Mkumbuke kuwa tuna stress za kumwaga. Tunarogwa kila kona.Kazini, nyumbani na hata majiani.
Sasa mtu akinywa pombe jana alafu asubuhi akanywa maji unyunyu ukatema. Sasa hapo ni kosa? Maana hajalewa ila unyunyu unatema.
Mnafoka hovyo kama vile sisi ni watoto wenu.
Tunawastahi tu kutafuna Big G Mashwain nyie . Mnanyanyasa sana watu.
Kuingia ofisini bado unanuka pombe, kuna mawili, aidha umekesha unalewa ama umezimua wakati ukija ofini, kwa hiyo umeianza kalenda ya leo ukinywa pombe.
Nilipokuwa boss nishatandika sana viboko walevi kama nyie, ukiwa boss ukafokafoka bila kuchukua hatua, staff wanakuzoea.
Viboko sitandiki kigomvi, natandika kirafiki tena kwa makubaliano, kama ni ubabe na mimi nilikuwa mbabe vile vile na sheria ya mamlaka inanibeba.
Tunakaa mezani tuna negotiate, nakuuliza, 'maonyo yote niliyokupa ya kuachana na ulevi kwanini haujirekebishi, sasa nimekuvumilia nimefika mwisho...
'chagua conditions hizi mbili, 'nikuandikie dissmisal au nikutandike mboko?'
Tena namueleza 'iwe siri yangu mi na wewe pamoja na ofisi'
Na ninamkumbusha athari za kifamilia zitakazotokana na kutimuliwa kwake ama kusimamishwa kazi.
Unakuta jamaa anasema nipige tu mkuu yaishe.
Tukiwa wawili tu, kiboko kinatafutwa kisha mlango unafungwa.
Naburuza mboko hadi mkojo unasogea, ama kutoka kabisa.
Anaondoka ofisini jicho mkoma na harudii kweli, wakawa wamenipachika A.k.a wananiita german.