Kuuawa kwa majenerali wa Urusi na vita kuchukua muda mrefu ni ishara kuwa jeshi hilo halina uwezo unaosemwa

Kuuawa kwa majenerali wa Urusi na vita kuchukua muda mrefu ni ishara kuwa jeshi hilo halina uwezo unaosemwa

Huyu Raisi wa Ukraine anaendesha vita kikomrdy. Anamdunda mtu halafu anapiga kelele yeye kuwa anapigwa.ni sawa na mwanamke anamdunda mumewe lakini kelele anapiga yeye ananiuaa
 
USA Hana visima vya mafuta Syria
Haya ukimakiliza kusoma nenda kampige makonzi Putin kwa kukudanganya kuwa aliyatimua majeshi yote ya Marekani Syria.
Screenshot_20220323-154814.jpg
Screenshot_20220323-154824.jpg
Screenshot_20220323-154842.jpg
 
Teh teh teh sisi tunaongelea Marekani kuthibiti visima vya mafuta vya Syria wewe unaongelea makampuni ya mafuta yaliyokuwa yanafanya biashara ya uchimbaji wa mafuta Syria.
Sasa kadhibitije wakati biashara inaendelea Kufanyika na serikali inamiliki 50%na zingine kampuni za China na India biashara inaendelea kufanyika bila shida yoyote.
 
Hawamiliki hata kidogo na serikali inaendelea kuuza mafuta huku makampuni ya mabeberu yakiondoka yamebaki ya China na India.biashara inaendelea huku serikali inamiliki 50%
Kwani hoja yako ilikuwa makampuni ya mafuta ya Mabeberu kuwepo Syria au Jeshi la Marekani kumiliki visima vya mafuta vilivyopo Mashariki mwa Syria?
 
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba Russia ilipanga kuwa imeiteka ikulu ya Kiev ndani ya siku mbili, wapachike vibaraka wao madarakani kisha warudi nyumbani. Lakini sasa hali imekuwa tofauti kama ambavyo ulimwengu umekuwa ukiitizama nguvu ya kijeshi ya Russia.

Hadi sasa majenerali 5 wa Russia wameuawa, kuuawa kwa Jenerali wa vita ni jambo la nadra sana kwani wao ni viongozi wakuu wa vita na mara nyingi wao ukaa eneo salama huku wakitoa maelekezo, mfano mara ya mwisho kwa Marekani kupoteza kiongozi wa juu kwenye uwanja wa mapambano ilikuwa ni vita dhidi ya Vietnam mwaka 1970. Lakini hii kwa Russia imekuwa tofauti, kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya kivita, inaonekana hali ya upambanaji ya wanajeshi wa Russia iko chini sana kiasi kwamba inalazimika kiongozi mkuu aende uwanja wa mapigano (frontline) kutoa maelekezo na kuamsha molari ya vijana wao.

Kitendo cha Majenerali hao kwenda frontline kimasababisha kuuawa kwao. Majenelari waliouawa mpaka sasa ni Andrei Sukhovetsky, Vitaly Gerasimov, Andrey Kolesnikov, Denis Glebov, Konstantin Zizevsky.

Kwa mujibu wa taarifa kitoka vyanzo mbalimbali, hizi ndizo sababu za Russia kutopiga hatua haraka ili kuiteka Kiev

1. Makadirio ya dharau kwa jeshi la Ukraine. Iko wazi kuwa serikali ya Russia uwekeza kwenye jeshi zaidi kuliko maendeleo ya watu, uwekezaji huu umeifanya Russia iingine vitani kwa kijiamini mno na kushindwa kujua uhalisia juu ya nguvu ya Kijeshi ya mpinzani wake. Ikumbukwe kuwa Ukraine ni nchi ya 12 duniani kwa kuuza vifaa vya kivita nje. Lakini ikumbukwe kuwa wakati Ukraine ikiwa sehemu ya Muungano wa kijamaa wa Kisovieti (Soviet Union), ilikuwa ikichangia uzalishaji wa silaha katika muungano huo kwa asilimia 30, lakini pia asilimia 40 ya utafiti wa kisayansi wa silaha ulifanyika Ukraine. Hivyo lilikuwa ni kosa kubwa kwa Russia kuwachukulia poa

Sababu ya pili ya Russia kushindwa kusonga mbele kwenye vita hii ni Rais Putin na wenzie kuwadanganya wanajeshi pamoja wananchi. Mpaka majeshi ya Russia yanaanza mashambulizi hawakujua hasa wanapigania nini, wao waliambiwa mnakwenda Ukraine kwa ajili ya kulinda amani, lakini kadri siku zilivyosonga walishangaa vita ikipamba moto na wanajeshi wengi kupoteza maisha. Kwa mujibu wa wanajeshi wa Russia waliosalim amri, walinukuliwa wakisema "Tuliambiwa tunakwenda Ukraine kulinda amani, tumefika huku tunaona kila mtu anakufa, imebadilika na kuwa vita kubwa"

Sababu ya tatu ni kuwa, kwa sababu ya kuikosea mahesabu Ukraine, mfumo wa Logistics wa jeshi la Russia ni mbovu. Wanajeshi wamejikuta hawapati huduma kwa wakati, ikiwepo kuletewa mafuta, chakula, maji nk hasa baada ya kukwama kwenye foleni iliyosababishwa na mashambulizi ya Ukraine. Kuna baadhi ya video zimesambaa zikionesha wanajeshi wa Russia wakiiba chakula Supermarket, jambo ambalo ni aibu.

Uwezo mdogo wa kupigana vita vya mtaani. Itakumbukwa kuwa Putin aliomba wanajeshi wa Syria wajitolee kuwasaidia, hii ni baada ya wanajeshi wa Russia kuwa na uwezo mdogo wa vita vya mtaa kwa mtaa, badala ya kupigana mtaani badala yake wamekuwa wakibomoa majengo ya raia kwa makombola ya kutoka mbali.

Sababu ya mwisho. Russia imeshindwa kulitawala anga la Ukraine kwa ndege za kivita, kuna idadi kubwa ya ndege za Russia zimedunguliwa kwa silaha za kubeba mkononi (Stinger missiles au MANPAD) kila zikiingia anga la Ukraine. Kuna duru zinasema nchi za NATO zilipenyeza vifaa vya kisasa vya kudungua ndege za kivita pamoja na vifaru. Hii imesababisha Russia kurusha makombora ambayo hayaendi kushambulia maeneo ya jeshi bali majengo ya wananchi

Mpaka sasa hakuna mji hata mmoja ambao Russia imejiahakikishia kuuteka kwa asilimia mia moja, kuna mji kama Mariupol na Kharkiv ambayo kwa muda wa wiki tatu sasa imekuwa kwa kiasi kikubwa chini ya Russia lakini bado wanapata upinzani kwa njia ya kuviziwa.

Ikumbukwe kuwa Russia ilishindwa vita na Chechnya mwaka 1996 hadi pale ambapo ilibidi wakae chini na kuweka maridhiano, Russia ilipoteza wanajeshi 5,700. Kwa mtizamo wangu, sioni hii vita kama itakwisha kirahisi kama ambavyo wengi walidhania, hii itakuwa vita ya aina yake kwani sababu zake haziko wazi, lakini pia namna ambavyo Russia wanatumia muda mrefu ndivyo ambavyo wanaruhusu NATO kupenyeza silaha, lakini pia kupeleka wanajeshi wazoefu kuisaidia Ukraine huku wakijifanya ni raia wasio na uzoefu bali wanaenda kujitolea. Wakati huohuo mbinyo wa kiuchumi ukiendelea kuwatafuna raia wa kawaida wa Russia.

NB: Kuvamia nchi hata kama ina uwezo mdogo wa kijeshi ni kazi ngumu kuliko kulinda nchi, kwani uwavamiao wako kwao na wanazijua chocho zote. Nina uhakika baada ya vita hii dunia itakuwa salama, hatutashuhudia tena nchi ikivamia nchi nyingine, najua Putin tayari anajuta na atakoma kama ambavyo USA amekoma kwa Iraq na Afghanistan.

Uchambuzi huu umetolewa na ndugu yenu Nkobe baada ya kusoma makala mbalimbali juu ya mwenendo wa vita hii
Bwana Utam
Paula Paul
Mwamaleki
STRUGGLE MAN
 
Yeye mrusi mwenyewe anataka muamini kuwa hana silaha za maana zaid ya nuclear. Unapo mu underestimate adui tayari umejijengea mazingira ya kushindwa.

Anyways juzi kati alijaribu ile hypersonic apo Ukraine, first time to be used in war.

Then inaonekana sasa amebadilisha mbinu, anakutaka mashariki na kusini afike kwa Moldova wajaribiane kwa ajili ya Transgender region ( 😀 )
 
Yeye mrusi mwenyewe anataka muamini kuwa hana silaha za maana zaid ya nuclear. Unapo mu underestimate adui tayari umejijengea mazingira ya kushindwa.

Anyways juzi kati alijaribu ile hypersonic apo Ukraine, first time to be used in war.

Then inaonekana sasa amebadilisha mbinu, anakutaka mashariki na kusini afike kwa Moldova wajaribiane kwa ajili ya Transgender region ( 😀 )
 
Yeye mrusi mwenyewe anataka muamini kuwa hana silaha za maana zaid ya nuclear. Unapo mu underestimate adui tayari umejijengea mazingira ya kushindwa.

Anyways juzi kati alijaribu ile hypersonic apo Ukraine, first time to be used in war.

Then inaonekana sasa amebadilisha mbinu, anakutaka mashariki na kusini afike kwa Moldova wajaribiane kwa ajili ya Transgender region ( 😀 )
Naona ume jijibu mkuu yote ulio yaandika ndio makosa ya Russia kwa Ukraine.
 
Mrusi hataki.kumaliza vita ni faida yake kwanza anaziteka Sila za western na zingine anaziripua. Hao mageneral wanasema wamekufa mbona hawajatuonyesha. Hata waziri wa majeshi walisema kafa wengine wakisema kafukuzwa na Putin mara tunamuona hai na yuko meza Moja na Putin
 
inaonekana hali ya upambanaji ya wanajeshi wa Russia iko chini sana kiasi kwamba inalazimika kiongozi mkuu aende uwanja wa mapigano (frontline) kutoa maelekezo na kuamsha molari ya vijana wao.
wataalam wengine wa kivita wanaainisha kuwa Urusi hutumia mfumo wa "single line extended" mfumo ambao hutoa fursa ya kupata hasara kubwa pale ambapo adui atapiga kwenye target
 
Nkobe
Mkuu uliona mbali sana.Mpaka leo Russia inasumbuka sana na hivi vita.Wanajeshi wake wengi (zaidi elfu 54) wamepoteza maisha,majeruhi kibao,vifaa vyao vingi vya kijeshi vimetekwa na kuharibiwa.
Putin ni sikio la kufa.......🤔
 
Halafu kuna watu utawasikia eti Urusi hatumii jeshi huko Ukraine anatumia wafungwa tu,sasa hao majenerali wanatoka wapi?!

Jamaa aliingiza jeshi wakafyekwa akajazia mamluki wa Wagner nao wakafyekwa,sasa anajazia wengine laki3.
 
Back
Top Bottom