Kuuliza si ujinga, Mtu akifariki watu wanasema Apumzike kwa Amani huwa wanamwambia marehemu au wanamaanisha nini?

Kuuliza si ujinga, Mtu akifariki watu wanasema Apumzike kwa Amani huwa wanamwambia marehemu au wanamaanisha nini?

The Lastdream

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2024
Posts
1,970
Reaction score
4,616
Wakuu ni aje,

Leo naomba kuuliza, kwanini mtu akifariki utaona watu wanaandika RIP au pumzika kwa Amani ndugu fulani au Mr fulani au Mrs fulani.

Hivi huwa wanamwambia Nani?! Marehemu au huwa wanamaanisha nini? Au ni tamaduni tu kama vile kunywa chai asubuhi japo hata usippkunywa haufi!

Wajuzi wa mambo karibuni.
 
wakuu ni aje

mkuu marehemu huwa hajui kitu

Mhu 9:5​

kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
 
kwahyo Haya maneno tunayoyasema Pumzika kwa Amani ni kujifurahisha sisi tu na wala hayana maana yoyote?
ila biblia mara nyingi inasema neno kufa kama “kulala”

Danieli 12:2 BHN​

Wengi wa wale ambao wamekwisha kufa, watafufuka; wengine watapata uhai wa milele, na wengine watapata uhai na kudharauliwa milele.
 
Marehemu Wanajua bhana, kinachokufa ni mwli sio roho zao, roho zao still zinaishi.
marehemu ni mtu aliyekufa.
sasa unaposema kinachokufa ni mwili na si roho zao mbona unatuchanganya?
Kwani mwili si ndio unakamilisha kiumbe ili aitwe mtu? Sasa kama unasema marehemu anakufa mwili si roho na maana ya marehemu ni mtu aliyekufa tuelewe lipi🤣!?
 
NIsipokumywa chai asubuh yan huwa nahis mawenge wenge. Bora ninywe hata kama bila kitu ninywe chai tupu tu, siku itakaa vizuri
ni kweli mkuu. Ila sio universal standard kwamba wote itakuwa hivyo. Kuna wasukuma wanaenda kuchunga alfajiri wanapiga ugali wakutosha. Kuna mimi nPenda juisi, kuna wanaopenda supu n.k. Hayo ni mapendeleo ila tulishafanya kama utamaduni kwa wengi wetu lazima tunywe chai asubuhi.
 
Unaupinga msahafu eti
Hapana mkuu, yeye ndio ajaelewa vyema huo msahafu na vlcontext nzima huyo muhubiri na hiyo sura alikoti huo mstari.

Huyo huyo muhibiri aliesema wafu hawajui neno lolote, mbele kidogo anasema ivi "Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa" (muhubiri 12:7). Sasa kama roho zao zinamrudia Mungu kwanini hao wafu wasisikie wala kujua lolote akati roho zao zipo hai.
 
Unataka nihitimishe vipi nikifa wakati nikifa ndio basi tena ,alie hai ndio anaweza thibitisha aliyekufa amekufa hakuna la zaidi juu yake.
yaani ujanielewa mkuu.
Kama ambavyo wazee zamani walijua radi ni hasira ya mungu ina maana upeo wa kufikiri kwao ulikuwa mwisho.
Kwanini usiseme labda hatujui nini kitakuwepo after kufa? Kwanini umehitimisha kwamba ukifa ni basi hakuna kitu baada ya hapo?
😂😂mbona usiseme sayansi bado haijagundua na ipo kwenye utafiti unaoendelea?
 
marehemu ni mtu aliyekufa.
sasa unaposema kinachokufa ni mwili na si roho zao mbona unatuchanganya?
Kwani mwili si ndio unakamilisha kiumbe ili aitwe mtu? Sasa kama unasema marehemu anakufa mwili si roho na maana ya marehemu ni mtu aliyekufa tuelewe lipi🤣!?
"Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa" (muhubiri 12:7)
 
Back
Top Bottom