Kuuawa kwa majenerali wa Urusi na vita kuchukua muda mrefu ni ishara kuwa jeshi hilo halina uwezo unaosemwa

Kuuawa kwa majenerali wa Urusi na vita kuchukua muda mrefu ni ishara kuwa jeshi hilo halina uwezo unaosemwa

Jibu swali..ni vita gani ya Kuiteka nchi nyingine USA ilichukua Muda mfupi zaidi na ikashinda kikamilifu?
Screenshot_20220321-205652.jpg
 
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ni kwamba Russia ilipanga kuwa imeiteka ikulu ya Kiev ndani ya siku mbili, wapachike vibaraka wao madarakani kisha warudi nyumbani. Lakini sasa hali imekuwa tofauti kama ambavyo ulimwengu umekuwa ukiitizama nguvu ya kijeshi ya Russia.

Hadi sasa majenerali 5 wa Russia wameuawa, kuuawa kwa Jenerali wa vita ni jambo la nadra sana kwani wao ni viongozi wakuu wa vita na mara nyingi wao ukaa eneo salama huku wakitoa maelekezo, mfano mara ya mwisho kwa Marekani kupoteza kiongozi wa juu kwenye uwanja wa mapambano ilikuwa ni vita dhidi ya Vietnam mwaka 1970. Lakini hii kwa Russia imekuwa tofauti, kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya kivita, inaonekana hali ya upambanaji ya wanajeshi wa Russia iko chini sana kiasi kwamba inalazimika kiongozi mkuu aende uwanja wa mapigano (frontline) kutoa maelekezo na kuamsha molari ya vijana wao.

Kitendo cha Majenerali hao kwenda frontline kimasababisha kuuawa kwao. Majenelari waliouawa mpaka sasa ni Andrei Sukhovetsky, Vitaly Gerasimov, Andrey Kolesnikov, Denis Glebov, Konstantin Zizevsky.

Kwa mujibu wa taarifa kitoka vyanzo mbalimbali, hizi ndizo sababu za Russia kutopiga hatua haraka ili kuiteka Kiev

1. Makadirio ya dharau kwa jeshi la Ukraine. Iko wazi kuwa serikali ya Russia uwekeza kwenye jeshi zaidi kuliko maendeleo ya watu, uwekezaji huu umeifanya Russia iingine vitani kwa kijiamini mno na kushindwa kujua uhalisia juu ya nguvu ya Kijeshi ya mpinzani wake. Ikumbukwe kuwa Ukraine ni nchi ya 12 duniani kwa kuuza vifaa vya kivita nje. Lakini ikumbukwe kuwa wakati Ukraine ikiwa sehemu ya Muungano wa kijamaa wa Kisovieti (Soviet Union), ilikuwa ikichangia uzalishaji wa silaha katika muungano huo kwa asilimia 30, lakini pia asilimia 40 ya utafiti wa kisayansi wa silaha ulifanyika Ukraine. Hivyo lilikuwa ni kosa kubwa kwa Russia kuwachukulia poa

Sababu ya pili ya Russia kushindwa kusonga mbele kwenye vita hii ni Rais Putin na wenzie kuwadanganya wanajeshi pamoja wananchi. Mpaka majeshi ya Russia yanaanza mashambulizi hawakujua hasa wanapigania nini, wao waliambiwa mnakwenda Ukraine kwa ajili ya kulinda amani, lakini kadri siku zilivyosonga walishangaa vita ikipamba moto na wanajeshi wengi kupoteza maisha. Kwa mujibu wa wanajeshi wa Russia waliosalim amri, walinukuliwa wakisema "Tuliambiwa tunakwenda Ukraine kulinda amani, tumefika huku tunaona kila mtu anakufa, imebadilika na kuwa vita kubwa"

Sababu ya tatu ni kuwa, kwa sababu ya kuikosea mahesabu Ukraine, mfumo wa Logistics wa jeshi la Russia ni mbovu. Wanajeshi wamejikuta hawapati huduma kwa wakati, ikiwepo kuletewa mafuta, chakula, maji nk hasa baada ya kukwama kwenye foleni iliyosababishwa na mashambulizi ya Ukraine. Kuna baadhi ya video zimesambaa zikionesha wanajeshi wa Russia wakiiba chakula Supermarket, jambo ambalo ni aibu.

Uwezo mdogo wa kupigana vita vya mtaani. Itakumbukwa kuwa Putin aliomba wanajeshi wa Syria wajitolee kuwasaidia, hii ni baada ya wanajeshi wa Russia kuwa na uwezo mdogo wa vita vya mtaa kwa mtaa, badala ya kupigana mtaani badala yake wamekuwa wakibomoa majengo ya raia kwa makombola ya kutoka mbali.

Sababu ya mwisho. Russia imeshindwa kulitawala anga la Ukraine kwa ndege za kivita, kuna idadi kubwa ya ndege za Russia zimedunguliwa kwa silaha za kubeba mkononi (Stinger missiles au MANPAD) kila zikiingia anga la Ukraine. Kuna duru zinasema nchi za NATO zilipenyeza vifaa vya kisasa vya kudungua ndege za kivita pamoja na vifaru. Hii imesababisha Russia kurusha makombora ambayo hayaendi kushambulia maeneo ya jeshi bali majengo ya wananchi

Mpaka sasa hakuna mji hata mmoja ambao Russia imejiahakikishia kuuteka kwa asilimia mia moja, kuna mji kama Mariupol na Kharkiv ambayo kwa muda wa wiki tatu sasa imekuwa kwa kiasi kikubwa chini ya Russia lakini bado wanapata upinzani kwa njia ya kuviziwa.

Ikumbukwe kuwa Russia ilishindwa vita na Chechnya mwaka 1996 hadi pale ambapo ilibidi wakae chini na kuweka maridhiano, Russia ilipoteza wanajeshi 5,700. Kwa mtizamo wangu, sioni hii vita kama itakwisha kirahisi kama ambavyo wengi walidhania, hii itakuwa vita ya aina yake kwani sababu zake haziko wazi, lakini pia namna ambavyo Russia wanatumia muda mrefu ndivyo ambavyo wanaruhusu NATO kupenyeza silaha, lakini pia kupeleka wanajeshi wazoefu kuisaidia Ukraine huku wakijifanya ni raia wasio na uzoefu bali wanaenda kujitolea. Wakati huohuo mbinyo wa kiuchumi ukiendelea kuwatafuna raia wa kawaida wa Russia.

NB: Kuvamia nchi hata kama ina uwezo mdogo wa kijeshi ni kazi ngumu kuliko kulinda nchi, kwani uwavamiao wako kwao na wanazijua chocho zote. Nina uhakika baada ya vita hii dunia itakuwa salama, hatutashuhudia tena nchi ikivamia nchi nyingine, najua Putin tayari anajuta na atakoma kama ambavyo USA amekoma kwa Iraq na Afghanistan.

Uchambuzi huu umetolewa na ndugu yenu Nkobe baada ya kusoma makala mbalimbali juu ya mwenendo wa vita hii
Kwa vikwazo alivyowekewa lazima hali yake iwe ngumu
 
Una zungumzia vita gani maana Israel alipigana vita nyingi, hiyo mwaka 1967 Misri hakuwa na Ant Aircraft system wala Ant tank missile , ndio maana Israel alitumia ndege tu kupiga majeshi ya waarabu, ila mwaka 1973 baada ya Urusi kuwapa Misri Ant aircraft system na ant tank missile(SAGA), waulize wayahudi walichokutana nacho
Wewe kweli mwehu,eti Nchi fulani haikuwa na hiki na kile,vita ni vita hata ukitumia mawe huo ndio uwezo wa silaha ulizonazo.
 
Wewe kweli mwehu,eti Nchi fulani haikuwa na hiki na kile,vita ni vita hata ukitumia mawe huo ndio uwezo wa silaha ulizonazo.
Wewe ndio mwehu asa unafikiri vile vifaa vya kijeshi vinavyo miminika kule Ukraine ni kwa ajili ya show off? vita bila vifaa vya kisasa huwezi toboa, ndio maana watu wa magharibi kila siku wanapeleka vifaa Ukraine
 
Sasa unataka kumlaumu nani,kama NATO inatuma vifaa na Urusi anachapika je ndio NATO waingie full mkoko itakuwaje? Ndani ya wiki watakuwa Kremlin.
 
By the way vipi Putin si alisema yeyote atakaemsaidia Ukraine atakipata cha moto na pia atalipua misaada ya silaha zinazongia imekuwaje hahafanya lolote hadi sasa au ndio ule Uchui wa Karatasi?
 
Sasa unataka kumlaumu nani,kama NATO inatuma vifaa na Urusi anachapika je ndio NATO waingie full mkoko itakuwaje? Ndani ya wiki watakuwa Kremlin.
Kwani NATO wamekatazwa wasiingie? kama ubavu wanao waje uwanjani, hakuna wanachoweza zaidi ya kutoa silaha tu na misaada ya kibanadamu, wanaogopa Ulaya itakuwa uwanja wa vita
 
By the way vipi Putin si alisema yeyote atakaemsaidia Ukraine atakipata cha moto na pia atalipua misaada ya silaha zinazongia imekuwaje hahafanya lolote hadi sasa au ndio ule Uchui wa Karatasi?
Msaada gani alisema ? yeye anapiga Ukraine anavyotaka kama unavyoona anapiga wazee, kina mama , watoto sasa hao NATO kama wana nguvu waje kumzuia, Zelensky anawaambia NATO waweke no flyzone mbona wana ruka ruka kama maharage? hiyo ndio red line yetu Warusi
 
Baghdad ilitekwa ndani ya wiki 3 tuu.
Mbona maelezo yako wazi wapi hujaelewa?
he 2003 invasion of Iraq[a] was the first stage of the Iraq War. The invasion phase began on 19 March 2003 (air) and 20 March 2003 (ground) and lasted just over one month,[24] including 26 days of major combat operations, in which a combined force of troops from the United States,
 
Nafikiri pia kwa Ukraine Kuua hao magenerali Ukraine kuna meseji wanatumia Putin

Sababu nchi ikiwa vitani kiongozi mkuu wa vita anakuwa Raisi Amiri Jeshi mkuu chini yake wanamfuata kivyeo vitani ni magenerali wa vita walioko msitari wa mbele

Kuua magenerali waongoza vita Ukraine ,Nchi ya Ukraine wanamtumia meseji kuwa tumeuwa magenerali wa vita walioko vitani next target Ni wewe Putin mpiga domo Kremlin

Maana ukiua Generali la Vita Putin atakuwa anaishi kwa kujificha kama nguchiro kuwa kama wameua magenerali wapiganaji wazoefu waongoza vita mimi ni nani

Meseji sent
 
Wameona Ukraine anatoshana nguvu na Russia ndio maana wamemuacha aimbe nae.
Wameona huku wanalia lia wao mpaka wanalazimisha wanamichezo wa Russia wakemee vita, kila eneo la mashariki wanapeleka Air defence system ahahhha
 
Nafikiri pia kwa Ukraine Kuua hao magenerali Ukraine kuna meseji wanatumia Putin

Sababu nchi ikiwa vitani kiongozi mkuu wa vita anakuwa Raisi Amiri Jeshi mkuu chini yake wanamfuata kivyeo vitani ni magenerali wa vita walioko msitari wa mbele

Kuua magenerali waongoza vita Ukraine ,Nchi ya Ukraine wanamtumia meseji kuwa tumeuwa magenerali wa vita walioko vitani next target Ni wewe Putin mpiga domo Kremlin

Maana ukiua Generali la Vita Putin atakuwa anaishi kwa kujificha kama nguchiro kuwa kama wameua magenerali wapiganaji wazoefu waongoza vita mimi ni nani

Meseji sent
Yaan Russia hata sisimizi hajaguswa mbona mnapenda kujidanganya, uwanja wa vita ni Ukraine, nakukumbusha juzi tu hapa Putin kahutubia halaiki ya watu hadharani sasa hiyo meseji sijui unampa Putin yupi
 
Back
Top Bottom