ielewemitaa
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 10,764
- 9,477
Week 3yom kippur war mlichukua muda gani pale mashariki ya kati
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Week 3yom kippur war mlichukua muda gani pale mashariki ya kati
siku sita tu ilitosha kuwasambaratisha arab coalition na urusi wenu wa buzaWeek 3
Acha uhuni kijana ni zaidi ya mwezi ile vita ilichukuaIraq ilichukua siku 4 kuimtoa Sadam madarakani
Una zungumzia vita gani maana Israel alipigana vita nyingi, hiyo mwaka 1967 Misri hakuwa na Ant Aircraft system wala Ant tank missile , ndio maana Israel alitumia ndege tu kupiga majeshi ya waarabu, ila mwaka 1973 baada ya Urusi kuwapa Misri Ant aircraft system na ant tank missile(SAGA), waulize wayahudi walichokutana nachosiku sita tu ilitosha kuwasambaratisha arab coalition na urusi wenu wa buza
kafuatilie vizur yom kippur war misri alichaipika sana pamoja mrusi wako wa buza maan unajichanganya tu hapaUna zungumzia vita gani maana Israel alipigana vita nyingi, hiyo mwaka 1967 Misri hakuwa na Ant Aircraft system wala Ant tank missile , ndio maana Israel alitumia ndege tu kupiga majeshi ya waarabu, ila mwaka 1973 baada ya Urusi kuwapa Misri Ant aircraft system na ant tank missile(SAGA), waulize wayahudi walichokutana nacho
6 day war ile vita ni mwaka 1967 ile ni six day war sio yom kippur war ebu kasome tena, ile ya mwaka 1973 ndio yom kippur war ambapo vita ilipiganwa zaidi ya week 2 mpaka 3 , ambapo huku Egypty wanaita ramadan war kule Israel yom kippur war , jifunze tenakafuatilie vizuri 6 day war ( yom kippur war) nimemaliza
Russia ndio dawa ya chawaRussia ni matapeli mno
hizo zote arab coalition ilishinda?6 day war ile vita ni mwaka 1967 ile ni six day war sio yom kippur war ebu kasome tena, ile ya mwaka 1973 ndio yom kippur war ambapo vita ilipiganwa zaidi ya week 2 mpaka 3 , ambapo huku Egypty wanaita ramadan war kule Israel yom kippur war , jifunze tena
1. 1967 ni six day war
2.1973 ni yom kippur war( Israel)or ramadan war( Egypty)
1. 1967 Israel alifanikiwa kuchukua Golan height (syria) na jangwa la Sinai kule Misrihizo zote arab coalition ilishinda?
Kama Taliban wangepewa Ant Aircraft system kama Ukraine unafikiri ndege za US zingeruka hewani zinavyotaka? Acha masikhara Ukraine amepewa msaada wa kiwango cha juu kabisaa
Kaka unazingua weledi bila vifaa ni uongo mtupu, mwenzako yuko hewani anapiga tu wakati wewe huwezi kumfikia hapa lazima uumie, ndio maana Ant aircraft system ni LAZIMA sio ombi, kama angepewa Taliban hii vita ya ardhin US angekimbia mapema tu kwa wale watalibanSoldiers win battles logistics win the war.
unaweza kuwa na hiyo ant aircraft ila huna askari wenye weredi.
kumbuka jeshi la Ukraine limesukwa hivi karibuni baada ya kuona kila putin akiota ndoto ya kuirudisha imaya ya Soviet anaenda Ukraine ana mega ardhi then atakaa baada ya muda ndoto ikijirudia anarudi tena chukua kipande kingine. aendi Poland ama kwingineko, yeye ni Ukraine tu kwasababu anajua Ukraine ni defenseless country.
Jeshi la Ukraine bado changa ndiyo maana nchi zinajitolea kuwapa ndege za Urusi ambazo wanauzoefu nazo.
na zaidi uking'ang'ania madai ya kuwa msaada ndiyo unawabeba Ukraine automatically unakuwa unakubali kwamba west inguvu kushinda Urusi. ikiwa msaada wake tu kwa Ukraine unaiyumbisha urusi vipi wao wakiingia kupigana full war na Urusi, Urusi itabaki kweli?.
yaan kwenye kipindi iki cha misaada Urusi ili paswa kutoa somo kuwa Nato kuwa yenyewe ni dedili zaidi ya misaada yao ( in dj afro voice) 😊😊
Huyu hapa Zelensky leo hii:Russia ni matapeli mno
Kufa kawaida vitani msikilize comedian amechoka huyu hapa:Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba Russia ilipanga kuwa imeiteka ikulu ya Kiev ndani ya siku mbili, wapachike vibaraka wao madarakani kisha warudi nyumbani. Lakini sasa hali imekuwa tofauti kama ambavyo ulimwengu umekuwa ukiitizama nguvu ya kijeshi ya Russia.
Hadi sasa majenerali 5 wa Russia wameuawa, kuuawa kwa Jenerali wa vita ni jambo la nadra sana kwani wao ni viongozi wakuu wa vita na mara nyingi wao ukaa eneo salama huku wakitoa maelekezo, mfano mara ya mwisho kwa Marekani kupoteza kiongozi wa juu kwenye uwanja wa mapambano ilikuwa ni vita dhidi ya Vietnam mwaka 1970. Lakini hii kwa Russia imekuwa tofauti, kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya kivita, inaonekana hali ya upambanaji ya wanajeshi wa Russia iko chini sana kiasi kwamba inalazimika kiongozi mkuu aende uwanja wa mapigano (frontline) kutoa maelekezo na kuamsha molari ya vijana wao.
Kitendo cha Majenerali hao kwenda frontline kimasababisha kuuawa kwao. Majenelari waliouawa mpaka sasa ni Andrei Sukhovetsky, Vitaly Gerasimov, Andrey Kolesnikov, Denis Glebov, Konstantin Zizevsky.
Kwa mujibu wa taarifa kitoka vyanzo mbalimbali, hizi ndizo sababu za Russia kutopiga hatua haraka ili kuiteka Kiev
1. Makadirio ya dharau kwa jeshi la Ukraine. Iko wazi kuwa serikali ya Russia uwekeza kwenye jeshi zaidi kuliko maendeleo ya watu, uwekezaji huu umeifanya Russia iingine vitani kwa kijiamini mno na kushindwa kujua uhalisia juu ya nguvu ya Kijeshi ya mpinzani wake. Ikumbukwe kuwa Ukraine ni nchi ya 12 duniani kwa kuuza vifaa vya kivita nje. Lakini ikumbukwe kuwa wakati Ukraine ikiwa sehemu ya Muungano wa kijamaa wa Kisovieti (Soviet Union), ilikuwa ikichangia uzalishaji wa silaha katika muungano huo kwa asilimia 30, lakini pia asilimia 40 ya utafiti wa kisayansi wa silaha ulifanyika Ukraine. Hivyo lilikuwa ni kosa kubwa kwa Russia kuwachukulia poa
Sababu ya pili ya Russia kushindwa kusonga mbele kwenye vita hii ni Rais Putin na wenzie kuwadanganya wanajeshi pamoja wananchi. Mpaka majeshi ya Russia yanaanza mashambulizi hawakujua hasa wanapigania nini, wao waliambiwa mnakwenda Ukraine kwa ajili ya kulinda amani, lakini kadri siku zilivyosonga walishangaa vita ikipamba moto na wanajeshi wengi kupoteza maisha. Kwa mujibu wa wanajeshi wa Russia waliosalim amri, walinukuliwa wakisema "Tuliambiwa tunakwenda Ukraine kulinda amani, tumefika huku tunaona kila mtu anakufa, imebadilika na kuwa vita kubwa"
Sababu ya tatu ni kuwa, kwa sababu ya kuikosea mahesabu Ukraine, mfumo wa Logistics wa jeshi la Russia ni mbovu. Wanajeshi wamejikuta hawapati huduma kwa wakati, ikiwepo kuletewa mafuta, chakula, maji nk hasa baada ya kukwama kwenye foleni iliyosababishwa na mashambulizi ya Ukraine. Kuna baadhi ya video zimesambaa zikionesha wanajeshi wa Russia wakiiba chakula Supermarket, jambo ambalo ni aibu.
Uwezo mdogo wa kupigana vita vya mtaani. Itakumbukwa kuwa Putin aliomba wanajeshi wa Syria wajitolee kuwasaidia, hii ni baada ya wanajeshi wa Russia kuwa na uwezo mdogo wa vita vya mtaa kwa mtaa, badala ya kupigana mtaani badala yake wamekuwa wakibomoa majengo ya raia kwa makombola ya kutoka mbali.
Sababu ya mwisho. Russia imeshindwa kulitawala anga la Ukraine kwa ndege za kivita, kuna idadi kubwa ya ndege za Russia zimedunguliwa kwa silaha za kubeba mkononi (Stinger missiles au MANPAD) kila zikiingia anga la Ukraine. Kuna duru zinasema nchi za NATO zilipenyeza vifaa vya kisasa vya kudungua ndege za kivita pamoja na vifaru. Hii imesababisha Russia kurusha makombora ambayo hayaendi kushambulia maeneo ya jeshi bali majengo ya wananchi
Mpaka sasa hakuna mji hata mmoja ambao Russia imejiahakikishia kuuteka kwa asilimia mia moja, kuna mji kama Mariupol na Kharkiv ambayo kwa muda wa wiki tatu sasa imekuwa kwa kiasi kikubwa chini ya Russia lakini bado wanapata upinzani kwa njia ya kuviziwa.
Ikumbukwe kuwa Russia ilishindwa vita na Chechnya mwaka 1996 hadi pale ambapo ilibidi wakae chini na kuweka maridhiano, Russia ilipoteza wanajeshi 5,700. Kwa mtizamo wangu, sioni hii vita kama itakwisha kirahisi kama ambavyo wengi walidhania, hii itakuwa vita ya aina yake kwani sababu zake haziko wazi, lakini pia namna ambavyo Russia wanatumia muda mrefu ndivyo ambavyo wanaruhusu NATO kupenyeza silaha, lakini pia kupeleka wanajeshi wazoefu kuisaidia Ukraine huku wakijifanya ni raia wasio na uzoefu bali wanaenda kujitolea. Wakati huohuo mbinyo wa kiuchumi ukiendelea kuwatafuna raia wa kawaida wa Russia.
NB: Kuvamia nchi hata kama ina uwezo mdogo wa kijeshi ni kazi ngumu kuliko kulinda nchi, kwani uwavamiao wako kwao na wanazijua chocho zote. Nina uhakika baada ya vita hii dunia itakuwa salama, hatutashuhudia tena nchi ikivamia nchi nyingine, najua Putin tayari anajuta na atakoma kama ambavyo USA amekoma kwa Iraq na Afghanistan.
Uchambuzi huu umetolewa na ndugu yenu Nkobe baada ya kusoma makala mbalimbali juu ya mwenendo wa vita hii
Nonsense!...kawadanganye wanao huo utotoKwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba Russia ilipanga kuwa imeiteka ikulu ya Kiev ndani ya siku mbili, wapachike vibaraka wao madarakani kisha warudi nyumbani. Lakini sasa hali imekuwa tofauti kama ambavyo ulimwengu umekuwa ukiitizama nguvu ya kijeshi ya Russia.

Subiria mitusi ya warusi wa bonyokwa 😀😀😀Urusi anapigwa hata na Rwanda tu!
Sababu ingine ni kuwa baada ya ukomunisti Urusi kuanguka na kuingia ubepari rushwa na upendeleo uliingia Serikali ya Russia ajira zikawa za upendeleo na Rushwa.Wengi walioajiriwa jeshini ni watoto wa makada wa chama tawala na viongozi wa zamani wa Majeshi ya Urusi na watoto wa viongozi waandamizi wa Serikali,bunge mahakama na ndugu zao.Wengine waliopenya ajira ni kupitia rushwaUrusi ina historia ya kutoa kafara askari wake katika vita zote wanazopigana.
chini ya wiki 1 Nato ilikuwa tayali imeitiisha Kabul na walipoteza Askari kama 10 tu.
na kwa miaka yote 20 ya kuikalia Afghanistan wamepotezea askari kama 2 elfu.
Wakati Urus kwa miaka 9 ya kuikalia Afghanistan alipoteza zaid 15 elfu askari.
sijui wanashida gani ndani ya jeshi lao!!.