Kuvunja undugu na ndugu zako wa damu wanaokutakia mabaya ni kosa?

Kuvunja undugu na ndugu zako wa damu wanaokutakia mabaya ni kosa?

ndugu yako akikutakia mabaya kashapoteza sifa za kua ndugu.potezea hao nyumbu
 
Tatizo kama lako limewatokea wengi. Kama ulisimuliwa tu potezea na usikae na vinyongo. Ndugu huwezi kumkimbia hasa yule wa damu. Halafu pia jifunze kubeba misalaba yako. Hakuna mtu anayelazimika kukupigia simu kukupa pole kisa ulienda jela. Hata wewe pia hulazimiki kujihusisha na matatizo yao. Kaa zako kimya kama wana makosa basi Mungu atawahukumu wenyewe. Na wewe kama ulikuwa ukiwadharau ndugu zako basi badilika. Tungesikia upande wa ndugu zako basi tungekuwa kwenye nafasi ya kuwashauri. Story yako haija-balance. WAPENDE NDUGU ZAKO.
 
Sio. Kila unachokitarajia utakipata
Umekosa pole
Achana nao pambana ukipata pesa ndugu watakuja
 
Wasalam ndugu zangu wana JamiiForums, ni mara nyingine naleta kwenu mada nyingine.

Vitabu vya dini vimekuwa vikituhusia sana tusivunje undugu kwa matatizo au changamoto za hapa na pale zinazotokea aidha kwenye jamii zetu au familia zetu, lakini kumekuwa na sababu nyingi zinazopelekea ndugu kuchukiana na kupelekea kuchukiana maisha na hata wengine kufikia kutokuzikana.

Kwa mfano mimi miaka 10 nyuma niliwahi kupata kupewa kesi mbaya sana ya jinai iliyonifanya nikae gerezani miezi 6 lakini kuna baadhi ya ndugu walikuwa wanashangilia huku wakisema Mwizukulu Mgikuru ndio basi tena mshenzi yule.

Huyo anaeshangilia matatizo yako hujawahi kulala au kula kwake na pia hujawahi kumuomba msaada wa aina yoyote! Sasa ndugu wa aina hii wa nini wakuu? Ipo haja ya kuwa nae?
ebu tuambie undugu unavunjwaje
 
Back
Top Bottom