Kuwa mkweli. Unabadilisha shuka ya kitanda mara ngapi kwa wiki?

Duu..tena umenikumbusha ngoja nikalibadilishe nilikuwa sikumbuki kama linabadilishwaga
 
Inategemea... kawaida siku 2-3. Nikisweat hata kidogo siwezi kulalia tena hilo shuka naona kinyaa. Kama upepo utavuma nikahisi vumbi, lazima nibadilishe. Kama mbebez yupo tukalala kawaida basi siku 2. Tukishiriki linabadilishwa.

Kiufupi siwezi kabisa kuona au kuhisi uchafu. Hata nyumba inadekiwa kila siku no matter what!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa nabadili shuka pale nnapoanza kupiga chafya, ugeni au harufu
 
Wanasema shuka inatakiwa ibadilishwe kila baada ya siku 3[emoji849]
Pia inategemeana na shughuli zinazofanyika hapo kitandani,na joto la dsm kama ni mkulima na kila wakati unapalilia mazao,hata masaa 12 haliwezi kudumu
 
Reactions: amu
Nabadili kila baada ya siku5
sio kwamba linachafuka La hasha! Nachoshwa na muonekano wake
natamani hata Rangi ya chumba niibadili kila baada ya mwezi huwa nachoshwa na mazingira yake yale kila ninapoingia room
Nashangazwaga na baadhi ya wanawake Room kwake hajapanga vitu, shuka kama la getho miezi 6 Nguo zimetupwa tupwa, vipodozi dirishani au viko hovyo hovyo kwenye dressing table, makopo ya liyoisha yanakaa miaka, chini michanga kibao Lakini akitoka Unatetemeka huyu mwanamke mzuri hivi katokea wapi '

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umesema "room mate" badilisha kichwa cha habari.Muulizane nyie mnaoishi kwenye maghetto na kwa wazazi wenu wengine tumeoa wengine zipo washing machine n.k naona umejisahau.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nabadili mashuka kwangu kila siku.
Sio chumbani kwangu tuu ila vyumba vyote nyumbani kwangu.
Kila asubuhi mashuka yanatolewa yanaenda kufuliwa yanatandikwa mengine.
Mkuu ushaolewa nije kukuposa maana wew unanitosha ila mtoa mada hatoshi kuwa mama wa familia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…