Kuvaa saa enzi hizi za dijitali ni mbwembwe au usharobaro?

mkuu, kwa ke kuvaa saa ni jambo la kawaida kabisa kwa kuwa ke akivaa saa ni kama amevaa bangili-urembo. si unajua siku hz pambo la bangili ni nadra sana kupatikana? tatizo ni kwa wale me wanaovaa bangili hii all day long.

We ni mshamba... na mtazamo wako wa kishamba, trust me or not saa inakamilisha ugentlemen... inaongeza youe value kila ukivaa... siwez acha vaa saa maisha tena za ukweli rolex, edfiece, seiko, tsot
 

katika mavazi ya MWANAUME viatu na SAA YA MKONONI vinaeleza mengi sana......saa ni saa na simu ni simu
 
Kwenye ndege huwa tunatakiwa tuzime simu na kama huna Airplane mode basi kama ni safari ya masaa10 utakuwa hujitambui uko wapi kama huna saa. Nafikiri ni aibu zaidi kuulizia muda kwa abiria mwenzako ndani ya ndege kuliko kuwa na saa yako. Saa ni muhimu na mtoa mada inawezekana hakupata kifungua kinywa akajikuja anatupa uzi ambao ni controversial. Baada ya kupata shule inayotolewa hapa akanunue saa.
 

Mkuu bora ukae kimya tu, inaonyesha wazi kuwa hauzingatii muda, saa ni kitu cha muhimu sana katika maisha, unapoivaa mtu anaweza kukutathmini wewe ni mtu wa aina gani, huwezi kila mara ukatoa simu mfukoni eti unaangalia saa, unaweza ukakosa vingi sana kama katika mkono wako huvai saa,

 
kesho watasema kubeba kamera wakati una simu yenye kamera ni ushamba!
 
Wahenga walinena: Bora unyamaze ili watu wadhani wewe ni mjinga kuliko uongee ili uwathitishie watu kuwa kweli wewe ni mjinga!" kisha wakaongeza" Mwenye busara huongea inapobidi lakini mjinga huongea ilimradi!"
 
Mbona una smartphone hapo na wakati kazi ya simu ni mawasiliano tu???

Kama kuingia mtandaoni utatumia computer.

Kama mziki una redio kwako.

Kwann usiwe na nokia ya tochi?maana yake ni kwamba tofauti na kazi ya kila kimoja kuna mauzo( status).
Au kwann usiuze redio kisa una simu,
 
Ndio maana kukawa na simu na saa hvyo vitu ni vwl tofauti,na istoshe kila binadam ana preference zake mwingne anapenda kuvaa saa,mwngne hapendi sasa kama ww hauwez kuvaa saa acha wengne wavae sio kuanza kuwaponda huo sio huungwana,kama hauna cha kupost bora ukae kmya kuliko kupost vtu vsivyokuwa na maana
 
Mkuu saa inavaliwa kwa malengo mawili, kuonyesha majira, vilevile kupendeza, kama ilivyo nguo, kusitiri mwili na kupendeza vilevile.
Mimi ni addict wa kuvaa saa, nikiisahau nitaomba ruhusa kazini niirudie.
Nisipovaa saa naona ni kama sijavaa chupi au fulana (vest),hata kama nilisahau kuvaa narudi home siendelei na safari.Saa ni sehemu ya mavazi yangu.
 
kesho watasema kubeba kamera wakati una simu yenye kamera ni ushamba!

Na siku hizi wenye simu za camera hujifanya tayari ni maphotographer kumbe ni sawa na wanafunzi wa chekechea kuvaa majoho ya wahitimu wa stashahada na wakajifanya tayari wamehitimu stashahada
 
We ni mshamba... na mtazamo wako wa kishamba, trust me or not saa inakamilisha ugentlemen... inaongeza youe value kila ukivaa... siwez acha vaa saa maisha tena za ukweli rolex, edfiece, seiko, tsot

Tena nikiona saa nzuri roho hunienda mbio ningekuwa na uwezo ningekuwa na saa angalau 10ni kama vile chupi au fulana ya ndani.
 
mleta mada umeshajipambanua wewe ni mtu wa kundi gani, jioni njema.
 
Mkuu una maana na wenye simu zenye radio wasinunue radio majumbani mwao?
 
Sikumbuki mara ya mwisho kuvaa saa na sitegemei kuivaa tena labda nikiwa kwenye chumba cha mtihani nitaibeba na kwenda nayo na baada ya kumaliza kupiga paper nitampa demu wangu avae kama bangili.

:israel:

Kumbe bado wa kusoma wewe, utakapohitimu utajua kwa nini bado tunavaa saa


Tukichepuka huwa tunazima simu sasa tutajuaje muda?
 
Namshangaa mtoa mada, nadhani si mwanamme kamili..ana elements za kike au bila shaka atakuwa shoga huyu!!
Nnachoona hapo ni majungu tu!!
 

Acha majungu kijana! Live ur life!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…