Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya harusi ni kazi sana

Aachane na sijui party sijui nini afanye kama ya akina Lulu..
 
Harusi nyingi waalikwa hutoa michango mwishoni mwishoni endelea kuwakumbusha kwa kuwasumbua kwa txt walau moja kila siku.
 
Anamtaka mc garab πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚...anaoa binti wa instagram au bwanaharusi naye ni walewale tu, yaani kashindwa toa 5m anataka ampe mtu 4m kwa ajili yakupiga piga kelele masaa 3 sijui manne.
😳 kwani ndio bei za Mc Gara B izi? saitakuwaje
 
Itakuwa walijua kuwa hawezi kutoa hiyo pesa ila aliwahadaa ili watu watoe michango mikubwa
 
Harusi imeshangwa au ndio basi tena?
 
akili za kuambiwa changanya na za kwako.....ilishantokea kama mwenyekiti......bwana harusi na mkewe mpaka leo hawajanimalia bado.....yaani bwana harusi mpaka nguo aliazima.....wacha kabisa....tulikunywa maji soda mwanzo mwisho...na maharusi wote ni walevi hatareeee....kikubwa ni KANISANI......mengine mbwembwe mfinyanzi....
 
Gharama za harusi ml 10 ad 7.wakati huo wana harusi wanaenda kukaa kwenye nyumba ya kupanga na kazi za kuunga unga
 
Hapo nikutafutiana lawama tu.kama yeye mwenyewe kashindwa kumalizia mchango wake anatemea Nini.πŸ˜€πŸ˜€,Aisee hapo unakazi ya ziada,!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…