Mwanakijiji;
Jana kulikuwa na wawakilisha na wanasheria kutoka Mtandao wa Vyama vya Kisheria.
Sijui niseme nini.
Katiba yetu pamoja na mapungufu yote, bado inatupa uwezo mkubwa sana wa kuleta mageuzi na kuwawajibisha watendaji wabovu, bila hata kwenda kwenye siasa. Jana binafsi nimejiona nasutwa sana nafsi kwamba kwa uvivu wetu tunashindwa kuzielew sheria za nchi yetu zinazotupa haki ya msingi. Si hivyo tu, hata katiba yetu iko wazi.
Ni hakika kuwa wengi hawajui hata katiba ya nchi inasema nini na ni nini nafasi yao.
Hakika tuna safari ndefu lakini inayowezekana kwa matumaini makubwa. Tusaidiane kuiboresha nchi yetu kwa manaufaa yetu na vizazi vijavyo.
Sanctus,
Kwanza pole sana kwa hekaheka ya mkutano wenu; kuandaa hata tafrija ndogo ni kazi kubwa na mwisho wake huwa uchovu mkubwa wa akili na mwili.
Ninasikitika kusema kwamba hayo unayoyaandika, ndiyo yamekuwa yakisemwa na kuandikwa na wasomi mbalimbali kwa nyakati tofauti. Mimi niko kwenye hivi vijiwe vya wasomi wa Kitanzania kuanzia mwaka 1993 na niliyoyasikia na niliyoyaona wakitenda ndiyo yamenifanya niachane kabisa na haya makongamano au mikutano isiyo na mwisho.
Matatizo ya Tanzania yanajulikana na kinachotakiwa ni utekelezaji. Wengine katika kila tulichojaribu kufanya TZ, kumekuwa na ukwamishaji wa ajabu kutoka kwa hao hao wasomi wetu. Inafika mahali unajiuliza hivi neno uzalendo lipo tena kweli kwa hawa wasomi wetu?
Usifikiri watu wako negative kwenye comments zao kwasababu tu hawataki mabadiliko, hapana, ni kwasababu wengi wamekumbana na ujinga mwingi unaofanywa na wasomi kwenye maeneo ambayo ungetegemea mtu hata angeweka uzalendo mbele.
Kuna watu tunawajua kabisa wanakwamisha baadhi ya juhudi za Watanzania wenzao kujiletea maendeleo, lakini ukiwakuta kwenye makongamano wao ndio mabingwa wa kuongelea uzalendo na opportunities zilizopo. Mtu unaweza kuchukia ukamtukana mtu kama huyo kwa unafiki na ukaambulia kesi ya bure.
Mimi nitaunga mkono mara moja wanataalauma ambao wanatekeleza kwa vitendo matatizo yaliyopo. Kwa mfano wa mazingira wanaotumia elimu zao na ujuzi wao kusafisha mazingira au kuwachukulia hatua wanaoharibu mazingira. Madaktari wanaotumia ujuzi wao kuzuia uozo wa kuhamishia wagonjwa wetu kwenda kutibiwa nje badala yake wanatoa ujuzi wao kwa vitendo ili hospitali zetu ziwe bora na ziweze kuwahudumia Watanzania wengi zaidi. Wanasheria ambao wanatumia ujuzi wao kuwafikisha mahakamani wale wanaoliibia taifa letu na pia kuzipinga kwa vitendo sheria mbovu ambazo zinazuia maendeleo.
Leo hii ninavyoandika, kuna Watanzania wengi wako mikoani wakijaribu kutatua matatizo ya Watanzania wenzao kwa vitendo lakini wanakwamisha na wasomi kwenye vyombo vyao mbalimbali kuanzia TRA, TCRA, Wizara, mikoa, wilaya na ofisi zingine zenye mamlaka ambazo ungetegemea hawa wasomi watumie elimu zao kutatua matatizo badala ya kuongezea matatizo.
Mimi nawatakia mafanikio kwenye chombo chenu; kadri watu wengi wanavyoandika hovyo hapa ndio iwe motivating factor kwenu ili mufanikiwe na muweze kutuonyesha sisi wote kwamba tulikuwa wrong. Nitafurahi kupata maazimio yenu ili nijue wapi na wengine tunaweza kuunganisha nguvu.