Kuuawa kwa Prigozhin na Imani ya Afrika kwa Putin na Washiriki Wake

Nimesoma mada zako kadhaa kuhusu mgogoro huu pamoja na Putin na nilihitimisha kwamba una chuki binafsi na Putin pamoja na Russia.

Ulichoandika leo kwa hakika hakina uhalisia na ashakum si matusi, haya ni maneno ya kwenye kahawa na watakaokubaliana nawe sio wafuatiliaji.

Swali moja tu kwako, umethibitisha vipi kuwa ndege hiyo ilitunguliwa kwa amri kutoka Moscow?
 


Hata sisi tuna facts' kama una chuki na Putin mtafute mrekebishe tofauti zenu, kuna vitu umepotosha hapo.
 
Unaweza nitajia mwanasiasa yeyote unayedhani ni mkweli na mimi nitakwambia uongo wake aliowahi kuusema hadharani.
Haya tupe uongo aliousema hadharani bwana JFK (Join Forces with the Kings)
 
Kwel kabisa,hakunaga mwanasiasa mkweli
 
Putin amefanya vibaya sana kumuua mwenzake.Yule hata ukimuangalia usoni anatisha.Ni swala la muda Putin atakuja kufa kifo kibaya na watakaomuua hawatatoka mbali.Kumuondoa mwenzake sio kupunguza maadui bali anaongeza maadui kumbuka Prighozin alikuwa na watu wanaomtii na kumpenda.Ni swala la muda tu.
 
Inasemekana hiyo Wagner mmoja wa waanzilishi wake ni Putin, hivyo haikuwa mali ya Prigozhin kwa asilimia zote.

Putin hasamehi kamwe wasaliti, hivyo kwa kilichompata Prigozhin kilitarajiwa.... hatimaye Wagner imemezwa na wizara ya ulinzi ya Urusi.
 
Kwenye Geopolitics hatuangalii yupi adui na yupi rafiki, au yupi mwema au yupi muovu.

Kwenye Geopolitics tunaangalia yupi "Maslahi" yake yanaendana au hayapingani na yetu bila kujali internal politics au foreign policies zake as long as hazina mahusiano yoyote au hazipingani na maslahi yetu

Russia ni key geopolitical player kwenye uasisi na mafanikio ya BRICS,
BRICS ni jina mwamvuli kwa nchi zote ambazo "maslahi" yao hayaendani na Western economic system pamoja na capitalistic & neo colonial institutions zake zote kama Petro dollar system, IMF, World Bank etc.

Russia kama ilivyo Africa, China, India na nchi nyingi zinazotaka kuwa sehemu ya BRICS ni wahanga wakubwa wa Western led World kwa mda mrefu, so "maslahi" yao yanaendana bila kujali tofauti zao za kisiasa au kijamii

So anachokifanya Putin Russia, sisi Africa hakituhusu, hata akiua raia wake

Tunachopaswa jali ni "Maslahi" yetu, inapaswa tutoke kwenye utumwa wa kiuchumi, na BRICS ni hatua moja wapo

Kuhusu mahusiano ya Russia (au USSR) na Africa, hujasoma historia?

Russia wamepita viongozi wehu kuliko Putin, lakini nitajie nchi moja ya Afrika iliyotawaliwa au kunyonywa na Warusi? Au Wachina? Au Wahindi?
 
ukweli ni kwamba, hata kama alikuwa rafiki yake wa utotoni, kitendo cha uasi alichokuwa amekionyesha ilikuwa ni tishio la kutomwamini tena na ingekuwa ujinga kama putin asingefanya alichofanya. kwa upande wa putin kwa africa, ukienda kwa kuaminiana hana shida, ila ukienda kwa usaliti au mguu mmoja ukiwa western countries lazima kuna siku utaona makucha yake tu.
 
Viongozi wa Afrika wanaomkumbatia Putin kama kwamba anawathimini wao sana ilihali akiua ndugu zake wa karibu sana na kufuta makaburi ya askari wa Wagner ambao ni warusi kama yeye waliomsiadia sana kwenye hiyo special military Operation ni viongozi wenye upungufu mkubwa sana wa akili. Watu wa Ukraine wako karibu sana na warusi kwa vile wanaongea lugfha moja na wana historia inayoshabihiana sana lakini anawaua bila huruma yoyote. Waafrika nyingi mtakuwa mna thamani gani kwake? Angalia hapa alivyofuta makaburi ya wagner baada ya kumuua Prigozhin. Ni mtu wa aina gani huyo kuheshimiwa na viongozi wetu?


View: https://rumble.com/v3bmx7q-wagner-cemeteries-being-paved-over.html?mref=1psd20&mc=6ztjq
 
Chawa mmagharibi at work
 
To assassinate Putin is next to impossible ndugu yangu. Huyo ni wa kiwango juu sana ktk security technology. Sijui Boris Yeltsin alipekua vipi hata akapata huyo Putin. Hatari sana. Putin has made Russia Great Again.
 
Kama ni kweli Prigozhin ameuliwa (assassinated) , basi muuaji alitaka mpost content kama hii ya mleta mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…