Mwizukulu mgikuru
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 5,715
- 13,739
Wasalam ndugu zangu wana JamiiForums, ni mara nyingine naleta kwenu mada nyingine.
Vitabu vya dini vimekuwa vikituhusia sana tusivunje undugu kwa matatizo au changamoto za hapa na pale zinazotokea aidha kwenye jamii zetu au familia zetu, lakini kumekuwa na sababu nyingi zinazopelekea ndugu kuchukiana na kupelekea kuchukiana maisha na hata wengine kufikia kutokuzikana.
Kwa mfano mimi miaka 10 nyuma niliwahi kupata kupewa kesi mbaya sana ya jinai iliyonifanya nikae gerezani miezi 6 lakini kuna baadhi ya ndugu walikuwa wanashangilia huku wakisema Mwizukulu Mgikuru ndio basi tena mshenzi yule.
Huyo anaeshangilia matatizo yako hujawahi kulala au kula kwake na pia hujawahi kumuomba msaada wa aina yoyote! Sasa ndugu wa aina hii wa nini wakuu? Ipo haja ya kuwa nae?