa hivyo unavyosema ni sahihi si angesema wasiende kwa hao wafanya biashara kununua vitu?

Kuna vitu maalumu ndiyo vimekatazwa (na hata kuiga) siyo vyote.
 
Back
Top Bottom