kwa hali ambayo mjadala wa bandari umefikia,mtu kama JK hakupaswa kukakaa kimya.
hiyo ya kutinga ikulu kimya kimya kwenda kushauri, ni unafiki, umbea,usengenyaji na usukunuku.kwanini asitoe tu msimamo wake hadharani?,anahofia nini?.
haoni kwamba kukaa kwake kimya kunazidi kuamsha mjadala unaomuhisha yeye kama masterminder wa project nzima ya dp world na bandari?.
Kwa kweli JK anatakiwa aseme neno moja tu kwa ajili ya kuliponya Taifa.
Mimi naamini, kwa heshima yake kama Rais mstaafu atasikilizwa na serikali pamoja na wananchi. Atoke hadharani, atumie hekima yake kuweka sawa suala la udini liloibuka. Wakristo na waislam sote ni wamoja tujirekabisha tuache hisia mbaya kwamba wakristo wakitoa maoni tofauti juu ya DPW wanasema hivyo kwa sababu mwarabu ni muislam. Au waislam wakimkubali DPW wanafanya hivyo kwa sababu kampuni ya DPW ni waislam.
Mbona DPW wameajiri hata wakristo. Mfano kwenye ile clip ya Mbeya walipokuwa wanaahidi kutoa Masaada wa msikiti, yule mkalimani wao alisema yeye ni mkristo.
Tukubali kwamba ni haki ya kila mtu binafsi au kikundi cha watu watanzania (kiwe cha kidini au vinginevyo) kutoa maoni na mapendekezo yao kwa kadri walivyojaaliwa na mwenyezi Mungu. Na siyo lazima yafanane, siyo lazima yakubaliwe. Tuvumiliane tunapotofautiana, tusikashifiane kwa misingi ya dini. Hakuna dini inayofundisha ubaguzi na matusi. Zote zinafundisha haki, amani na upendo.
Lakini tukianza kutazamana kwa mrengo wa imani za dini, hatutakuwa na mwisho mwema. Kama nchi, tunajichimbia kaburi la kujizika wenyewe. Of course ndiyo itakuwa furaha ya Dubai kwani atakuwa ametugawa ili atutawale vizuri, hususan atakapofanikiwa kuanza shughuli zake huku tukiwa tumeshindwa kubadilisha vipengele-janja vya mkataba, simply kwa sababu ya ubishani wetu.
Na mjue huu mkataba haurudi nyuma. The best way ni kubadili maeneo mabaya na kuwa makini zaidi kwenye HGA's. Maeneo mabaya baadhi yake ni kuondoa kipengele cha kuwapa bandari zote, muda wa ukomo, uwekezaji uwe wa ubia DPW na serikali (TPA) na mengine kwa mujibu wa wanasheria. Aidha wakati wa kurekebisha serikali iwaalike wabobevu kama kina Prof Shivji n.k. kuja kutoa ushauri. Iwatumie watu wake hawa vizuri hata kama wamestaafu.
Otherwise, we are doomed!